Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,554
- 113,736
Wanabodi,
Jana Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa aliliambia Bunge kuwa kupungua kwa mizigo bandarini Dar, kumechangiwa, pamoja na mambo mengine, na mdororo wa uchumi wa dunia, na chaguzi za majirani zetu wanaotumia bandari ya Dar es Salaam; hivyo wafabiashara walipunguza kuagiza mizigo! .
Katika kuwahakikishia Watanzania kuwa bandari ya Dar es Salaam itarejea katika hali yake ya kawaida ya kumhudumia mizigo mingine, Waziri Mkuu amesema serikali ya Tanzania imepokea barua kadhaa kutoka serikali za nchi majirani zetu waliokuwa wakipitisha mizigo yao bandari ya Dar es Salaam kuwa sasa wataendelea kupitishia mizigo yao yote bandari ya Dar es Salaam! .
Jee ni kweli barua hizo zipo, na jee kama hakuna tatizo lolote, iweje nchi hizo zilete barua?!. Kwani zilisimamisha kupitishia mizigo yao bandari ya Dar es Salaam hadi zile teacher barua kuwa sasa zitaendelea kupitishia? !. Kuna Uwezekano wa Bunge kuwa limedanganywa tuu ili kuwahadaa Watanzania kuwa there is nothing wrong with kupungua mizigo bandari ya Dar es Salaam, and serikali ya Tanzania has nothing to do with that situation bali ni mdororo wa uchumi na siasa za nchi Jirani?!.
Tena wabunge makini waombe barua hizo ziletwe bungeni ili na sisi akina Tomaso, tuzione! .
Bandari ni moja za pillars za uchumi wa taifa na mapato ya nchi hii, hivyo suala la kupungua kwa mizigo bandarini ni very serious, sensitive na critical issue inayohitaji majibu serious na credible na sio majibu rahisi kwa maswali magumu huku majibu mengine yakiwa ni majibu ya kisiasa tuu!.
Hoja kuu ya kupungua kwa mizigo bandarini Dar ni wasafirishaji wa mizigo waliokuwa wakipitishia mizigo yao bandari ya Dar es Salaam, kuamua kuihama bandari ya Dar es Salaam na kupitishia mizigo yao bandari ya Mombasa na bandari nyingine hadi Beira kwa "sababu fulani! " ambayo haitajwi au inakwepwa! .
Wakati sisi bandari yetu mizigo inapungua, bandari za wenzetu mizigo inaongezeka!, sababu ingekuwa ni mdororo wa uchumi wa dunia, then kote mizigo ingepungua direct proportional na mdororo wa uchumi! .
Kubwa kuliko ambao ni kama uongo wa mchana kweupe ni hizo barua zinazodaiwa kuandikiwa na serikali jirani kutoa hakikisho kuwa mizigo yao yote itapitia bandari ya Dar es Salaam! .
Maswali ni. ..Hiyo mizigo iliyopungua ni mizigo ya serikali hizo hivyo serikali hizo zimeiandikia serikali ya Tanzania kuihakikishia kuendelea kupitishia mizigo yao yote bandari ya Dar es Salaam? !.
Kama mizigo ni ya wasafirishaji binafsi, watu, mashirika na makampuni ambao wanafanya cost/benefits assessment na kuamua kukimbia bandari ya Dar es Salaam na kutumia bandari nyingine!, hivyo hizo barua za serikali zao, zitawalazimisha wasafirishaji hao kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa lazima hata kama sio cost effective?!.
Kwanini viongozi wa Serikali wanakwepa ku deal na chanzo halisi na kisababishi cha kupungua kwa mizigo bandarini Dar na badala yake wanatafuta visingizio vya mdororo wa uchumi wa dunia na hadi ahadi hewa?!.
Kama mizigo imepungua kwa mdororo wa uchumi wa dunia, hiyo mizigo kutoka hizo nchi walizotuandikia barua itatokea wapi?!, au wao ndio uchumi wa dunia waliamua uchumi wa dunia udorore sasa wameurekebisha hivyo wametuhakikishia mizigo? !.
Kama hatuta deal na chanzo halisi (the root cause) ya kushuka kwa mizigo bandarini Dar na kuukata huo mzizi wa fitna, muda wa sababu za visingizio utapita bila mizigo kuongezeka!, muda huo ukifika, viongozi wetu watatueleza nini? ! .
Hitimisho.
Hili ni swali la uwezekano (posibility) wa Bunge letu tukufu kudanganywa na tafadhalini sana msiojua lugha, sijasema Bunge letu limedanganywa! . Mawazo yangu yananiambia sababu za kupungua mizigo bandarini Dar zipo na zinaeleweka na sio hizi zinazoelezwa!, na hata mashaka ya kuwepo barua toka nchi hizo!.
Kwa hivyo kama ikitokea hizo sababu zilizotolewa bungeni ndizo sababu zenyewe halisi na barua hizo pia zipo, then itakuwa Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, hajalidanganya Bunge letu tukufu bali Pasco wa JF ndie aliyedhania tuu kuwa Waziri Mkuu Amelidanganya Bunge kutokana na sababu alizoelezwa huyu Pasco ni tofauti na zilizoelezwa bungeni hivyo itakuwa Pasco ndiye alidanganywa na Waziri Mkuu kasema ukweli! .
Hili likifanyika Pasco atarejea na uzi mwingine wa sababu alizoelezwa yeye za kupungua kwa mizigo bandarini Dar es Salaam na sababu hizo zitalinganishwa na zile zilizotolewa bungeni kisha "the time will judge the truth! ".
Nawatakia Furahi Dei Njema! .
Ijumaa Karim !.
Pasco.
NB. Wataalam wa sheria, hivi kuuliza swali kama kuna uwezekano wa kiongozi fulani amedanya, ikitokea kiongozi huyo hajadanganya! linaweza kuwa ni kosa kwa muuliza swali? !.
Pasco