Kupiga marufuku uvutaji sigara maeneo yenye mikusanyiko

fokonola bokoyoka

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
966
638
Ni jambo linalosikitisha viongozi wetu kupitia Wizara ya Afya wamekaa kimya kuhusu hawa watu wasio na adabu kwa kuvuta sigara hadharani au kwenye mikusanyiko ya watu wawili au zaidi.

Kwa kweli wamekuwa kero sana katika jamii yetu na kwa wale wasiotumia hii aina ya starehe. Report na tafiti nyingi za kiafya zimebainisha hatari ya uvutaji sigara lakini serikali yetu imekaa kimya wakati vifo vingi vinatokana na uvutaji lakini ni bora serikali ikapeleka muswada bungeni ili uvutaji holela wa sigara ukomeshwe maeneo yenye mkusanyiko.

Nchi kama Uganda tayari imeshaliona hili na utekelezaji ushaanza rasmi hivyo kupitia uzi huu tunatumai kuwa serikali itaandaa muswada utakao kuna kuwa sheria na kukomesha uvutaji holela wa sigara maeneo yenye mkusanyiko.
 
Back
Top Bottom