Kupima uwezo wa Rais Jakaya Kikwete?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupima uwezo wa Rais Jakaya Kikwete??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumain, Nov 17, 2009.

 1. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimechoka na vigezo vinavyotumika kupima uwezo na mafanikio ya rais wetu kwa muda wote katika JF forums je
  1. Si halali kupima uwezo wa rais kwa kigezo kimoja tu cha kuzibiti ufisadi ..yaani EPA, Richmond..etc after all watuhumiwa wako mahakamani wengi tu..ala..
  Tuangalie mambo mengine mengi anayoyafanya na kufanikiwa mfano:-
  a) Kuongezeka kwa enrollment kuanzia primary mpaka university kwa miaka ya ke minne --kielimu siyo mafanikio hayo??
  b) Kuna program za kujenga zahanati kila kata..kusogeza huduma za afya karibu na wananchi---siyo mafanikio??
  c) Kuongezeka kwa utalii na watalii tangu ashike nchi..siyo mafanikio hayo???
  d) Barabara za lami mpaka kigoma.rukwa nasikia dodoma-arusha is on track..siyo mafanikio hayo?? kwa miaka minne
  e) Uhuru wa habari and tolerance of our president to the freedom of expression..zitto ameliona hili naye..
  Bana ye mnyonge mnyogeni haki yake mpeni...mlitaka awafanyeje? wana JF mbona hamna shukrani hasa wewe mwanakijiji.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Maisha bora kwa kila Mtanzania. Hiyo ilikuwa ahadi aliyoitoa kupata kura. Ni kigezo tosha kupima uwezo wake.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Natoa shukrani zangu za dhati kwa Mh. Rais wetu kwa kuwezesha hili. Nampongeza kwa kweli. Hata hivyo nikiwa kama mtu anayependa kudadisi mambo badala ya kuyapokea tu mazima mazima na kuyapigia magoti na makofi mithili ya jinsi vile waumini wa dini wafanyavyo; ningependa sana kujua the motive behind this. Ni vigezo gani haswa vimemfanya Mh. Rais wetu awe enabler and proponent wa uhuru wa habari?!

  Kwa mifano negative ya EPA na Richmond uliyotoa, je hili kama positive aspect ya mafanikio imetokea tokea tu, au kuna sababu nyuma yake, ipi hiyo?!
   
 4. S

  Shamu JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninaamini kwamba vitu hivyo vyote ulivyosema kuhusu rais ni kweli. Lakini lazima ujue umuhimu wa kumpa critics Rais wakati akiwa madarakani. Rais kulaumiwa kuhusu UFISADI ni muhimu; kwa sababu, RUSHWA na UFISADI ndiyo tatizo kubwa ktk TZ. Akimaliza urais ndiyo tutaanza kumsifia, lakini siyo sasa hivi. Let's build this Great Nation, TZ.
   
 5. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hayo no matangazo ya kibiashara tu mkuu, kama yale ya sigara! Hakuna nchi duniani wananchi wake wote wanaoweza kuishi maisha bora!
  Kumbuka msemo aliofuata baada ya uchaguzi "Maisha bora hayapatikani kwa kukaa vijiweni"
   
 6. Kabwela

  Kabwela Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Tumaini pole kwa kulewa kidogo hasa kwa taaria za kusikia tu bila uhakika. Jaribu kufikiri kipi bora hasa:
  1. ni kutanua barabara ya Chalinze -Segera na kale ka kipande ka kwenda Bagamoyo kawekwe lami ili JK aende kwa raha bagamoyo au kutanua barabara ya Kimara Chalinze ambayo kwa sasa muda wote kuna foleni kutokana na watu kukimbia mabomu mbagala na ugumu wa maisha mjini na kuongezeka njia ya Kibaha?
  2. Kujenga majengo ya madarasa na zahanati bila kuwa na mkakati kabla wa kuandaa walimu na wahudumu wa afya kwenye hizo shule za kila kata na zahanati ambazo hazina dawa?
  3. Shule zinazosemwa nyingi hazina hata vyoo na nyingi ni madarasa 2-3 tu ambazo hazina walimu na hakuna hata nyumba za walimu wakati watoto wao wanasoma st..... Arusha?
  4. mwaka 2005 November chips maya ilikuwa sh 500/= na sasa hikulikana imeshafika kiasi gani na sukari ilikuwa 600/= kwa kilo na sasa imeshafika 1,400/=, kuungamisha umeme ilikuwa 240,000/= na sasa ni 470,000/=;
  5. Richmond wanasingizia ni tamaa za uwaziri mkuu za Sita na kupenda vyeo kina Mwakyembe, je hizi gharama za umeme zinazopanda kila siku na walala hoi ndio tunaolipa wao wanalipiwa na serikali. hivi ni kweli ni kampeni za vyama vya upinzani kuipiga vita serikali ya CCM au ni nini?

  Naomba unifafanulie mnaposema maisha bora kwa kila mtanzania JK anamaanisha kuwa ndio hivi au upeo wako kutathimini mambo ni mdogo kiasi hicho unchoonesha hapo?
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  JK,

  Alishasema wazi kwamba angependa watu wawe na uhuru zaidi, akasema wa in transition.... so motive yake iko simple.... wewe na mimi tuwe huru.... kwenye hotuba zake amekuwa akisema hili
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwenye vita ya Ufisadi pia, kuna haya aliyofanya ambayo kwa msomi mzuri hawezi kuyabeza.

  1. Kupitisha sheria ya PCCB, ambayo ndio inawezesha sasa Hosea kuweza kupeleka watu kwa pilato b4 that mpaka uone watu wana exchange coine/notes.

  2. Kupitisha sheria ya National Audit Office, na kufanya report ya CAG, kujadili bungeni openly mpaka hata madudu ya office ya rais.

  3. Kupitisha sheria ya mwendesha mashitaka na kumfanya awe huru zaidi.

  4. Sheria ya uchaguzi kupitishwa kuhuru ufadhili wa vyama wakati wa uchaguzi na kutofautisha business na siasa.

  5. etc etc etc.

  Kwa mwenye kuwa na mtizamo mpana.... hayo sio mambo hapa, kwa kuwa sheria ni endelevu na kumpeleka mtu kwa pilato ni jambo la muda tu.
   
 9. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ondoa hilo la barabara hakuna hata moja aliyojenga yeye zaidi ya zile alizozikuta ujenzi unaendelea suala la barabara heshima iende kwa mkapa.
  Mbona haujaongelea kutembeza bakuli kila leo kama ni moja ya mafanikio kwa Jk?
   
 10. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Tumaini. First let me say Thank you for your very nice and good observation.
  Lakini umesahau kitu kimoja mkuu! Feeling wananchi walio nayo kuhusu ufisadi ina pain in Greater %ge than happiness %ge we get in enjoying his achievements.
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Pole kaka, na pia asilimia kubwa ya barabara za Mkapa, zilikuwazishapangwa na kutafutiwa wafadhili na Mwinyi.

  So kuna issue ya kupokezana vijiti mzee, ukiona mkandarasi yuko site, ujue kazi ya ujenzi na uchoraji ilianza miaka mitatu nyuma... okay!!!

  So do not expect... unasanifu mwaka huu, unatoa tenda mwaka huu, ujenzi unaanza mwaka huu na unaisha mwaka huu... tulia kidogo ufikiri kaka... kujenga barabara sio sawa na kununua ndizi sokoni tandale.
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  All of those will be great mkuu. Just support your point with facts & figures. Tupe data mkuu kuthibitisha yote usemayo.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,516
  Trophy Points: 280
  Mada ni nzuri tuu za wasifu wa JK. Hii ndio demokrasia ya JF. Ila huna sababu za kuweka majina ya wana JF ambao hatuna utamaduni wa kuwaimbia wanasiasa nyimbo za shangwe na mapambio. Jenga hoja tetea hoja yako majina achana nayo.
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Angalau kwenye suala la elimu sikubaliani na wewe!!! mkuu, wewe ulitakaje? Ulitaka kwanza ianze mass production ya waalimu kabla ya mashule? then baada ya hao walimu kuwa produced wangeenda wapi?! Ulitaka shule ya wanafunzi 100 iwe na walimu 20 au wangebaki mtaani kusubiri kuongezeka mashule? tuacheni masihara waungwana, hivi ni kweli hamna mikakati ya kutatua tatizo la waalimu hata baada ya Mkwawa na Chang'ombe kuwa university colleges of education?! hivi ni kweli hamna mikakati ya kuongeza waalimu licha ya kwamba admission ya waalimu kwenye vyetu ni kubwa maradufu kuliko taaluma yoyote ile?! Let's open our eyez man!! hata mimi mwenyewe awali nilikuwa sikubaliana kabisa na suala la kuongeza mashule kama njugu wakati hamna waalimu!!! Nilikuwa sana naji-defend kwele nadharia inayopatikana kwenye kitabu cha KIJIJI CHETU, kwamba kinachohitajika sio wingi wa watu bali hata watu wachache lakini wenye kiu ya kuleta maendeleo!! But later nikakaa chini na kutafakari- nikaona ni kama mchezo wa kuku na yai!!! nani kaanza!!! Nikajiuliza nini hasa kilitakiwa kuanza kati ya mass production ya waalimu au ujenzi wa mashule!!! nikakuta, ilibdi kwanza mashule ili walimu wakishapatikana tayari wawe na vitu vya kazi!! From hapo, nikatoa kijiba cha roho!!
   
 15. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ndo kusema we hapa umefikiria nini na umetuelimisha nini juu ya mafanikio ya JK bado mi nasimama kwanye ukweli kuwa bado yeye hajajenga barabara labda tusubiri kama ndo yupo bado kwenye plan.
   
 16. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wenye kusubiri maisha bora toka kwa wanasiasa, watasubiri sana hadi kaburini.
   
 17. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nianze kwa kusema SAWA BABISA "UMENENA VYEMA" Katika vipengele ilivyo onesha, bado sikubaliani na wewe kwamba JK ameleta maendeleo. Mikakati yote hiyo ulikuwatayari ilisha anzishwa kwenye hawamu ya tatu.
  Pia ukiangalia kilichofanyika hakilingani na hali halisi ya fedha zilizo tumika. Kweny utalii hakuna kilichofanyika bali hali imekuwa mbaya zaidi. Gharama zimekuwa zikipanda holela holela bila mpangilio na sehemu nyingine zimebinafsisha/zimepewa wawekezaji ambao wanachokifanya ni kubeba mali asili zetu hasa wanyama wakiwa hai na kupeleka makwao.
  Shule wanafunzi wengi bado wanasoma wakiwa wamekaa chini na waalimu wengi bado hawajalipwa mafao yao.
  Unapoona kuna sehemu ambayo inatiliwa mkazo, basi fahamu kuna walakini.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Pole sana kaka na wewe nadhani unatoa hizi habari kwa wototo wa miaka 10.
  Mie ni mtu wa miaka 50's sidanganyiki.
  Mwinyi aliacha nchi haina kabisa pesa kwenye consolidated fund hizo pesa aliziomba wapi? Nchi ilikuwa na hali mbaya sana.
  Tupe data ku Substantiate hoja yako hizo pesa alizipata wapi Mwinyi bwana.
  Tunajua mpango mahususi wa mkapa wa kujenga barabara zetu kutokea katika internal funds alianzisha yeye na utekelezaji ulifanyika, na Mwinyi hastahili sifa yoyote kwa hili.
  Narudia sisi ni watu wazima hatudanganyiki kwa kitu mkuu tumeshuhudia mengi ya uongo yakitolewa na watu kama nyinyi.
  MF
   
 19. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  wananchi mbona hawana pain kihivyoooo!!! labda kale kakikundi chenu wachachee mlokosaa ulajii kwa mkuluu ndo mnaendelezaa chokochokooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  1. Ndugu, hakuna shida yeyote wananchi wa bagamoyo kupata barabara..ni maendeleo hayo?
  2. Kuna barabara ya kwenda Handeni kutokea mkata inajengwa kiwango cha lami na kutokea korogwe kwenda handeni kiwango cha lami..ni maendeleo hayo...???
  3. Kuna barabara ya Arusha -Dodoma, Arusha -singida kiwango cha lami..maendeleo hayo??
  4. Barabara ya Rukwa-Kigoma, Rukwa -Mbeya kiwango cha lami..maendeleo hayo??
  Hizi zote ni project za awamu ya nne?? miaka minne kafanya kazi bana ..acheni hizoo??
  Kuna ndugu anasema mipango ya awamu ya tatu NO NO, Kuna mambo vile awamu ya tatu iliyakuta kutoka awamu ya pili..mfano barabara ya kusini (rufiji) ilishasainiwa na mwinyi na wafadhili kutoka kuwait lakini baadaye ilionekana kama ya Mkapa vile...tuwe wakweli bana!
   
Loading...