Kupaka Rangi Gari Zima

Kupaka Rangi Gari Zima

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,184
Reaction score
88,929
Wakuu Habari.

Nimekuwa nikipaka rangi kwa mafundi wa hapa na pale kila ninapopata tatizo la body ya gari.
Hii imepelekea gari kuwa na rangi tofauti tofauti mfano mlango unakuta rangi imekolea upande mwingine imepauka etc. Pia wamekuwa wakijaza sana “puti” sasa imeanza kubanduka banduka na kuvimba vimba.

Nataka kupaka rangi loote. Gari ni Collora jeusi (metallic black).

Nilienda gereji kwa wachina pale Tazara kwa mbele (Sokota) roughly wakasema Mil 1.7 itagharimu. Na huduma itakua ni full rangi, full body repair, na marekebisho madogo madogo ya body. Ila wakasema ikitoka itakuwa kama imetoka kiwandani.

Sikufanikiwa kuona sample za kazi zao. Kwakuwa nilienda siku ya sikukuu so nilikutana na muhusika nje tu.

Naomba mwenye uzoefu au ushauri wa mahala ninapoweza kupata hii huduma kwa hali ya juu. Kwa bei rafiki zaidi.

Shukrani.
 
Kama hii sehemu unayoiongelea ni AutoBot wale wa pale Tazara vingunguti nakushauri waachie gari wafanye kazi!..
Hutojutia kuchangamka kwa bei zao!.
Unaweza kununua simu mtaani 90,000 halafu ikaharibika kioo ukaambiwa kutengeneza kioo ni laki mbili.
 
Kama injini yake nzima kabisa shuka nao mpaka moja then fanya kazi ila kama kuna vitu havipo sawa bora hata ubadili injini afu mambo ya rangi mbele kwa mbele kuliko kurekebisha rangi afu baada ya muda tu gari liwe linashinda gereji

Sent using Jamii Forums mobile app

Point ya maana sana hii.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama hii sehemu unayoiongelea ni AutoBot wale wa pale Tazara vingunguti nakushauri waachie gari wafanye kazi!..
Hutojutia kuchangamka kwa bei zao!.
Mkuu ni Sokota opposite na ile Total Shell geti lao limeandikwa tu China Garage.
 
Kama injini yake nzima kabisa shuka nao mpaka moja then fanya kazi ila kama kuna vitu havipo sawa bora hata ubadili injini afu mambo ya rangi mbele kwa mbele kuliko kurekebisha rangi afu baada ya muda tu gari liwe linashinda gereji

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani Boss. Nimekua nayo kwa Miaka 3 sasa. Kusema kweli Engine ipo vema. Uwa najitahidi kuwahi kubadirisha Oil na service za muhimu kwa wakati so sijaona Matatizo kabisa hadi sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom