Kupitia kwa ‘Baraka ‘ za Vyeo ‘ Mfululizo ‘ alivyopata kwa muda mfupi Afande Charles Mbuge tunajifunza yafuatayo

Kila jambo na wakati wake, wakati si ukuta, alipangalo Mungu mwanadamu ni nani hata aweze kulipangua, hakika Mungu ni Mwema,wote tumeuona mkono wake, tuzidi kumwomba wote wanaopitia aliyopita huyu mkuu, mkono wake uzidi kutugusa, Ni Katika Jina La Yesu Kristu Mwana Wa Mungu Aliye Hai.Amen

Unatarajia lini Kuanzisha / Kufungua Kanisa lako Ndugu Baba Mtumishi ili nianze kuwa ni miongoni mwa Waumini wako Waandamizi?
 
Ukidharauliwa na Mabosi wako na Wafanyakazi wenzako usiumie wala kusikitika.
Ukinyanyasika na Mabosi / Wakubwa wako usihuzunike wala usikate tama.
Hata kama Mabosi / Wakubwa watakuchukia Wewe tekeleza tu Majukumu yako Kiufanisi
Unaweza ukachukiwa na wengi ( hasa Mabosi / Wakubwa wako ) ila Mwenyezi Mungu atambariki Mtu Mmoja ambaye hukumtegemea na atakuwa ndiyo Mkombozi wako na atakuinua na kukufanya uwe Binadamu kamili katika Watu.
Uvumilivu unalipa japo unaweza ukayapata hayo Malipo yako kwa Kuchelewa.
Kama ipo ipo tu hata kama Mabosi / Wakubwa wako watakuwa mara kwa mara kwa Chuki zao tu wanakuandikia Ripoti mbaya.
Kusali sana na Kujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la muhimu mno katika Maisha ya sasa ya Mwanadamu ambayo yamejaa Chuki, Wivu, Majungu na Fitina.

Kwa tuliobahatika kidogo Kuyasikia mambo aliyokuwa akifanyiwa huyu Brigedia Jenerali ambaye naamini sasa atakuwa ni Meja Jenerali na Wakubwa zake hasa alipokuwa Mlalakuwa miaka ya nyuma na kwa Majungu tu ya baadhi wakaamua Kumuondoa hapo na Kumtupa kabisa Ruvu acheni tu Afande Charles Mbuge sasa ‘ atambe ‘ na Yeye ale Bata.

Ama hakika Mungu ni Mwema.
anaandaliwa kuwa CDF wabaadaye,huyu aliyopo muda wake ukiisha.
 
Charles Mbuge ni mtu wa watu na hupenda kujumuika na kila mtu, na hiyo ni sifa mojawapo ya kung'aa kwa nyota ya mtu.

Ila si wote wanaojumuika basi nyota zao hung;'aa na kuonekana kwenye fursa yoyote ya kimaisha.

Charles Mbuge anapenda mpira na kwa wale wapenzi wa mpira wanaitambua timu ya Ruvu JKT ambayo ilipanda daraja na inacheza ligi kuu, aliehakikisha timu hiyo inapanda ni Charles Mbuge.

Nyota ilianza kung'aa zaidi jina lake lilipopitishwa ili apewe kitengo cha michezo pale JKK kutokana na mafanikio ya JKT Ruvu.

Kila mahala alipopelekwa kutelekeza kazi kazi hizo zimekamilika kwa asilimia 101.

Charles Mbuge alipewa kazi ya kusimamia mji wa serikali Dodoma pale Mtumba na akiwna vijana wapatao 1500 wakapiga kazi na mji ukakamilika na vijana wale wote 1500 waliajiriwa sehemu mbalimbali kwa maagizo ya raisi John Magufuli.

Sasa Magereza wakapewa pesa wajijengee mahali pa kujisitiri wao wakawa wanapiga hesabu za kugawana hizo pesa na ndio sababu hata yule nanihino akatumbuliwa.

Raisi Magufuli alipotembelea mradi huu wa nyumba za Magereza na kuona madudu yaliyofanywa akakumbuka kazi ya Charles Mbuge na huyu kwa kiingereza namwita "Gaffer" akapewa kazi na kaipiga ndani yamuda ulopangwa.

Hongera sana meja jenerali Charles Mbuge kwa mafanikio yako na kupanda vyeo viwili ndani ya muda mfupi kutoka cheo cha kanali, brigedia jenerali na sasa meja Jenerali.
Bangi..
 
Amiri Jeshi Mkuu alipompandisha Cheo mwaka huu nilifurahi mno na baada ya leo tena kusikia amekuwa Boss mpya wa JKT ndiyo nimefurahi sana tu Ndugu. Mimi sijapita huko katika Umedani / Jeshini ila kwa Maelezo ya Watu ' Waandamizi ' kama Watatu hivi waliokuwa nae Kikazi / Kimajukumu waliwahi kuniambia kuwa Jamaa ( Afande ) alikuwa akinyanyasika na hata akidharaulika mno na Wakubwa hasa hasa ile Awamu iliyopita kiasi kwamba hata wana Medani wengine wakawa wanaumia kuona Jamaa akifanyiwa Mtima Nyongo huo.

Nina uhakika tokea Siku ile alivyopandishwa Cheo na Rais JPM na hivi leo tena amekuwa Boss wa JKT wale ' Maadui ' zake Wakuu Kikazi ambapo kati yao 75% wameshastaafu Kazi ila 25% bado wapo ingawaje nao Kustaafu Kwao hakuko mbali kutoka sasa naamini Baraka hizi na Afande Charles Mbuge Kupandishwa Cheo kunaweza kuwafanya ama wakose Usingizi au na Wao sasa wakajiandaa Kumpigia Simu za Kumuomba Msamaha kama ulivyokuwa Utaratibu wa hivi karibuni wa Watanzania au hata Maadui zake wengine kuomba ' appointment ' nae pale Mlalakuwa au Dodoma ili wakamuombe Msamaha ' mubashara ' kabisa.

Acheni Mungu aitwe Mungu tu Ndugu zangu na hapa duniani kamwe tusidharauliane wala tusikomoane kwani huwezi jua Kesho huyu unayemfanyia hivyo Mwenyezi Mungu atambariki na kumfanya awe nani hapo Kazini au katika Eneo fulani ambapo unaweza nawe ukajikuta unaumbuka na unaona hata Aibu kama hata si kutamani Ardhi ipasuke kabisa utokomee nayo.

Hivi wajeda nao wanapigana majungu?

.......Huu mwandiko naufananisha na jamaa mmoja mjuajijuaji sana humu Jf.
 
Humu ni jamiiforums siyo group LA WhatsApp la. Ofisi yenu.Halafu ndiyo mnajiona mnasiri haya sasa kumbe hats nyie wambea tu kama Shelawadu wengine.Haaaaaa
 
Wengi tunayapitia haya mazingira ya bw Afande mbuge, wakatishaji tamaa wamechachamaa kama wametumwa na shetani ila tunaamini ipo siku moja watashuhudia ukuu wa Mungu!
Ukidharauliwa na Mabosi wako na Wafanyakazi wenzako usiumie wala kusikitika.
Ukinyanyasika na Mabosi / Wakubwa wako usihuzunike wala usikate tama.
Hata kama Mabosi / Wakubwa watakuchukia Wewe tekeleza tu Majukumu yako Kiufanisi
Unaweza ukachukiwa na wengi ( hasa Mabosi / Wakubwa wako ) ila Mwenyezi Mungu atambariki Mtu Mmoja ambaye hukumtegemea na atakuwa ndiyo Mkombozi wako na atakuinua na kukufanya uwe Binadamu kamili katika Watu.
Uvumilivu unalipa japo unaweza ukayapata hayo Malipo yako kwa Kuchelewa.
Kama ipo ipo tu hata kama Mabosi / Wakubwa wako watakuwa mara kwa mara kwa Chuki zao tu wanakuandikia Ripoti mbaya.
Kusali sana na Kujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la muhimu mno katika Maisha ya sasa ya Mwanadamu ambayo yamejaa Chuki, Wivu, Majungu na Fitina.

Kwa tuliobahatika kidogo Kuyasikia mambo aliyokuwa akifanyiwa huyu Brigedia Jenerali ambaye naamini sasa atakuwa ni Meja Jenerali na Wakubwa zake hasa alipokuwa Mlalakuwa miaka ya nyuma na kwa Majungu tu ya baadhi wakaamua Kumuondoa hapo na Kumtupa kabisa Ruvu acheni tu Afande Charles Mbuge sasa ‘ atambe ‘ na Yeye ale Bata.

Ama hakika Mungu ni Mwema.
 
Kwaninhuko Ruvu ndiko wanakwenda walionyanyasika?
Kukaa makao makuu na kupewa kikosi ipi nzuri?

Ukiona mtu anachukiwa na watu wengi juwa yeye mwenyewe ndio mchawi
Kama anachukiwa mbona alipandishwa vyeo na kufikia ngazi aliyokuwa nayo kabla ya cheo cha sasa?

Kama wakubwa wake walimchukia mbona hawakumfukuza kazi?.
Kwani lazima? Na kwanini unaonekana Kuteseka sana na Mafanikio ya ghafla na Kuinuliwa Kimamlaka kwa Afande Charles Mbuge Ndugu? au na Wewe ndiyo wale wale mliokuwa mkinyanyasa Baba wa Watu Kipindi kile alipokuwa pale Mlalakuwa na hadi alivyohamishiwa Ruvu? Basi kwa sasa ndiyo mtamkoma na Mwenyezi Mungu anawaumbueni hapa hapa kwa Kumuinua na nyie Kubakia hapo hapo. Tubuni upesi na muanze Kujipanga Kupanga Mistari ya kwenda Kumuomba Msamaha. Mna bahati Baba wa Watu huwa hana Malipizi ( Visasi ) ila hili ' Zali ' ndiyo lingenikuta Mimi ' Maadui ' zangu wote mngenikoma na ndipo mngejua ni kwanini Wimbo wa Taifa hadi leo hauna Video na kwanini Nyoka hana Ugoko.
 
WEWE NI MPIGA MAJUNGU

udharauliwe na usamehewe.
Kwani lazima? Na kwanini unaonekana Kuteseka sana na Mafanikio ya ghafla na Kuinuliwa Kimamlaka kwa Afande Charles Mbuge Ndugu? au na Wewe ndiyo wale wale mliokuwa mkinyanyasa Baba wa Watu Kipindi kile alipokuwa pale Mlalakuwa na hadi alivyohamishiwa Ruvu? Basi kwa sasa ndiyo mtamkoma na Mwenyezi Mungu anawaumbueni hapa hapa kwa Kumuinua na nyie Kubakia hapo hapo. Tubuni upesi na muanze Kujipanga Kupanga Mistari ya kwenda Kumuomba Msamaha. Mna bahati Baba wa Watu huwa hana Malipizi ( Visasi ) ila hili ' Zali ' ndiyo lingenikuta Mimi ' Maadui ' zangu wote mngenikoma na ndipo mngejua ni kwanini Wimbo wa Taifa hadi leo hauna Video na kwanini Nyoka hana Ugoko.
 
Ukidharauliwa na Mabosi wako na Wafanyakazi wenzako usiumie wala kusikitika.
Ukinyanyasika na Mabosi / Wakubwa wako usihuzunike wala usikate tama.
Hata kama Mabosi / Wakubwa watakuchukia Wewe tekeleza tu Majukumu yako Kiufanisi
Unaweza ukachukiwa na wengi ( hasa Mabosi / Wakubwa wako ) ila Mwenyezi Mungu atambariki Mtu Mmoja ambaye hukumtegemea na atakuwa ndiyo Mkombozi wako na atakuinua na kukufanya uwe Binadamu kamili katika Watu.
Uvumilivu unalipa japo unaweza ukayapata hayo Malipo yako kwa Kuchelewa.
Kama ipo ipo tu hata kama Mabosi / Wakubwa wako watakuwa mara kwa mara kwa Chuki zao tu wanakuandikia Ripoti mbaya.
Kusali sana na Kujikabidhi kwa Mwenyezi Mungu ni jambo la muhimu mno katika Maisha ya sasa ya Mwanadamu ambayo yamejaa Chuki, Wivu, Majungu na Fitina.

Kwa tuliobahatika kidogo Kuyasikia mambo aliyokuwa akifanyiwa huyu Brigedia Jenerali ambaye naamini sasa atakuwa ni Meja Jenerali na Wakubwa zake hasa alipokuwa Mlalakuwa miaka ya nyuma na kwa Majungu tu ya baadhi wakaamua Kumuondoa hapo na Kumtupa kabisa Ruvu acheni tu Afande Charles Mbuge sasa ‘ atambe ‘ na Yeye ale Bata.

Ama hakika Mungu ni Mwema.
Afande Mbuge ni Mtu wa wapi ?
Namaanisha Kabila
Natanguliza Shukrani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom