Kuota ukiwa shule

Kuota ukiwa shule

Ndoto muda mwingine sio za kuziamini maana kama jambo ambalo unalipenda sana kulifanya nna umekaa nalo kwa muda mrefu mara nyingi huwa linakutokea katika ndoto mfano mm napenda sana elimu ya astronomy kila siku usiku lazima nikague nyota zote angani na sayari mfano mwezi huu nafuraia sana kuona sayari tatu angani kwa macho yangu ambayo ni venus Jupiter na mars sasa kitendo hiki cha kupenda elimu ya nyota inanipelekea kuota sana mambo ya anga mara nyingi naoota nakuwa napaaaa naenda juuu natoka nje ya dunia yetu naenda mpk sayari nyingine huko mpk katika mwezi na sayari nyingine ktk ulimwengu mwingine naiona dunia ile sasa shida inanikuta njia ya kurudi duniani siiujui naanza kulia naamka 😁😁😁
 
Hiyo ndoto ni ujumbe kwako kwamba maisha yako yamerudishwa nyuma au umekwama kimaisha ni lazima uchukue hatua ujinasue kwenye hali unayopitia, usipuuze huo ujumbe.
Nimeamini kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kushindwa vibaya kimaisha na kuota ukiwa shule.

Kila siku huwa naota nikiwa shule na mara nyingi wakati wa mitihani na mara zote matokeo huja vibaya.

Kwenye maisha halisi sasa..vita ni kubwa sana

Kwani humu kuna mtu anaota akiwa shule na muda huo maisha yake yapo safi?
 
Huko kwenye maombi nafikiri nimemaliza maombi yote..waganga siwaamini sana
Ukiomba maombi ya kukataa ndoto hizo na hali ngumu unayopitia hakikisha unaambatanisha maombi na sadaka, usipuuze hili mkuu.

Ikiwezekana funga hata siku 3 ukifanya maombi ya kukataa hizi ndoto na ambatanisha maombi yako na sadaka......

Sadaka ina nguvu kubwa mno.
 
Ukiomba maombi ya kukataa ndoto hizo na hali ngumu unayopitia hakikisha unaambatanisha maombi na sadaka, usipuuze hili mkuu.

Ikiwezekana funga hata siku 3 ukifanya maombi ya kukataa hizi ndoto na ambatanisha maombi yako na sadaka......

Sadaka ina nguvu kubwa mno.
sana boss
 
Kuota upo shule inaweza kuwa na maana tofauti kulingana na muktadha wa ndoto yako na jinsi unavyoijisikia ndani ya ndoto hiyo. Hapa kuna baadhi ya maana ambazo kuota upo shuleni inaweza kuwa nazo:
  1. Maandalizi ya jambo muhimu: Kuota upo shuleni inaweza kuashiria kwamba unajiandaa kwa jambo muhimu, kama vile mtihani au kazi muhimu. Shule ni mahali ambapo tunajiandaa kwa maisha yetu ya baadaye, hivyo kuota upo shuleni inaweza kuwa ishara ya maandalizi yako kwa ajili ya siku zijazo.
  2. Kujifunza kitu kipya: Shule ni mahali tunapojifunza na kuendeleza ujuzi wetu. Kuota upo shuleni inaweza kuwa ishara kwamba unajifunza kitu kipya au unahitaji kujifunza kitu kipya.
  3. Kukumbuka jambo muhimu: Kuota upo shuleni inaweza pia kuwa ishara ya kukumbuka jambo muhimu ambalo unahitaji kulifanya au kuliangalia. Hii ni kwa sababu, kama nilivyotaja hapo awali, shule ni mahali tunapoandaa maisha yetu ya baadaye, hivyo ndoto ya shule inaweza kuwa ishara ya kukumbushwa juu ya mambo muhimu katika maisha yako.
  4. Kuhisi wasiwasi au mkazo: Kuota upo shuleni inaweza pia kuwa ishara ya hisia za wasiwasi au mkazo unaojisikia katika maisha yako. Hii ni kwa sababu shule inaweza kuwa na maana ya mtihani, shinikizo la kufaulu, na hata unyanyasaji kutoka kwa wenzako wa shule. Kwa hiyo, kuota upo shuleni inaweza kuwa ishara ya hofu yako au mkazo katika maisha yako.
  5. Kumbukumbu za zamani: Kuota upo shuleni pia inaweza kuwa ishara ya kumbukumbu za zamani, hasa ikiwa ndoto yako inakuonesha katika shule ambayo uliwahi kusoma. Hii inaweza kuwa ishara ya kutamani kumbukumbu za zamani au kukumbuka mambo ambayo yalitokea katika maisha yako ya zamani.
Ni muhimu kukumbuka kwamba ndoto ni za kipekee kwa kila mtu na inaweza kuwa na maana tofauti kwa kila mtu. Inashauriwa kuwa na utafiti na kujitathmini kwa undani kuhusu ndoto yako ili kuweza kuelewa maana yake.
 
Ukiomba maombi ya kukataa ndoto hizo na hali ngumu unayopitia hakikisha unaambatanisha maombi na sadaka, usipuuze hili mkuu.

Ikiwezekana funga hata siku 3 ukifanya maombi ya kukataa hizi ndoto na ambatanisha maombi yako na sadaka......

Sadaka ina nguvu kubwa mno.
nitalifanyia kazi hili.
 
Ndoto muda mwingine sio za kuziamini maana kama jambo ambalo unalipenda sana kulifanya nna umekaa nalo kwa muda mrefu mara nyingi huwa linakutokea katika ndoto mfano mm napenda sana elimu ya astronomy kila siku usiku lazima nikague nyota zote angani na sayari mfano mwezi huu nafuraia sana kuona sayari tatu angani kwa macho yangu ambayo ni venus Jupiter na mars sasa kitendo hiki cha kupenda elimu ya nyota inanipelekea kuota sana mambo ya anga mara nyingi naoota nakuwa napaaaa naenda juuu natoka nje ya dunia yetu naenda mpk sayari nyingine huko mpk katika mwezi na sayari nyingine ktk ulimwengu mwingine naiona dunia ile sasa shida inanikuta njia ya kurudi duniani siiujui naanza kulia naamka
Sayari ya tatu si Dunia (Earth)?
 
Back
Top Bottom