Kuongezeka kwa ombwe kubwa la vijana wasio na ajira; Nini mtizamo wako ifikapo 2020?

mack4444

Member
Sep 4, 2016
6
2
hali ya ongezeko la vijana wengi waso na ajira nchini inazidi kuongezeka kila machweo hata wale walotegemea kuajiriwa na serikali kumetanda kiza nene wasijue hatima yao baada ya ahadi waloahidiwa kupita je kama hizi ahadi ndogo ndogo hazitimii kwa wakati uloaidiwa kwenye mass media je hizo ahadi kubwa kubwa za viwanda zitatimia kwa wakati au tutafika 2020 hali bado tete
 
Haijawahi kutokea ajira zikakosekana, hiyo nidhana inayoletwa na kuchagua kazi au kung'ang'ania mahala fulani, na hasa mjini.waje vijijini walime. Wanataka ofisi wote tukiwa viongozi au wanyakazi za ofisini nani atalima? Chakula hakikoasi soko ila kwa bahati mbaya sana!
 
Serikali ndio muajiri mkuu wa wana nchi wake kwa
1.Kuwapa elimu bora, itakayo wafanya, wajitegemee na waendane na ushindani hasa katika soko la kimataifa.
2.Kwa kuajiri yenyewe , watu wanao itwa watumishi wauma.
3.Kwa kuweka , kuandaa na kuhimiza uwepo wa mazingira mazuri ya taasisi binafsi ili zi waajiri watu mfano kuweka mazingira yanayo wavutia wawekezaji.
4.Kutumia faida ya rasilimali zake , ili kuongeza viwanda vikibwa na vidogo ili kufanya ajira zile zinazo hitaji nguvu kazi (unskilled labourers) kuwa nyingi, mfano kuweka sheria nzuri zitakazo leta faida kwenye sekta ya madini na utalii

Tujiulize serikali ya sasa ina fanya kitu gani kati ya hivo hapo zaidi ya kufanya matamko na kutumbuana tuu!!?
 
Back
Top Bottom