Ikiwa Deni la Taifa limeongezeka Kwa 5 Trillion kutokana na kushuka Kwa thamani ya Tshs, Mwigulu una maono Gani?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
17,697
27,163
Salaam, Shalom!!!

Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Nchemba amedai kuwa, deni la Taifa limeongezeka Kwa zaidi ya Trilioni 5 kutokana na kuporomoka Kwa thamani ya Shilingi.

Jambo Hilo Hilo la kuporomoka Kwa thamani ya pesa yetu ya kitanzania( Tshs) ndiyo Hasa inafilisi wafanyabiashara kariakoo na Mahali pengine nchini.

Utakuta mfanyabiashara ana mtaji wa milioni 800 Kwa Mfano, kutokupatikana Kwa Dola na kupatikana Kwa dollar Kwa shilingi 3000 Kwa dollar Moja mtaani, kutapunguza mtaji wa mfanyabiashara na kusababisha apoteze kiwango Cha Mzigo ambacho angenunua ikiwa dollar ingekuwa unapatikana Kwa 2300.

Kwa namna Moja au nyingine, wizara ya Fedha inahusika Moja Kwa moja kuleta shida hiyo Kwa kuendekeza mikopo Kila kukicha.

Waziri Mwigulu una maono Gani kuhakikisha nchi inalipa madeni haya na kupunguza mikopo?

Waziri Mwigulu, una maono Gani kuhakikisha pesa yetu ya Tshs inaimaika kama ambavyo pesa yetu ya kitanzania enzi za Mwl Nyerere, Dola Moja ya kimarekani, ilibadilishwa Kwa Tshs 10 pekee? Mbona shilingi yetu inazidi kuporomoka?

Narudia tena, Waziri Mwigulu ni liability Kwa Uchumi wetu, mtu sahihi Kwa wakati huu ni Mh Kimei.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
 
Magufuri alidhibiti hata wakati wa Korona mambk yalienda,,lakini tukamnanda Jiwe na wazirinwake wa fedha Dr mpango..sass tumepata wasikivu wanatekeleza tunachotaka
Usitusingizie,

Hatukuwahi kuwachagua sie,

Ni ghafula tu, kunasikia aliyekuwa kiongozi wa Uvccm ni waziri wa Fedha.
 
Halafu Eti ana PHD!!

Kweli waziri kudhani kuwa utapata Kodi Kwa kutoza akiba za wananchi walizotunza bank kupitia muamala na kutoza line za simu ni uchumi huo?
PhD yake ni ya darasani au ya kupewa?
 
Salaam, Shalom!!!

Waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Nchemba amedai kuwa, deni la Taifa limeongezeka Kwa zaidi ya Trilioni 5 kutokana na kuporomoka Kwa thamani ya Shilingi.

Jambo Hilo Hilo la kuporomoka Kwa thamani ya pesa yetu ya kitanzania( Tshs) ndiyo Hasa inafilisi wafanyabiashara kariakoo na Mahali pengine nchini.

Utakuta mfanyabiashara ana mtaji wa milioni 800 Kwa Mfano, kutokupatikana Kwa Dola na kupatikana Kwa dollar Kwa shilingi 3000 Kwa dollar Moja mtaani, kutapunguza mtaji wa mfanyabiashara na kusababisha apoteze kiwango Cha Mzigo ambacho angenunua ikiwa dollar ingekuwa unapatikana Kwa 2300.

Kwa namna Moja au nyingine, wizara ya Fedha inahusika Moja Kwa moja kuleta shida hiyo Kwa kuendekeza mikopo Kila kukicha.

Waziri Mwigulu una maono Gani kuhakikisha nchi inalipa madeni haya na kupunguza mikopo?

Waziri Mwigulu, una maono Gani kuhakikisha pesa yetu ya Tshs inaimaika kama ambavyo pesa yetu ya kitanzania enzi za Mwl Nyerere, Dola Moja ya kimarekani, ilibadilishwa Kwa Tshs 10 pekee? Mbona shilingi yetu inazidi kuporomoka?

Narudia tena, Waziri Mwigulu ni liability Kwa Uchumi wetu, mtu sahihi Kwa wakati huu ni Mh Kimei.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Kwa nini unapendekeza mtu unayemtaka???Mbona hupendekezi Paramamba Kabudi,Peter Serukamba,Biteko au Bashir Ally.
 
Nchi haiwezi kuwa na "exchange rate peg'' kweny pesa yake , wenzenu wanaweka vingingi ili iwe fixed kwa vile wana uchumi mkubwa nyie kila siku kuimport lazima thamani ishushe la sivyo hampati bidhaa kutoka nje.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom