Kupimisha Kiwanja na kupata offer...

Kupimisha Kiwanja na kupata offer...

shegacool2015

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
394
Reaction score
133
Habari za jioni wana Jf.
Nina Kiwanja kidogo around 1000sqm nataka nipime nipate offer, jirani zangu wao swala lakupima hawataki kuliskia sasa nilitaka kujuaa kwa Kiwanja kidogo kama hicho process zinakua vp na gharama inakua aje?
 
Procedure ya kupima kiwanja kiwe kidogo au kikubwa au vingi ni ileile, ila gharama ya kupima kiwanja kimoja ni kati ya Tsh. 800,000= - 1,300,000/=. Kama kuna upimaji wa zamani (Adjacent Survey) ulioidhinishwa jirani na kiwanja chako, itafanya gharama iwe ndogo zaidi.

Siku hizi hakuna suala la offer, bali unaomba hati moja kwa moja ukishapata "approved survey plan" Gharama za ufutiliaji kupata hati ni zako mwenyewe katika ofisi za manispaa husika.
 
Huyu anayekuambia 800000 kupima kiwanja sidhani kama ni surveyor. Kupima kiwanja hadi unapata plani yako ni kuanzia 2000000,chini ya hapo mtazimiana simu. Kama ni nje ya dsm bei hiyo inawezekana. Ni mimi suryeyor nimemaliza 2005 na Bsc in Geomatics
 
Nakushauri andaa milioni 3.5 utaletewa hhati nyumbani Ikiwa kamili.
 
Nakushauri andaa milioni 3.5 utaletewa hhati nyumbani Ikiwa kamili.

Sa hati italetwaje bila kupima bhana!!! Mbona rushwa mnaipa kipaumbele bila sababu?kwani akifata taratibu itakuaje bhana?
 
Habari za jioni wana Jf.
Nina Kiwanja kidogo around 1000sqm nataka nipime nipate offer, jirani zangu wao swala lakupima hawataki kuliskia sasa nilitaka kujuaa kwa Kiwanja kidogo kama hicho process zinakua vp na gharama inakua aje?

Kupima peke yako itakuwa gharama sana, washawishi wenzio mpimiwe block nzima! Hizo gharama wanazotoa wadau hapo ni karibia sawa na kupima block nzima! Mimi huku kwetu nilifuatilia nikaambiwa niwatafute jirani zangu angalau wanne tulipe hiyo gharama halafu wao wapime block nzima!! Wafuate watu Wa ARDHI wakupe utaratibu mzima! Humu ndani utakumbana na wajasliamali tu!!
 
Kweli umu kuna wababaishaji na wezi ....kuna rafiki yangu kapimiwa kwa mil1.2 pamoja na hati na kila kitu na kapimiwa peke yake mtaa mzima.

Ni Jirani yangu ila cha ajabu mikoa yetu tofauti, yeye pwani mm dar ila tuko jiran, sasa umbali km 1 ndio ulete tofauti ya mil1.2 kwa mil2 au 3.5 ??? Watu wa dar mnapenda metremko
 
Jamani asanteni, pusha la magogoni ..yani Tz na kule nchi za Asia bila kutoa kitu kidogo mambo hayaendi sawa, ila m3 kwa sqm 1000 naziona bado nyingi Sana, ngoja nizichange nipate hata 2m nijaribu kufanya utaratibu, cz wa bongo nikipaacha bila ku survey wanazewa kujihalalishia.......na hivi nikiwa na Pesa process hadi kupata hati inachukua mda gani
 
Last edited by a moderator:
Stesheni 2005 kulikuwa hakuna Bsc in Geomatics Bali Land Surveying. Wakati huo tuliwaita LS mi nilikuwa LMV.
usichukulie mambo kwa ujumla. je kama kasoma ughaibuni? au unamaanisha duniani kote hiyo kozi ilikuwa haipo. think beyond your nose.
 
Stesheni 2005 kulikuwa hakuna Bsc in Geomatics Bali Land Surveying. Wakati huo tuliwaita LS mi nilikuwa LMV.

Lol!!! Umevamia Treji Kwa Mbele, Inawezekana Wewe Ni Kanjanja Wa Elimu Ona Wenye Taaluma Wanavyokuumbua, Tuambie Hiyo BSC Ya Geomatic Umeipatia Wapi??
 
Lol!!! Umevamia Treji Kwa Mbele, Inawezekana Wewe Ni Kanjanja Wa Elimu Ona Wenye Taaluma Wanavyokuumbua, Tuambie Hiyo BSC Ya Geomatic Umeipatia Wapi??

Msome vizuri uyu mtaalam, hajasema BSC kasema Bsc

Alafu hajasema BSC ya Geometic kasema Bsc in Geometics, aya mambo yanatofauti kubwa, ndio tofauti ya msomi na kanjanja!!
 
Msome vizuri uyu mtaalam, hajasema BSC kasema Bsc

Alafu hajasema BSC ya Geometic kasema Bsc in Geometics, aya mambo yanatofauti kubwa, ndio tofauti ya msomi na kanjanja!!

Sasa naona umekuwa mwalimu wa Grammar,usituhamishe kwenye mada
 
Labda nitoe mfano ulio hai kabisa na current hapa nilipo;sisi tumejikusanya kama watu 5 na tuna jumla ya ekari 14 na Mara baada ya vipimo vya shamba zima Kwa eneo LA ekari hizo 14 tumepata viwanja 22 na mpimaji amesema kila kiwanja kimoja tumpatie laki mbili unusu je ni sahihi kweli au anatupiga huyu jamaa?
 
Aisee na mimi ni swali kama lako... Gharama za kupima kiwanja kimoja ni sawa na kipima ekari 20 na kuzikata kwenye viwanja vidogo vidogo?
 
Labda nitoe mfano ulio hai kabisa na current hapa nilipo;sisi tumejikusanya kama watu 5 na tuna jumla ya ekari 14 na Mara baada ya vipimo vya shamba zima Kwa eneo LA ekari hizo 14 tumepata viwanja 22 na mpimaji amesema kila kiwanja kimoja tumpatie laki mbili unusu je ni sahihi kweli au anatupiga huyu jamaa?

That is fair and cheap, kama unapima viwanja vingi kwa wakati mmoja gharama ya kupima kiwanja kimoja inapungua. Kwa mfano kama ungekuwa unapima viwanja 1000, gharama ya kiwanja kimoja ingekuwa katiki ya 70,000/-80,000/= kwa makadirio, lakini haitazidi 100,000/= kwa kiwanja.
 
Huyu anayekuambia 800000 kupima kiwanja sidhani kama ni surveyor. Kupima kiwanja hadi unapata plani yako ni kuanzia 2000000,chini ya hapo mtazimiana simu. Kama ni nje ya dsm bei hiyo inawezekana. Ni mimi suryeyor nimemaliza 2005 na Bsc in Geomatics

Uwe unasoma vizuri kile kilichoandikwa na ukaelewa. Bei niliyoitoa iko sawa kabisa ila inategemea wapi kiwanja kipo na kama kuna upimaji wa zamani jirani kabisa na hicho kiwanja.
 
Staff mwenzangu kapata hati last year na katumia 1.2m tu....kiwanja chake kipo Goba ...acheni kutisha watu na hizo 3.5m zenu .....mimi nimempa mtu kazi hii nitatoa ushuhuda hapa.....
 
Back
Top Bottom