Uchaguzi 2020 Kupita bila Kupingwa ni Mbinu chafu za NEC Au kukubalika kwa CCM?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,644
30,007
Hata angekuwa anagombea Yesu, Mtume Mohammed au Ibrahim, bado watu wangejitokeza kuwapinga kwa Hoja mbadala,

Hivi Leo hii sababu gani yaweza kumfanya mtanzania anayetaka uongozi apite bila kupingwa nje ya Uzwazwa wa wanaoongozwa sehemu husika?

Hakuna mtu sahihi au anayeweza kukubalika 100% kwa watu wote, hivyo kupingwa lazima kuwepo,

Leo hii unashangaa majimbo kadhaa wamepita bila kupingwa,

Hii ni Ama njama za NEC kuwaengua washindani kwa figisu figisu, na kuibeba CCM!

Sifa gani za mgombea anayeweza kupita bila Kupingwa?

Au Jimbo linapaswa kuwa na maendeleo gani ili kiongozi wake aendelee kupita bila Kupingwa?

Kwa kifupi hakuna!!!

Pia, tunaendelea kuwatishia watu kwamba CCM ikitoka madarakani amani itatoweka, hizi ni habari zilizozoeleka na Kupitwa na wakati
 
Tatizo ni tume na upinzani dhaifu unaoamini maneno na si kutenda vitendo. Zama za kupita bila kupingwa zilikwisha pita miaka mingi kwani upinzani kwa sasa umejitanua hadi kwenye vitongoji.
 
Ni uhuni na udhalimu wa CCM wakishirikiana na NEC na vyombo vyao vya ulinzi na usalama. Ila mwaka huu ndo mwisho wake. Nguvu ya umma lazima iseme jambo mwaka hu.
 
..mapingamizi ndiyo chanzo cha kuvurugika amani wakati wa chaguzi zetu.

..yanasababisha vurugu, tensions, na mihemko, isiyokuwa ya lazima.
 
Kupita bila kupingwa ni mtindo wa zama za mawe.Tutapata wapi Sera zako wakati kampeni hakuna.
 
Hilo sio swali, majibu yake yanaonekana kila kukicha kwa yanayofanywa na ma DED, nakushangaa ulieanzisha huu uzi, kwani wewe ni kipofu? au hujui kusoma?!
 
Kupita bila kupingwa ni mtindo wa zama za mawe.Tutapata wapi Sera zako wakati kampeni hakuna.
Ajabu Sana hili, Kama mtu anapita bila kupingwa hiyo haki ya kuchagua na kuchaguliwa inatekelezwa vipi?
 
Hata angekuwa anagombea Yesu, Mtume Mohammed au Ibrahim, bado watu wangejitokeza kuwapinga kwa Hoja mbadala,

Hivi Leo hii sababu gani yaweza kumfanya mtanzania anayetaka uongozi apite bila kupingwa nje ya Uzwazwa wa wanaoongozwa sehemu husika?

Hakuna mtu sahihi au anayeweza kukubalika 100% kwa watu wote, hivyo kupingwa lazima kuwepo,

Leo hii unashangaa majimbo kadhaa wamepita bila kupingwa,

Hii ni Ama njama za NEC kuwaengua washindani kwa figisu figisu, na kuibeba CCM!

Sifa gani za mgombea anayeweza kupita bila Kupingwa?

Au Jimbo linapaswa kuwa na maendeleo gani ili kiongozi wake aendelee kupita bila Kupingwa?

Kwa kifupi hakuna!!!

Pia, tunaendelea kuwatishia watu kwamba CCM ikitoka madarakani amani itatoweka, hizi ni habari zilizozoeleka na Kupitwa na wakati
hee mimi nilidhani sheria ndio ilivyo kwa sasa kumbe Tume imeamua wenyewe wengine yapite bila kupingwa. tisaidiane huku kupita bila kupingwa tumeanza awamu ya tano au.
 
Watu walionunua ndege madaraja reli bwawa la Umeme wakuza uchumi wanalazimisha kupita bila kupingwa? Nonsense
 
Back
Top Bottom