Mheshimiwa umeeleza vizuri ila tu Kuna angalizo kidogo hapa Chini
Kundi la vijana kuanzia 20 - 25 wengi bado wako kwenye adolescence, adolescence inaanzia 18 - 25, adolescence ni kile kipindi cha balehe ambacho mtu anataka kujaribu kila kilicho mbele yake, atataka kubadilisha aina zote za wanawake n.k
From 26 - 29 kijana anakua ametoka chuo na kukutana na Street life na anaanza kuwajibika na maisha yake moja kwa moja, hata hivyo masuala ya starehe za kukesha usiku, kwenda kwenye matamasha i. e Fiesta, clubs bado anakua nayo, maana at this stage ana kazi, na pengine zile vurugu za nyuma zika double kwa kuwa ana ajira na pengine kapanga yuko kwake na total freedom
Kuanzia 30 - 35 ukomavu unaanza katika maisha ya huyu mtu, si ajabu na ka cheo kamepanda kazini, mara nyingi ni vile vyeo baada ya hatua ya ukarani sasa amekua supervisor na kadhalika hivyo anaanza kutambua maana ya uwajibikaji kwa vitendo, Hapa anaanza kuchangia harusi mbali mbali za wenzie kazini, hivyo na yy kupata uchungu lini atachangiwa
Sasa hapo kuanzia 35+ tayari amefanya maamuzi, anajitambua, amesumbua sana mabinti kwa kuwa play sana na sasa ameamua kutulia na kuoa, na kuanzia hapo ule upuuzi wote wa nyuma ameacha, wasichana ni mashahidi wa hili, wanaume kuanzia age si wasumbufu sana kwenye mapenzi, na ukienda kwenye daftari la ndoa zilizofungishwa utaona age ndio wengi sana
Hivyo mabinti wanayajua haya makundi vizuri kuliko sisi wanaume, wanajua lile kundi la 18-25 ndilo sumbufu kuliko yote, likifuatiwa na lile la 26-29
Hivyo wanaelewa kundi lipi walau watakua kwenye safe side
Hii analysis sio suala la vijiweni, yoyote aliesoma somo la psychology anaelewa na naongea kitu gani, kwenye psychology wameyachambua haya makundi kulingana na umri na kiuhalisia pia iko hivyo
Hii haina maana ni wote, msomi yoyote aliesoma probability anaelewa kitu kinachoitwa sample katika utafiti, unaweka utafiti wako ktk asilimia na hivyo una conclude
Hivyo akina dada wanaoweka sharti hilo la kuitaji Mchumba wa 35+ wana uzoefu na makundi haya