๐—–๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ฑ๐˜‚๐—ฎ ๐— ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐— ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ถ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—บ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿณ

๐—–๐—ต๐—ถ๐—ป๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜‡๐—ถ๐—ป๐—ฑ๐˜‚๐—ฎ ๐— ๐—ฏ๐—ฎ๐—น๐—ฎ๐— ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ถ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐—ฎ ๐—บ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿณ

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,359
Reaction score
2,791
Hatimaye china imefanikiwa kuweka mpango madhubuti wa kuweza kuunda MbalaMwezi bandia nchini CHINA ifikapo mwaka 2027.

Dawa_20250718_150449_0000.png


Hebu fikiria unatoka nje na kutembea usiku wa manane unakutana na Mwanga mweupe laini , hakuna taa za Barabarani, hakuna umeme.

Juu unakuta sehemu kubwa inatoa mwanga ambao umetengenezwa na binadamu Kama mwezi vile unatoa mwanga usiku ili watu waweze kuona kama mchana.

Huo ndio mpango wa China mwaka 2027. Kioo cha satellite kilichoundwa kuakisi mwanga wa jua Kurudi Duniani. Uzinduzi wa kwanza kufanyika kwenye Jiji la Chengdu Mwaka 2027.

Inasemakana mwanga wake una nguvu mara 8 ya MbalaMwezi Halisi, lengo kubwa ni kupunguza gharama za Matumizi ya nishati mjini , vijijini nyakati za usiku.

Wasiwasi mkubwa ni Uchafuzi wa mwanga, kuvuruga mzunguko wa usingizi na kupelekea watu k kuzani usiku kama mchana.

#moon #artificialintelligence #china๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ณ #teknolojia #bongotech255 #fahamuzaidi #explorepage #technews
 
Ni zaidi ya history ya kale(babelioni) Hii ni technology issue. Fikiria wakati wakivumbua smartphone halafu wewe udai ni babelioni!
hata ujenzi wa miaka ya Babeli ilikwa teknolojia ya kiwangoncha juu, hata pyramids pia. uzuri ni jukwaa huru, hatuchaguliani cha kuamini. baki na unachokiamini
 
hata ujenzi wa miaka ya Babeli ilikwa teknolojia ya kiwangoncha juu, hata pyramids pia. uzuri ni jukwaa huru, hatuchaguliani cha kuamini. baki na unachokiamini
Ahsante kwa ushauri wako. Ila huu sio ubishi,ni points.
Je mungu hapendi au anakataza technology ya artificial moon?
 
Mtume wa dini fulani ataupasua vipande viwili kama alivyopasua mwezi.
 
Aisee sawa watu wanaoweza kufikiri na kuleta suluhisho la matatizo ije tu tuone itakavyofanya kazi.
Wahandisi wa Kitanzania tuna nini sie cha kuondoa matatizo kwetu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom