Kupanda kwa Bei ya Umeme: Serikali Ndiyo Ibebe Lawama Nyingi siyo Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupanda kwa Bei ya Umeme: Serikali Ndiyo Ibebe Lawama Nyingi siyo Tanesco

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Dec 31, 2010.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,
  Jana usiku kulikuwa na kipindi cha moja kwa moja cha mahojiano kilichorushwa na ITV. Mada ilihusu kupanda kwa bei ya umeme. Kuna jamaa mmoja hakusita kuelekeza lawama kwa serikali kwamba ndiyo chanzo kikuu cha kusuasua kwa sekta ya umeme nchini. Maana yake ni kwamba wananchi wanaumia kutokana na uzembe wa serikali wa kutowekeza kwenye umeme kama inavyofanya kwenye sekta zingine kama kilimo. Binafsi ninamuunga mkono huyo jamaa. Najua Tanesco ina matatizo ya kimenejimenti ambayo kwa namna moja au nyingine nayo yanaongeza gharama kwa mtumiaji wa umeme lakini serikali bado haijawa serious na uwekezaji kwenye sekta ya umeme, kama alivyofanya Mwl. Nyerere. Badala yake serikali inaingia mikataba mibovu na makampuni binafsi na kuilazimisha Tanesco kununua umeme kwa gharama kubwa sana ambazo mwisho wa siku mwananchi wa kawaida ndiye anayezibeba.

  Hivi tuwe wakweli jamani, kwa nini serikali haiwekezi kwenye miradi mikubwa ya umeme na kuikabidhi Tanesco. Ndiyo maana watu wengi wanasema kwamba hiyo ni miradi ya wakubwa kwa malengo binafsi. Mnasemaje wana JF? Karibuni jamvini.
   
Loading...