• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Jinsi ya kunyamazisha watu wanaokusema eti kisa ''gari lako chafu''

E

EngineOil

Member
Joined
Sep 29, 2019
Messages
7
Points
45
E

EngineOil

Member
Joined Sep 29, 2019
7 45
2201927_kristina-flour-BcjdbyKWquw-unsplash.jpg

Umeshawahi kusemwa (au kuchekwa) na watu eti kisa ''gari lako chafu?''
2202132_IMG_20191029_142224.jpg

Unawajua hawa watu. Wanapenda sana kufuatilia mambo hayawahusu. Wasione kitu na wanaanza kukosoa. Hawajui unapitia changamoto gani kimasha. Wanakosoa bila kuelewa.

Je, ungependa ''kuwanyamazisha'' hawa watu wenye tabia ya kukusema eti kisa ''gari lako chafu?''

Huu ujumbe ni kwa ajili yako.

Naitwa Michael. Ni mmiliki wa Car Wash huku Kunduchi pembeni ya Hospitali ya RESA. Tunatizamana na kambi ya Jeshi.

Watu wengi wanadharau sana. Wako radhi wafuatilie mambo yako (na mambo ya watu wengine) badala ya kupambana na hali zao.

Watafuatilia kila kitu kuhusu maisha yako. Chakula unachokula. Nguo ulizovaa. Mpenzi wako. Kiatu ulichovaa. Utanashati wako. Mtu usipendeze na kuamua kujifanyia kitu kizuri na watu wataongea. Mtu usimpeleke mtoto wako ''international school'' na ndio kwanza kama umechochea moto hivi.


Kila sehemu unayoenda majungu hayaishi.

Na hizi fitna zinapitiliza mpaka kwenye chombo chako cha usafiri. Watakucheka na kukusema eti kisa ''gari lako chafu'' (inawahusu nini?) Hawajui unapitia kipindi gani katika maisha yako. Wanakosoa bila kuelewa.

Kama umewahi kukutana na watu wa aina hii...Njoo tukuoshee gari lako ili hawa watu wanyamaze milele.


Njoo Tunga'arishe Bodi Ya Gari Yako Kama ''Kiatu Cha Fundi.''

Ili kila sehemu unayopita uwaumize macho yao kwa usafi wa gari lako. Njoo tukupulizie parfume. Marashi yenye harufu nzuri kama mtoto wa kizanzibari. Ili ukiwapa lifti wajishtukie kwa harufu kali za miili yao.

Njoo tukutolee vumbi na matope kwenye makapeti na viti vya gari. Ili wasafishe miguu yao kabla ya kupanda kwenye gari lako.

Njoo tukuoshee gari Ili usifiwe kwamba unajua kutunza gari. Na kama ukitaka kuliuza liwe lina mvuto sokoni. Wale wote wanaokusema eti kisa gari lako chafu wanyamaze milele.


Sasa unaweza ukasema kwamba
''nina mfanyakazi nyumbani ambaye huwa anaosha gari langu''

Au ‘’kuna vijana ambao huwa nawatumia mtaani’’

Sababu zote hizo ziko sawa. Ni kweli huna huna haja ya kuoshewa gari na Car Wash. Kijana wako wa nyumbani (au mtaani) anaweza akawa anafanya kazi nzuri tu.

Uko sawa kabisa, mpaka unaposhuhudia rangi ya gari ikiwa imechubuka. Au, baada ya gari kuoshwa, kuna manyoya yamebaki kwenye vioo. Na hii siyo kwasababu kijana wako hajui kuosha gari. Ni kwamba tu kuna aina ya vitambaa maalum kwa ajili ya kuosha gari.

Kuna kitambaa kinaitwa soft. Kuna vitambaa ambavyo LAZIMA viwe vilani ukiwa unafuta gari. Na kuna kitambaa maalum cha kuosha matairi.

Waoshaji wa mtaani pia wanaweza wasiwe na mashine za kutoa vumbi ndani ya gari. Na kama unataka kuosha injini, wengi wao hawana mashine ya presha ili kuepuka kumwaga maji maeneo yanayoweza kuzima injini.

Changamoto zote hizi hazipo kwenye Car Wash yetu. Tuna mashine ya kunyonya vumbi, sisimizi, mate yaliyokauka, biskuti, n.k ndani ya gari. Na pia tuna mashine ya mkono(au presha) ili kuondoa vumbi na matope kwenye bodi ya gari, matairi, injini, na chini ya gari.

Gharama za huduma? Ni bei nafuu tu. Car Wash zote zile ambazo zinajielewa gharama zao ni kuanzia shilingi elfu kumi na mbili na kuendelea.

Sisi tunakufanyia kila kitu--kuosha bodi, kutoa vumbi na uchafu ndani ya gari, kuosha makapeti, kufuta viti, kupaka polish kwenye dashboard, kuosha injini(kama ukitaka)--kwa shilingi elfu kumi tu. Au shilingi elfu tano kama unataka kuosha bodi peke yake.

Ufanisi wa kazi ukoje? Tunajua kuosha gari au hizi ni ‘’bla-bla-bla’’ tu? Naomba uangalie picha hapo chini. Gari lako pia litafanana kama hapo chini. Tutakusafishia gari mpaka ling’ae kama kiatu cha fundi.

2202106_GARI_FUNDI_KUOSHA_GARAGE.jpg


Usalama wa gari yako je? Car Wash yetu ina fence. Unaweza ukaacha gari yako. Na ukarudi hata kesho na utalikuta. Kwasababu tuna milnzi na funguo za geti. Na kama hii siyo staili yako. Tuna eneo ambalo unaweza ukakaa ili uangalie gari lako likiwa linaoshwa.

Hakuna mtu atayekimbia au kuiba gari lako. Na unaweza ukaacha hata millioni 10 ndani ya gari yako. Haitaguswa hata shilingi elfu kumi.

Masaa ya kazi? Ofisi ziko wazi Jumatatu mpaka Jumapili. Kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa moja usiku.

Tunafanya service ya gari? Ndio. Kama unataka kubadilisha Oil, Oil fitler, Oil coolant, kuongeza mafuta ya breki, au labda unataka kubadilisha AC filter. Vitendea kazi tunavyo.


Gari lako litaoshwa mpaka ling'ae ''kama kiatu cha fundi.''

Na kama baada ya kuosha gari...wale watu wenye tabia kukusema...eti kisa gari lako chafu...hawatakaa kimya...njoo siku inayofuata na udai hela yako (Niko serious)

Gari lako lazima ling’ae au tutakurudishisa hela yako.

Ofisi ziko Kunduchi pembeni ya hospitali binafsi inayoitwa RESA. Tunatizimana na kambi ya jeshi. Au kama unataka maelekezo ya kwa njia ya simu, nipigie kwenye hii namba 0622 862 822.

Asante kwa kusoma,

Ni mimi rafiki yako Michael

Namba ya simu: 0710 888 996(whatsapp ni hiyo hiyo pia)

P.S.
Kama unampango wa kuja wahi mapema ili kuepuka usumbufu wa kukaa kwenye foleni. Na kama ukipiga simu na haipokelewi. Piga tena. Kwasababu naweza nikawa naongea na mteja mwingine muhimu kama wewe. Mungu akubariki.
 

Attachments:

Kambaku

Kambaku

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Messages
3,017
Points
2,000
Kambaku

Kambaku

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2011
3,017 2,000
Ziko wapi hizo picha kaka maiko?
 

Forum statistics

Threads 1,403,901
Members 531,427
Posts 34,438,330
Top