Kupenda kwa akili

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Habari zenu Wakuu,

Kwenye pitapita zangu Jf nikakutana na mdau akimshauri jamaa aliepigwa tukio na Mwanamke wake wa ndoa, na moja ya ushauri aliompa huyo alietendwa ni "PENDA KWA KIASI USIPENDE MAZIMA".

Comment ya mdau ilinifanya nifikirie kwa mapana na marefu na mwisho wa siku nikapata jawabu ya kwamba kupenda kwa kiasi kunafanana sawasawa na kupenda kwa akili.

Kama hamjanielewa ngoja nieleezee kidogo!

Kupenda kwa akili ni hali ya kuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu pale ambapo unaona kuna kosa/makosa yanafanyika eg. Umemfumania Mume/Mke, ushirikina, kutokuwa na adabu n.k

Kupenda kwa akili hakuhusiani na Hisia/Moyo bali ni Maamuzi, Makubaliano na Ukweli.

Watu wanaopenda kwa akili huwa hawasamehi Usaliti, lakini watu wanaopenda bila ya kutumia akili ndio husamehe na kuendelea na maisha kwa kusingizia watoto, wazazi n.k

NB. PENDA KWA AKILI, USIPENDE KWA HISIA.

Mjanja M1
 
Upendo ni sababu ya kusamehe maovu yote.Hakuna kupenda kwa akili bali unaweza kuishi na mume au mke kwa akili.Ukipenda unakuwa umependa mazima hakuna akili wala uchawi.
Upo sahihi, lakini nahisi haujalielewa bandiko langu Mkuu.

Kupenda tunapenda, ila kupenda na kuwa mjinga hilo ni kosa na kwa wenye akili tunasema hujapenda kwa akili.

KUPENDA KWA AKILI NI KUTOKUBALI HISIA ZIZIDI AKILI.
 
Nimelielewa sana tena sana.
Ninachokifahamu ni kuwa huwezi ukapenda kwa dhati kisha ukabaki na akili zako timamu.
 
_20231203_145249.JPG
 
Well put mkuu,Wanaume tuache ushoga tufuate aliyotuelekeza MUNGU,tutumie Akili hayo mambo ya Hisia sijui upuuzi Gani tuwaachie Wanawake.Tatizo sijui ni haya makuku ya kisasa tunayokula,maana Wanaume kibao skuizi wanalialia sijui machozi wanatoa wapi,Jana manzi hapa mtaa kamsuprise msela Kwa birthday party Jamaa kaangusha mchozi,ukiangalia Wanaume tunazidi pungua
 
Inaonekana huyo jamaa hajawahi kupendwa kama huyo bidada anavyompenda.

Mwambie asisahau kutumia akili.
 
Back
Top Bottom