Kuota kwa Kiingereza

onlytruth

Senior Member
Dec 9, 2016
136
133
Asubuhi hii nimemsikia mwendesha kipindi LULU ZA KISWAHILI,TBC akisema kama we in Mswahili,hujui Kiingereza huwezi kuota kwa Kiingereza!
Naomba kutofautiana naye: Mimi naongea Kiingereza kwa kiwango cha chini( kadri),lakini kuna nyakati naota nikiwa kwenye mikutano,naongea Kiingereza cha hali ya juu(nagundua hilo baada ya kuamka na kukumbuka ndoto hiyo,na hata kuangalia kwenye dictionary yale maneno magumu niliyoyatumia ndotoni)
Kumbe kuota kwa Kiingereza inawezekana!
 
Nakuunga mkono hata mimi kiingereza changu ni kile cha pcm lakini kuna kipindi naota namwaga ung'enge utafikiri nilizaliwa kw malkia..

Ila kuna utafiti unasema huwez kuot mtu usiemjua, kwa maana sura mpya.. Watu wote unaowaota ni wtu ambao macho yako yashawahi kuwaona, hata kama ni kwa fraction of second lakin umewaona..

Hii nikiivuta katika lugha huwa naamin maneno yale ninayoota nayatamka aidha nimesoma sehemu ama nimesikia sehemu..
So hata kama hujui kiinhereza waweza ota yale uliyowahi kusikia.

Ila kama we ni mswahili hujawahi kukiskia kiingereza hta siku moja ni ngumu kuota unaongea kiingereza.
 
Asubuhi hii nimemsikia mwendesha kipindi LULU ZA KISWAHILI,TBC akisema kama we in Mswahili,hujui Kiingereza huwezi kuota kwa Kiingereza!
Naomba kutofautiana naye: Mimi naongea Kiingereza kwa kiwango cha chini( kadri),lakini kuna nyakati naota nikiwa kwenye mikutano,naongea Kiingereza cha hali ya juu(nagundua hilo baada ya kuamka na kukumbuka ndoto hiyo,na hata kuangalia kwenye dictionary yale maneno magumu niliyoyatumia ndotoni)
Kumbe kuota kwa Kiingereza inawezekana!

Unaweza hata kuota Kimasahi, tatizo liko wapi ? Au wewe ulifikiri labda Kiingereza ni nini? Ni Lugha tu!
 
Back
Top Bottom