Kupwaya kwa uongozi wa CHADEMA

Kweli watz bado sana. Hivi ni kweli mtu kama huyu naye anajihesabu kwamba katoa hoja. Hotuba ya wenje haina shida yoyote. Shida iliyopo ni uelewa wa wana_cuf ni mdogo mno kiasi wanashindwa kutafsiri mambo katika uhalisia wake
 
Tatizo la Chadema ni kugeuza bunge la bajeti kuwa jukwaa la kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015.
 
Ndugu umejitahidi kufafanua lakini hujakumbuka kuwa hoja aliyokuwa anajenga Mh Wenje ni juu ya usiri mkubwa wa baadhi ya vyama vya kisiasa juu ya misaada inayopewa kutoka nje ...nahii ndo hoja ya msingi ambayo wengi wetu hatukuisikia kwa kuwa tumeinyima nafasi kwa kushadadia kipengere cha ndoa za jinsia moja.

 
kaka wewe hotuba umeisika au umeisoma kaka?wacha kupotosha umma,hata mwalimu Nyerere alisema vijana wa leo ni wavivu kufikiri nadhani wewe ni mmoja wapo

wenje tangu amezaliwa hajawahi kuwa makini?.ni kikaza wa dunia
 
nimeona jioni wakati bunge lina ahirishwa na jinsi wabunge wa cuf walivyokuja juu.ukweli chadema wako sahihi na mhe wenje,alikuwa na haki ya kukataa kuomba radhi.nime google vyama vya kiliberali africa,tanzania ni cuf,na vitu waliberali wanachosimamia ni hayo mambo ya ushoga.cuf walipaswa kukanusha,mbona ccm wanaitikadi ni wajamaa ilhali matendo ni ya kibepari?.turejee hotuba ya mhe.wenje hakuna tusi mule cuf wamejitusi wenyewe.
 
Yaani kweli tumefikia hatua ya kubishania milengo ya vyama? Poor politicians! Wapinzani mipasho,serikali mipasho aaaaagh!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
KAKA "BANIAN MBAYA KIATU CHAKE DAWA" CUF wanapokea misaada ya waLIBERAL ila hawataki watu wajue waLIBERAL wana misimamo gani. NA UKIONA HOJA ZAO SI KWAMBA MH WENJE KASEMA UONGO. ILA HAWATAK ISEMWE WAO WANA UHUSIANO NA WATU HAO WAKATI USHAHID UPO... CUF MNAPOKEA MISAADA TOKA KWA CHAMA KINACHOUNGA MKONO USHOGA,USAGAJI NA NDOA ZA JINSIA MOJA MKIAMBIWA MNATOKA MAPOVU MDOMON JAMAN HILI NALO MPAKA UENDE CHUO AU FORM SIX? MBONA ELIMU NDOGO TU YA DARASA LA SABA AMBAYO WENG WENU MNAYO? HATA YA MADRASA TU INATOSHA ACHENI KUPOKEA MISAADA YA HAO MAKAFIRI.
 
All in all ile hotuba kwenye huo uchambuzi wa mirengo ilikuwa sio sahihi hata kidogo. Wenje alitakiwa akubali kuomba radhi na kuondoa vipande hivyo kwani havinamaslahi yoyote kwa taifa.

Haina maana kuwa unapokuwa katika mrengo fulani basi nakubaliana na kila kitu kinachowakilishwa na wengi. Hatuwezi kukubaliana kwa kila kitu, ila katika mambo machache ya msingi.

Pamoja na mapenzi yangu makubwa sana kwa CDM, lakini Wenje amechemsha bab kubwa. CUF walikuwa na kila sababu hata kufanya fujo kuhakikisha kuwa hotuba ile haisomwi.
 
Iwapo Uongozi wa Chadema unadhani mikakati yao ya kuja kuongoza nchi ni kwa kupitia wanachma na washabiki wao tu wataakuwa wanafanya kosa kubwa sana.

Na ktk kufanikisha adhima hiyo wanapaswa kuzingatia lugha wanayotumia, mahali na wakati wa kuyatumia.

Sikutaraji Viongozi makini wanaopanga mikakati ya kupata ridhaa toka kwa Watanzania wote kuongoza nchi waruhusu hadithi za namna hii ziingizwe kwenye hotuba wakati huu na mahali hapa. hizi ni story za majukwaani kwenye kampeni.

Hasa baada ya hali ya hewa kuharibika asubuhi viongozi makini ilikuwa ni kumshauri Wenje aombe msamaha na kuondoa misamiati yake 'after all you have nothing to loose' kuliko kusimamia utetezi wa ukweli unaokukosesha uungwaji mkono wa kundi fulani la watu.

Ni saikolojia ya darasa saba tu kwani CUF huwezi kuitenganisha na maelfu ya wapenzi wake Zanzibar, utachukuaje nchi bila kura za Wazanzibari? ati ukitaraji watu watakuelewa kama unavyoelewa wewe!!
 
CHADEMA inabidi muanze kuuthamini muda wenu kwa kupeleka hoja zenye maana bungeni.

Mheshimiwa Mbowe ameitoa mbali sana CHADEMA kwa misaada itokanayo pamoja na mambeo mengine Club Billicanaz!

Ushoga wenyewe unakoanzia ndio huko huko kwenye vilabu vya pombe vinavyowapa mapato.
 
mleta mada huelewi unachokitetea.

je CUF haipokei pesa toka kwenye vyama vyenyel mlengo wa kishogo.?

ukweli unauma lakini ndio mtaji wa chadema.!!
 
Msimshangae, hao ndo watanzania wenyewe, unafikiri kwa ujinga huu wa ccm bado wangeendelea kutawala kama wasingekuwa na mtaji wa majuha kama muanzisha mada. safari bado ni ndefu na yenye misukosuko kwa wanaofikiri kwa makengeza. mungu tuokoe
 
kidogo kuna mantiki tunataka chama ambacho kitajijenga kwa kutoa hoja ya malengo yake kiasi kwamba hata mwanachama wa chama kingine aone siku ya kupiga kura kuwa hawa watatupeleka mbele kwa hoja zao na awapigie kura.
hoja ya leo bungeni ni uchambuzi wenye lengo la kupaka matope na hakuna chama kinachoweza kuvumilia kupakwa matope mbele ya umma kinyamaze. kwa mda mrefu vyama vyetu vinapenda kujinadi kwa kusema fulani anashirikiana na fulani kitu ambacho si hoja ya chama kingine kupigia kampeni.

tuko na matatizo mengi hivyo tunataka chama kitakachojikita katika kutuambia kitatatuaje matatizo yanayotukabili. kejeli kama hizi hazikijengi chama bali zinakibomoa maana ukiitamka wasiofikiri watashangilia hapohapo, lakini wanaofikiri ambao ndio wengi watakaa kimya ila watakudharau mwisho wa siku utakuja kujiuliza mbona nilikuwa nashangiliwa lakini nimeanguka.

jengeni chama kwa kuweka mikakati ya kubuni sera za kukomboa watanzania na hizo ndizo mzinadi hadharani achaneni na sera za kujiimarisha kwa kushambulia vyama vingine. weka mikakati mtangaze sera zenu wakati wote mfano sera za kupambana na mafisadi sio lazima mtaje watu lakini muwaahidi wananchi mkipewa nchi mtafanya nini kwa mafisadi na nini matokeo yake kwa wananchi, waelezeni watu sera yenye mvuto ya kufuta kodi kwenye vifaa vya ujenzi na mnasema wazi tunaitaka serikali iliyoko madarakani ifute kodi hiyo na sisi tukiingia tutafuta ili kama chama tawala kitaamua kuchukua hiyo sera sio ninyi kupinga bali itakuwa vema na wananchi watajua chama fulani ndio kimetukomboa.

yapo mengi ya kujikita nayo ambayo yatawashawishi watanzania walio wengi kuwaunga mkono maana mtakuwa mmewagusa. jiulize hii hoja ya CUF na ushoga itawaongezea wafuasi kiasi gani. busara inahitajika kujiepusha na mtizamo wa vurugu mbele ya wananchi. wekeni dira ya jinsi gani mnataka kushawishi watanzania wawakubali alafu ndio mtafute hoja kupitia hiyo dira yenu kwa kuangalia dira itakayowafanya mshangiliwe majukwaani na siku ya kupiga kura muonekane mashujaa. tafadhali tafuteni mbinu ya kukua kwa haraka maana maisha yenyewe haya mafupi tunataka mabadiliko wakati wetu ili maisha yetu yaboreke tukiwa bado na nguvu zetu


bora tubaki maskini kuliko kubariki ushoga na usagaji,suala hili lilishasemwa na ccm bila kutaja chama watu wakajua ni cdm mpinzani wake mkuu. cdm leo wamewaambia cuf kuwa wale waliofunga ndoa nao wanawasema kw mafumbo washituke, sasa ubaya wao uko wapi

pili yale yalikuwa maneno ya utangulizi katika hotuba yake kabla ya kuanza kuchambua bajeti, kumbuka hili n jambo la msingi watz tulijue kwani ni sera ya mambo ya nje ya cuf,. kama cuf watashika dola watahalalisha ufedhuli na uchafu huo kwasababu watu wanaoshirikiana nao wameukubali uchafu huo katika katiba za vyama vyao,je wao wataukataaje iliali fedha wanapokea huko?
 
Uongozi wa juu cdm ndiyo tatizo unaruhusu mambo yasiyona tija kuingizwa kwenye hotuba yao, mm chadema nafananisha.na.wanamazingaombwe waliokiwa wakitujaza mashuleni kutuonyesha maajabu na michezo mbalimbali kimbe ni uwongo tuu
 
Mimi ni mpenda mageuzi. Kuna muda niliamini kwa nguvu kabisa kuwa uongozi wa Chadema unaweza kufanya kazi nzuri ya kukiongoza chama hadi kuchukua nchi na kuleta mabadiliko tunayoyataka. Lakini kadri siku zinavokwenda ndiyo nagundua udhaifu wa uongozi wa Chadema.
Leo bungeni imesomwa hotuba ya ovyo kabisa toka Chadema na kuleta mtafaruku mkubwa bungeni. Humo bungeni walialikwa wanafunzi wa vyuo na kushuhudia Wenje akisoma hotuba ya kijinga kabisa ambayo haina tija kwa Taifa letu wala kwao.Unaongelea maneno ya kuudhi kama ushoga kukilinganisha kikubwa kama CUF unategemea nini? Wana CUF na wengineo watakupenda kweli? What was the strategy kuleta upuuzi ule? Kama Dr. Slaa ndio umakini wake umeishia pale basi ujue nchi hii itaongozwa na CCM milele, mark my words. Kwani najua Dr. Slaa kama Katibu Mkuu aliipitia hotuba ile na kuipa baraka zake. The same goes with Mbowe. Haiwezi kusomwa hotuba bungeni bila ya wao kuipitia. Na kama hawakuipitia then hawafai. Na kama wameipitia na kuipa baraka zao basi pia hawafai.Mkiwa na viongozi kama Wenje ambao mnataka siku moja waongoze nchi, then you have another think coming.
Wake up,Slaa and Mbowe: Chadema kinaondoka! Tafuteni watu makini kwenye nafasi za uongozi ili muendelee. Chadema hakipendwi kwa sababu ni chama makini, bali kwa sababu watu wameichoka sana CCM, lakini CCM ni makini zaidi na wana mikakati mikubwa kuliko Chadema kwa mbali sana. We angalia hotuba za CCM bungeni uje ulinganishe na za Wenje na mambo ya ushoga wapi na wapi. As Prof. Muhongo said the other time hotuba za upinzani zinatakiwa zije na alternative solutions kwa matatizo ya taifa letu lakini si kuja na porojo tu zisizo na hoja yoyote. Soon the people will see thru Chadema and call your bluff. We need a strong and competent opposition!

Hivi kazi ya vijana nchini nini? na hasa wale wenye hata uwezo wa kusoma na kuandika kama wewe pepo(nisamehe sina namna nyingine ya kukwita umenikera sana nakuapia ungekuwa mbele yangu ningekutwanga ngumi) umenikera kweli ile hotuba umeielewa wewe? mimi sasa ninachokiona hili taifa asilaumiwe yeyote kama upeo wetu ndio huu, tangu lini facts zikawa utumbo kwa waelewa? sasa ikibidi lolote mungu atupe watz kama pigo watakaobahatika watakuja kujenga nchi naona vijana wasasa hatuwezi kuchambua mambo kwa mustakabali mwema wa nchi yetu ila ushabiki. hivi kweli hotuba ya wenje imekuwa tatizo sana zaidi ya yule jamaa wa kigoma mjini aliyetukana watz bungeni na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. we are cursed!!!! na mimi nasema na hii laana izidi tu kututafuna watz no body cares....watoto wetu watakuja jifunza kwa upuuzi huu, fikiri brooooo tena wewe haki ya mungu ungekuwa karibu nami sidhani kama tungeishia pazuri kimtazamo..
 
Mimi ni mpenda mageuzi. Kuna muda niliamini kwa nguvu kabisa kuwa uongozi wa Chadema unaweza kufanya kazi nzuri ya kukiongoza chama hadi kuchukua nchi na kuleta mabadiliko tunayoyataka. Lakini kadri siku zinavokwenda ndiyo nagundua udhaifu wa uongozi wa Chadema.
Leo bungeni imesomwa hotuba ya ovyo kabisa toka Chadema na kuleta mtafaruku mkubwa bungeni. Humo bungeni walialikwa wanafunzi wa vyuo na kushuhudia Wenje akisoma hotuba ya kijinga kabisa ambayo haina tija kwa Taifa letu wala kwao.Unaongelea maneno ya kuudhi kama ushoga kukilinganisha kikubwa kama CUF unategemea nini? Wana CUF na wengineo watakupenda kweli? What was the strategy kuleta upuuzi ule? Kama Dr. Slaa ndio umakini wake umeishia pale basi ujue nchi hii itaongozwa na CCM milele, mark my words. Kwani najua Dr. Slaa kama Katibu Mkuu aliipitia hotuba ile na kuipa baraka zake. The same goes with Mbowe. Haiwezi kusomwa hotuba bungeni bila ya wao kuipitia. Na kama hawakuipitia then hawafai. Na kama wameipitia na kuipa baraka zao basi pia hawafai.Mkiwa na viongozi kama Wenje ambao mnataka siku moja waongoze nchi, then you have another think coming.
Wake up,Slaa and Mbowe: Chadema kinaondoka! Tafuteni watu makini kwenye nafasi za uongozi ili muendelee. Chadema hakipendwi kwa sababu ni chama makini, bali kwa sababu watu wameichoka sana CCM, lakini CCM ni makini zaidi na wana mikakati mikubwa kuliko Chadema kwa mbali sana. We angalia hotuba za CCM bungeni uje ulinganishe na za Wenje na mambo ya ushoga wapi na wapi. As Prof. Muhongo said the other time hotuba za upinzani zinatakiwa zije na alternative solutions kwa matatizo ya taifa letu lakini si kuja na porojo tu zisizo na hoja yoyote. Soon the people will see thru Chadema and call your bluff. We need a strong and competent opposition!

Aisee wewe ndiye MJINGA na MPUMBAVU wala si hotuba ya Wenje (kambi ya upinzani) au viongozi wa CHADEMA!!!.

Baada ya hii nikuulize maswali ma2; Mosi, umeisoma hotuba ya Wenje mwanzo mpaka mwisho? Swali la pili
umeielewa logic iliyomo humo? Kwa nini watanzania(hasa wewe) hatupendi kusema na kuusikia UKWELI? Na kwa nini hawa jamaa wabunge wa CUF wakisaidiwa na kiongozi wa kikao cha leo Bwana JOB NDUGAI na baadhi ya wabunge wa CCM waliamua kuvuruga kikao kwa makusudi?.....Hapa mkuu sikubaliani na wewe, una tatizo,umepwaya kama walivyopwaya wabunge wa CUF leo...pole sana!

HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SI KULETA VURUGU/FUJO!!
 
Unajua kupenda sana ni hatari,hata mwanamke akiwa chongo utasema ni makengeza,lkn kwa utafiti wangu wa harakaharaka,nimegundua wanaotetea upuuzi huuu ni wa kanda ile ya Mweshimiwa NASARI aliyetaka wajitenge na JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.wanashindwa kujua makosa yao,sisi na maswala ya USODOMA NA GOMORA na CUF wapi na wapi,nyinyi ni wa upinzani,mututetee kwa mambo ya msingi,muwabane hao munaowaita ni mafisadi !!!.
 
Back
Top Bottom