Haoshi mtu vyombo bana unless muwe ndani ya ndoa changa.Hivi Bishanga kweli na umri huu kukura kakara mara nidondoshe misahani,mara ukoko unimwagikie,lol kwa lipi hasa,najipendekeza kwa nani,ili iweje?
Yaani kumbe ulikuwa unamaanisha visahani na vibakuli vya chakura. mimi nilifika mbali sana mpaka nikaweka hii scenario lakini sikuweza kupata jawabu
Viombo=Chama
Walaji= Mafisadi kwa ujumla wao
Chakula= Ufisadi
Kwababu chakula huchafua viombo, vivo hivyo ufisadi huchafua chama(viombo), baada ya vyombo kuchafuka ni lazima visafishwe, nani wa kusafisha? ni mapacha watatu tu swali bado linarudi pale pale kwanini mapacha watatu tuu.
Chombo hivyo chombo gani kiasi cha kupewa thamani nani akoshe? kwangu mie chombo thamani yake wakati wa kupakua na kula. Hayo ya kukosha na kusahaulika kabatini wala hayaniumizi kichwa.
Halafu mnajua umbile la chombo linachangia ladha ya chakula? Namaanisha, waweza kula usishibe, au mmoja wenu kuvimbiwa.
Nafanya kazi na mke wangu na wote tunarudi nyumbani tumechoka...hatuna house girl hivyo twafanya kazi zote kwa kushirikiana.
tunapika kwa pamoja,akiwa anapika mboga basi mie napiga ugali au wali...tukimaliza akiosha vyombo mi nina suuza.
jmosi na jpili sote tupo free.asubuhi ya jmosi ni usafi kwa kwenda mbele na jioni ni mtoko kwenda kusuuza nafsi.
jpili asubuhi ni ibadani na mchana no muvi zaidi na mambo mengine ya wakubwa.
hakuna ubwana wala utwana.
naomba hali hii isitoweke kamwe.
Mkuu wana kondoo walio wengi wameongoka karibuni na bado hawajaanza nena kwa lugha.
Tafadhali watazame nao pia kwani hawataelewa mafundisho haya.
alamsiki