Kupata Sauti na TV kwenye LapTop | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupata Sauti na TV kwenye LapTop

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by BabaDesi, Oct 13, 2012.

 1. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Salaam, Wataalamu wa JF.
  Nina maswali yangu mawili ambayo nimepata kuyauliza huko nyuma lakini sijapata jibu la uhakika ambalo limeniwezesha kupata ufumbuzi wa matatizo yangu. Naombeni msaada wangu.


  1. Laptop yangu ni TOSHIBA EQUIUM A100-333 Model PSAAQE-00600AV. miezi kama miwili hivi katika kuminya minya sijui vijana waliminya nini lakini ikapoteza sauti. Naangalia DVD vizuri lakini hakuna sauti. Nikapata ushauri kutoka JF kui-stall tena Audio Device. Nikafanya hivyo kwa kui-install RealTek AC'97 Audio. Cha ajabu ni kwamba sauti haijarudi. Je ni nini ninachotakiwa kufanya, kwa lugha nyepesi, ili kupata sauti??

  2.Kwa kawaida huwa saa Mbili kamili za Usiku ninakuwa bado niko kwenye mihangaiko lakini hupenda sana mahali nilipo niangalie angao taarifa ya habari kutoka kituo chochote cha TV.
  Je ninaweza kupata maelekezo, kwa lugha nyepesi, ya kuweza kufanya Laptop yangu iweze kupokea pia matangazo ya Television?
  Mara kadhaa nimejaribu kufuata njia ninazozisoma kupitia JF lakini kila mara ninafika mahali ninakwamba, ama kutokana na uhafifu wa maelezo ninayopata kutoka JF ama kutokana na Kutokuelewa kwangu.

  Swali: Je naweza kufanya LapTop yangu ikapokea matangazo ya Local TV Channel na nikaweza japo kuangalia taarifa ya habari ya ITV?? Kwa Namna Gani???? Kwa Lugha nyepeeesi tafadhali!:poa
   
 2. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa, shikamoo BabaDesi. Pili, pole kwa kukosa uhondo wa sauti. Tatu, kuhusu sauti, sijui kama iko mute ama? Tafadhali jaribu kuangalia, na kama haipo muted. Je umejaribu kuchomeka headphone ama speaker na kuona? Kama bado jaribu. (windows yako ni ipi?). Nne. Kuna kitu kinaitwa usb tv stick. Naamini itakufaa hiyo. Hebu itafute mkuu, huwa haina complications naamini. Sijui lugha yangu ni rahisi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Habari za siku nyingi Baba Desi.....

  Umepotea sana mkuu, hatuonani kabisa kule kwenye Jukwaa letu la Burudani na Michezo, hasa kwenye jukwaa dogo la burudani, nyimbo za enzi hizo.....

  Turudi kwenye swali lako la msingi, Unatumia operating system gani?....Kama ni MS Windows,ni ipi?, XP,Vista , 7 ama 8?


  Watch tv on laptop without internet - General-Laptops-Notebooks - Laptops-Notebooks
   
 4. Fatma Bawazir

  Fatma Bawazir JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  mh shikamoo baba desi hiyo laptop umeitumia muda mrefu unaielewa vizuri kama ingekua ktk sound iko mute ingekuwa umesha gundua na kama tatizo lingekuwa ni driver pia ingekuwa umesha lipatia ufumbuzi hapo tatizo hao vijana watakua wame conect hiyo laptop na tv au redio kwa ajili ya ku record audio music kwenye laptop sasa itakuwa wameipa high volume na soud card imeungua ili kuhakikisha play file lolote la music nenda ktk sehemu ya kuongeza volume utaona mawimbi ya sauti yanapanda na kushuka kama ilivyokuwa kawaida yake tangu awali lakini sauti hakuna na ikiwa driver za sound hakuna basi hata kale ka spika kinakuwa hakipo ikiwa utasibitisha kwa hivyo basi cha kufanya nenda tu kariakoo kanunue extenal sound card uchomeke ktk usb ili uendelee kupata saund na bei yake iko kwenye elfu kumi


  Extenal sound card

  Capture.PNG
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Ah, Mkuu Balantanda! Habari za Miaka Mkuu? Upo? Mi nilirudi kijijini kwanza kwa ajili ya masuala ya kujaribu 'Kilimo Kwanza' na si unajua tena ukiwa kijijini inabidi vi-bundle hivi vya Internet unakwenda navyo kwa kubembeleza mkuu!!
  Makiri kwamba sikujua kwamba umejificha huko. Nitapita kuchungulia huko wakati naendelea kutafuta ufumbuzi wa tatizo langu.

  OP yangu ni Windows XP, mkuu.

  Natanguliza, Ubarikiwe!
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Fatma B, Salam.
  Asante kwa ushauri wako. Kama ulivyosema, yote hayo nimeyajaribu na bado Ltop imeendelea kuwa Bubu. Naona kweli itabidi zinitoke Alfu 12 nikatafute hiyo kitu.
  Halafu kwa si wastaafu tena ukitaja Alfu 12 ni kama umetaja Laki 1 na mia 2! ha haa! :lol:

  Anyway, asante sana kwa Ushauri wako mwema.
  Ngoja tuvute tuvute tuone kama kuna member atakuwa na ushauri mbadala.

  Ubarikiwe sana FB (sio FaceBook!)
   
Loading...