Kuota namulikwa na mwezi mchana

Kuota namulikwa na mwezi mchana

lian rich

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2016
Posts
303
Reaction score
291
Habari za siku mingi wakuu, Nina hii ndoto inanikosesha amani na sielewi ni nzuri au mbaya
Nimetoa ni mchana ila kutazama juu nikaona mwezi ndio upo wakati natembea nikagundua mwanga ni mweupe wa mbalamwezi badala ya ule wa jua tuliouzoea na watu wakaanza kunikagua na kunishangaa nimemulikwa na mwanga wa mwezi na wakaconfirm mwanga ule unaonimulika ni wa mbalamwezi ndoto ikaisha

Mwenye Kujua tafasiri msaada tafadhali manake nawaza ndio kufa au vipi
 
Sijui maana ya ndoto yako ila sio ya kawaida....
Sali sana kuna uwezekano una kipaji au uko tofauti na watu wote...sali na muombe sana MUNGU
 
Sijui maana ya ndoto yako ila sio ya kawaida....
Sali sana kuna uwezekano una kipaji au uko tofauti na watu wote...sali na muombe sana MUNGU
Nasali mkuu ila naogopa natamani nipate walau mwanga kidogo wa maana ya hii ndoto
 
Hii ndoto nilishawahi kuiota na maana yake siifahamu
 
Mwezi mchanga 🌙 ni symbol wanayoitumia waislamu kwenye minara ya majengo yao ya ibada.
 
Nasali mkuu ila naogopa natamani nipate walau mwanga kidogo wa maana ya hii ndoto
Kama unasali uoga ni wa nini? Kama ndoto yako umeona sio ya kawaida kaa katika imani yako sali na omba sana Mungu akufunulie ila ukitanguliza uoga mbele hautaelewa kamwe
 
Kama unasali uoga ni wa nini? Kama ndoto yako umeona sio ya kawaida kaa katika imani yako sali na omba sana Mungu akufunulie ila ukitanguliza uoga mbele hautaelewa kamwe
Sawa
 
Ktk vitu sijawahi kuvizingatia ni ndoto yaani nimekuwa nazipuuzia kiasi hata kama jana nimeota ukiniuliza asubuhi nilichoota nakuwa sikumbuki.
 
Kwa imani ya kikristo mwezi una wakilisha wazazi. Kumbuka ndoto ya Yusuf. So kwa ndoto yako maana yake ni kuwa unazo baraka za wazazi wako na kuna uwezekano ukafuata nyayo zao ktk mambo kadha wa kadha na ukafanikiwa.

Ni ndoto njema usiogope
 
Back
Top Bottom