Mgoyangi
Senior Member
- Feb 6, 2008
- 184
- 9
Mtaalamu adai Uganda ndiyo inayolihujumu Ziwa Victoria
Paul Mabuga, Mwanza Mei 7, 2008
Sato wamepungua kwa karibu asilimia 80
KUPUNGUA kwa kasi kwa kina cha maji katika Ziwa Viktoria hakusababishwi tu na mabadiliko ya tabianchi (climate change) bali na kuanzishwa kwa mabwawa ya kufua umeme nchini Uganda, utafiti mpya umeonyesha.
Kwa kiasi kikubwa kupungua kwa maji ya kina cha Ziwa Viktoria kunatokana na shughuli za binadamu na si mabadiliko ya tabianchi. Na hii ni baada ya Uganda kukiuka kanuni za matumizi ya maji ya Ziwa hilo, anasema mtafiti kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Yustina Kiwango katika taarifa ya utafiti wake.
Kwa mujibu wa ripoti ya mtafiti huyo, baada ya Uganda kujenga Bwawa la Kiira mwaka 2000 na hivyo kuwa na mabwawa mawili ya kuzalisha umeme katika mji wa Jinja, jingine likiwa ni lile Nalubaale ( zamani Owen Falls), ilitumia maji kwa wingi kinyume cha makubaliano yake na Misri yaliyofikiwa mwaka 1957 kuhusu matumizi ya maji ya Ziwa Viktoria.
Kulingana na utafiti huo, mabwawa hayo yamekuwa yakifyonza maji kutoka Ziwa Viktoria katika kiwango cha asilimia 20 hadi 50 ambacho ni juu ya kile kilichokubaliwa na nchi hizo mbili. Ni kutokana na hali hiyo, kina cha maji katika Ziwa Viktoria kilipungua kwa mita mbili na nusu kwa kipindi cha kati ya mwaka 2000 hadi 2006.
Serikali ya Uganda katika miaka ya 1990 ilitoa kipaumbele katika upanuzi wa huduma ya ugavi wa umeme kama njia ya kukabiliana na umasikini na kuinua uchumi hususani katika maeneo ya vijijini ambako asilimia 90 ya wananchi wanaishi.
Chini ya mpango huo iliamuliwa kuwa Bwawa la Nalubaale lipanuliwe na kuzalisha zaidi umeme kutoka uwezo wa megawatt 180 na kufikia megawatt 380. Bwawa la Kiira lilianza kuzalisha umeme mwaka 2000 kwa uwezo wa megawatt 200.
Kiwango anaeleza katika utafiti wake kuwa mapitio ya mwenendo wa mvua kwa karibu miaka 100 katika eneo la Ziwa Viktoria na vyanzo vyake, yanaonyesha kuwa, hali ya hewa inaweza kuwa inachangia uhaba wa mvua na kupungua kwa kina, lakini si katika kiwango kikubwa kama hicho na hivyo sababu pekee kuwa ni mabwawa haya mawili ya Jinja .
Katika utafiti huo uliosimamiwa na Eric Wolasnki wa Chuo Kikuu cha Cook cha Australia, Kiwango anaonyesha kuwa kupungua huko kwa kina cha Ziwa Viktoria kuna athari kubwa kwa wananchi wanaolitegemea Ziwa hilo kwa ajili ya kipato na chakula, na hivyo kuifanya hali hiyo kuwa hatari kwa maisha ya watu hao. Zaidi ya watu milioni tatu katika Afrika Mashariki huendesha maisha yao kutokana na Ziwa Victoria.
Ufuatiliaji wa takwimu za miaka zaidi ya sita katika Rasi ya Mlaga unaonyesha kuwa samaki wa asili wa ziwa hilo hususan Sato, wamepungua kwa karibu asilimia 80. Hali hiyo, kwa mujibu wa utafiti huo, inasababishwa na kukauka kwa ardhioevu ya Mirutende ikiwa ni matokeo ya kupungua kwa kina hicho.
Ardhioevu ya Mirutende (papyrus wetlands) hutumiwa na samaki wa asili wa Ziwa Viktoria kwa ajili ya kujificha wakati wanapowindwa na pia kama sehemu ya kuzaliana. Samaki hukulia katika maeneo hayo wakila wadudu na mimea iliyopo katika eneo hilo.
Maeneo ya ardhioevu ya Mirutende, kwa mujibu wa utafiti huo, ina hewa ndogo ya oksijeni, kiasi ambacho samaki wakubwa kama Sangara, ambao hula samaki wadogo, hawawezi kuishi na kuwashambulia samaki hao katika maeneo hayo. Pia Mirutende huchuja kemikali zinazoingia ziwani kutoka viwandani. Mimea hiyo imekauka baada ya ziwa kupungua kina.
Ni rai ya Kiwango kwamba maisha ya watu kando kando ya Ziwa Viktoria yanategemea ardhioevu ya Mirutende, na anatoa wito kwa Serikali na mamlaka katika ukanda wa ziwa hilo, kuliangalia suala hilo na kuja na mikakati madhubuti ambayo itadhibiti suala la kupungua kwa kina cha maji katika ziwa hilo.
Lakini wakati utafiti huo unawanyooshea kidole Waganda, lakini pia pameibuka tatizo jingine; nalo linahusu mradi wa kutoa maji Ziwa Viktoria, katika eneo la Ihelele, wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza, kwenda katika miji ya Kahama na Shinyanga ambao kwa sasa upo katika hatua za kukamilika.
Mtafiti huyo anaamini, hata hivyo, kwamba kwa Watanzania kuna nafuu ya hoja; kwani mradi huo utakuwa ukifyonza meta za ujazo 80,000 kwa siku, kiwango ambapo ni karibu mara 300 ikilinganishwa na kinachofyonzwa na mabwawa mawili ya umeme ya Uganda ya Nalubaale na Kiira ambayo huchota jumla ya meta za ujazo 25.920,200 kwa siku.
Mradi wa kutoa maji Ziwa viktoria kwenda miji ya Kahama na Shinyanga unatarajia kuwanufaisha wananchi wapatao 420,000 baada ya kukamilika, kiwango ambacho baadaye kinatarajiwa kufikia watu milioni moja katika kipindi cha miaka 20 ijayo.