Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
KAMA KUPENDA NI SUMU
1)Mahaba usiniue,nifaidi penzi lakoPenziletu lichanue,niwe nawe peke yako
Kwako peke nitulie,nisije kwacha mwenzako
Mwenzako nisiumie, kukosa upendo wako
Basi acha nizimie, kama kupenda ni sumu.
2)kuloga usinendee,mimi si kama wengine
Moyoni kwangu tulie, siwezi kwenda kwingine
Ahadi hii ya pekee, nimpe nani mwingine
Kama si wewe nanie,nitaumia pengine
Basi acha nizimie, kama kupenda ni sumu.
3)Siku zikienda mbele, wazidi wako uzuri
Sautiyo si kelele, nzuri zaidi zimari
wa sasa siyo wa kale,Kweli unanipa hari
Wapunguza sirazile, ninapopandwa na mori
Basi acha nizimie, kama kupenda ni sumu.
4)Walosema ni kidonda, jumbe hawakukosea
Usione ninakonda, wewe nakufikiria
Shika moyo unadunda, wewe tu wakuwazia
Kama wivu ni kidonda wewe utakitibia
Basi acha nizimie, kama kupenda ni sumu.
Shairi=KAMA KUPENDA NI SUMU
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com