Kupungua kwa utani na shemeji

Kupungua kwa utani na shemeji

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,104
Reaction score
1,924
Bila shaka mtakubaliana nami,siku hizi utani na shemeji umeenda unapungua ukilinganisha na miaka 7 iliyopita,ilikuwa mpaka unamwita shemeji 'wife' au 'husband' na haikuathiri kitu.Kwa hali ya sasa naona kabisa shemeji yako atakuwa kama mama mkwe/baba mkwe,na wakwe watakuwa kama shemeji zetu
Pazia 3
 
Mbona shemeji poa tu. Kizuri kula na nduguyo.
 
tangu nyimbo ya hainaga ushemeji tunakuga kuwa namba moja on trending
waliooa na wenye uhusihano rasmi wakashtuka

mipaka ikawekwa na ukuta kama wa machimbo ukajengwa
 
Hii imesababishwa na jinsi Ulimwengu unavyokwenda sababu ni wachache wanaoweza kustahmili ule utani ukabaki kuwa utani kama ilivyokuwa zamani walio wengi hawachelewi kutaka kuugeuza kuwa kweli.
 
Basi tuu woga wa kizazi cha sasa. Mbona awali kulikuwepo na wimbo wa "shemeji, shemeji huku mwazima taa"
na utani ulikuwepo tu. Tena hiyo ya mambo ya "silencer" ndio mbaya maana watu wanazuga kuogopana kumbe...
wakikutana chobingo ni balaa tupu
 
Kwa kizazi hiki hapana kuruhusu mazoea ya kijinga jinga eti kisa ushemeji, dunia inaenda kwa kasi sana.

Bora kuishi na mwanamke/mwanamme kwa tahadhari kubwa maana siku hizi mashemeji wengi hawaogopi kuvuana nguo.
 
Back
Top Bottom