Sisi wenye watoto wanaosoma nje ya nchi tunasikitika sana kwa hali inayotisha kwa kuporomoka kwa kasi ya kutisha kwa shillingi ya Tanzania dhidi ya Dollar ya Marekani. Leo hii dollar moja ya Kimarekani CRDB inauzwa Tshs.2339. Sasa hivi inatuchukua fedha nyingi sana za Kitanzania ili kupata dollar ya kulipia gharama za watoto wetu wanaosoma ng'ambo. BOT chukueni hatua za haraka kuinusuru hali hii.