Kuporomoka kwa magazeti ya Rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuporomoka kwa magazeti ya Rostam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Oct 8, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari za kuaminika kutoka kampuni ya uchapishaji wa magazeti ya New Habari inayomilikiwa na Mbunge wa Igunga Rostam Aziz zinasema kwamba gazeti la kila siku la Mtanzania limeporomoka mauzo kiasi kwamba mhariri wake Danny Mwakiteleko ameondolewa katika mabadiliko makubwa yaliyotangazwa mapema mwezi huu.

  Kwa wanaomfahamu Mwakiteleko, kuporomoka kwa Mtanzania kimauzo hakuingii akilini kabisa -- hasa kutokana na umahiri wake – ikikumbukwa kwamba miaka kadha iliyopita alipokuwa mhariri wa gazeti la Majira aliweza kuliboresha gazeti hilo hadi kufikia kiwango cha kuwa mpinzani mkubwa wa gazeti la Nipashe la Reginald Mengi.

  Mwakiteleko sasa kapewa wadhifa wa kuwa Naibu mhariri Mkuu wa magazeti ya New Habari, hatua inayoonekana kama kumpandisha cheo. Lakini habari za uhakika ni kwamba kaondolewa kwa agizo kutoka kwa mmiliki, Rostam, baada ya kuona mauzo yanaporomoka sana tangu ashike gazeti hilo takriban miaka miwili iliyopita.

  Ilikuwa ni wakati Rosemary Mwakitwange akiwa CEO wa kampuni na alimuajiri kutokana na umahiri wake na kwa mshahara mkubwa sana. Kuna baadhi wanasema Mwakiteleko alibadilika baada ya kuondoka kwa Rosemary ambaye alikosana na Rostam kuhusu suala la mwelekeo na sera za magazeti ya New Habari hasa katika masuala ya kundika habari za ufisadi.

  Habari zinasema kwamba Rostam alimwambia Mhariri Mtendaji Muhingo Rweyemamu amuondoe Mwakiteleko kama mhariri wa Mtanzania na atafute pa kumweka, hivyo akaamua kumweka kuwa naibu wake.

  Gazeti hilo, lililojijengea sifa kubwa miaka ya nyuma sasa linapitwa na karibu magazeti yote ya Kiswahili ya kila siku na sasa hivi meza nyingi za kuuzia magazeti hapa Dar halionekani. Linaanza pia kutishiwa na gazeti jipya la Jambo Leo ambalo ninakuja juu kwa kasi sana.

  Kuporomoka kwa Mtanzania (kama ilivyo kwa gazeti la kila wiki la RAI) linatokana na msimamo wake kuhusu masuala ya ufisadi – lilikuwa linajitambulisha sana na wale wote wanawatetea mafisadi – kwa bayana, lakini mara nyingi kwa ujanjaujanja tu. Inadaiwa kuwa stori nyingi za ukurasa wa mbele zilikuwa zinatokana na agizo la Rostam mwenyewe au washauri wake -- kama vile Salva Rweyemamu.

  Mara nyingine stori hizo huwa zinaletwa nzima nzima dakika za mwisho kabla ya kwenda mtamboni na hubandikwa zilivyo. Mwakiteleko alikuwa akiridhia hivyo kwa sababu mbili – agizo kutoka juu, na kulinda mshahara wake mkubwa.

  Kwa hivyo ni kitu cha kushangaza kuona Rostam amemgeuka Mwakiteleko ili hali yeye mwenyewe ndiyo sababu ya uzorotaji wa gazeti.

  Lakini kuna maelezo mengine tofauti – kwamba wahariri wengi wa magazeti ya New Habari, hususan Mtanzania, Mtanzania Jumapili na RAI (kama vile Balile, Manyerere, Munyunku, Matinyi, Sarah Mosi, Mayage n.k.) hujipendekeza tu kwa Rostam katika kuandika stori wanazofikiria zitampendezesha yeye na zile wanazoona zinaweza kumsafisha katika matatizo yake yanayomuandama – hata kama ni kuwachafua watu wengine.

  Kwa vyovyote vile, hali hii imeathiri sana magazeti hayo. Nafasi ya Mwakiteleko, Muhingo kamteua Balile kuwa mhariri wa Mtanzania, katika hatua ambayo wengi wanaona ni kuzidi kulididimiza gazeti hilo.

  Habari zinasema kwamba kama Mwakiteleko alikuwa anatetea mafisadi kiujanjajanja, basi Balile atafanya hivyo kwa bayana kabisa.

  Tungoje tuone.
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii habari mbona ipo ipo tu?, Rosemary Mwakitwange bado ni CEO wa New Habari cop.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  After all, hata yakiporomoka, who cares!.

  Kuna magazeti mbadala meengi sana, ambayo yamejenga Heshima kubwa ya uandishi uliotukuka!

  Hatutaki magazeti ya kuwapamba watu fulani na kuwaponda wengine, na yanayoandikwa kwa maelekezo ya MMILIKI! Shame on them!
   
 4. g

  geek Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Linaanza pia kutishiwa na gazeti jipya la Jambo Leo ambalo ninakuja juu kwa kasi sana.

  Mbona hii kidogo inanipa wasi wasi.....?
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Hiki ndicho ulichotaka kukifikisha kwa wakulu naona umezunguka sana bwana jambo leo. Wabongo kwa usanii tu.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hii imekaa kuudaku zaidi.hapa sio mahali pake
   
 7. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Yeah yeah,

  Jamaa kaja kulitangaza gazeti la Jambo Leo ambalo JK ana hisa na kina Ben Kisaka na crew yake. Si mchezo
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  I concur with you Mukulu.
   
 9. N

  Nanu JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii kweli imekuja kutangaza Jambo Leo on expense ya Mtanzania. Uliyeleta hoja hujatulia na una-kaunafiki au unajifunza unafiki. Hata magazeti yakiporomoka, who cares? Ungekuja na hoja kuwa Watanzania hawapati habari hapo tungekuelewa na pia ungetuambia ni kwa vipi.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Pia kuna maelezo mengine ya kuondolewa kwa Mwakiteleko. Ni intrigue za Muhingo rweyemamu, Managing Editor. Kwa kuwa anamzidi mshahara ameona ni bora amtafutie njia ya kutokomea. Kampa ka-unaibu ka-geresha tu nafasi ambayo haina kazi pale mbali na kujisomea magazeti -- ili aondoke mwenyewe, ikishindikana ataondolewa tu.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Udaku siyo udaku, ukweli ni kwamba mabadiliko yametokea pale New habari, kampuni ambayo haijatulia tangu Rosemary aondoke kama CEO last year. na kuteuliwa kwa Balile kumrithi Mwakiteleko ni kama vile kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi. Huyo jamaa ni mlamba viatu ile mbaya!
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nyote mliochangia mada hii, pamoja na mtoa mada mwenyewe mnashangaza kweli kweli! Hivi nani aliwaambia kwamba Rostam aliinunua habaro Corporation kwa ajili ya kuongeza mauzo ya magazeti?
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sawa kabisa. Hili ndilo tatizo la kuandika habari za hisia nakuzilemba kwa "habari zinasema" au "wachambuzi wa mambo ...." wakati mwandishi, mchambuzi na habari ni mtu yule yule. Tanzania Daima Jumapili katika ukurasa wake wa kwanza (lead strory) ni hivyo hivyo yaani ina habari za kiudaku.

  Hata hivyo haishangazi Magazeti ya Rostam yakiporomoka. Hata katika barua ndefu toka kwa Salva Rweyemamu kwenda kwa Rostam (iliwekwa JF) ilionya hivyo. Mimi nina marafiki zangu ambao kamwe hawanunui magazeti ya New Habari Corporation kwa vile ni ya Rostam.
   
 14. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Lakini watatumia ma-trekta ya Jeetu Patel.....hahaha....lol
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naona vigumu kukubaliana nawe, pamoja na wachangiaji wengine, kwamba aim ya thread hii ni kulikweza Jambo Leo. Hivi Jambo Leo ndiyo mbaya mkuu wa Mtanzania? Au mnamaananisha kwamba kwa kuwa JK ana hisa ktk gazeti hilo la Jambo Leo (kitu cha tetesi tu kisicho na uthibitisho) basi ndiyo sasa anampiga vita 'king maker' wake?

  Tuwe makini tunapojibu hoja, tusikurupuke tu.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani hlo Jitu Tapeli lina hisa katika New habari? Nifahamisheni.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I totally agree with you PJ 101 % -- who cares if we are to see the last of those papers?
   
 18. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hatuna independent journalists miaka yote!ndio maana tuna hali hii mpaka leo.Nchi zenye demokrasia ,magazeti yana play part vizuri sana hasa kama opposition parties ni weak.I guess wote hawa walisoma TSJ ,ambacho kilikuwa chuo cha propaganda cha TANU na SISIEM.Siwaamaini wa akina Tido Mhando,Makwaia wa Kuhenga na wengi wao.Hakuna investigative journalism,tangu lini mfisadi Rostam akaandikwa na magazeti yake?Hawa waandishi wake ni shame kwa wazawa watanzania
   
 19. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Rosemary Mwakitwange bado ni CEO wa habari cop. mpaka leo.
   
 20. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nah, she is nah longer there..
   
Loading...