Kupanda kwa Nondo: Kwanini serikali isiuze vyuma chavu?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Hii ni Serikali ya Wanyonge tena wafia uongozi imara wa JPM. Kuna suala la kupanda kwa vifaa vya ujenzi ikiwemo na Nondo.

Sasa ukiangalia maeneo ya Bandarini kuna shehena ya mabehewa ya TRC yamejiozea tu pale na kuleta uchafu kwanini wasiuze kwa wenye viwanda vya kutengeneza nondo. Pia ije na mkakati wa kusafisha gereji bubu kwa kutoa vyuma chakavu vyote na kupeleka viwandani.
 
Kwa kweli inashangaza sana vifaa vya ujenzi kupanda bei kila wakati

Walisema watachunguza lakini kila siku afadhali ya jana!
 
Mahitaji ya chuma yako juu sana, hayo mabehewa hayatasaidia chochote, ni kama kuweka tone moja kwenye simtank, bei itabaki pale pale
 
Kwa kweli inashangaza sana vifaa vya ujenzi kupanda bei kila wakati

Walisema watachunguza lakini kila siku afadhali ya jana!
Hivi unategemea mtu anayetengeneza tatizo ndiyo huyo huyo aje kulitatua!? Jiongezeni bwana hata kama ni akili za kizuzu!!chanzo cha yote hayo ni serikali yenyewe tu, kwenye kuongeza kodi za ajabu ajabu kila leo, watu wanapewa targets , na bila kufikia hiyo target ni hatari kwao, unategemea nini hapo ndio maana huwezi isikia serikali inakuja na jibu stahiki tofauti na matamko ya kisiasa tu!!!ambayo siku tatu tu, yanasahaulika na maisha yana baki pale pale!!bei ya mafuta ya kula, kuna nini licha ya matamko yote yale?!!eti kodi inakusanywa na TASK FORCE!
 
Back
Top Bottom