Kuondolewa Motor Vehicle Licence janga kwa wananchi wa kawaida

Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.

Unaongea utumbo. Kuna wataalamu wametafakari jambo hilo kwa kina. Wadau wengi wameshirikishwa kutoa maoni yao. Kwanza wewe ni nani mpaka ufike mahali useme eti hukubaliani nacho?
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Unashindwa kukubaliana vp na kitu ambacho tayari kina subiri UTEKELEZWAJI....!!

Ni wewe uliye leta Mada Jamvini...!
Nilitegemea usikilize na upate maoni ya WADAU wanasemaje...?

Umehitimisha MADA yako kwa kuonesha unapingana na MABADIRIKO hayo yaliyo fanywa na TRA wakiiwakilisha Serikali..

Je ulipenda ama unapenda wengine wote TUUNGANE na wewe KUPINGA hili...!!?

Ok...wacha nipite waje wengine....
 
Tumelishwa kulalamika OK,,, twendeee,,, jiulize vyakula toka %5 hadi 2%,uwekezaji nmesikia kuna vitu vmepunguzwa kodi ili kuvutia ujenzi wa viwanda na uwekezaji,,, huon itakuwa furaha kwa wananchi??
Uwekezaji bila umeme?umeme huu wa mshumaa ndio mnajivunia?
 
Wacha nikaweke oda ya gari yadi kabisa manake mateja watamiminika kwenye mayard ya magari, sasa tunarudi mtindo wa zamani mama ana gari yake mtoto ya kwake, nikivaa suti nyeusi natoka na benz nikivaa jeans natoka na hilux ya blue.
Mkuu nadhani hujaelewa kodi inayo zungumziwa. Importation tax ipo palepale.
 
Wacha nikaweke oda ya gari yadi kabisa manake mateja watamiminika kwenye mayard ya magari, sasa tunarudi mtindo wa zamani mama ana gari yake mtoto ya kwake, nikivaa suti nyeusi natoka na benz nikivaa jeans natoka na hilux ya blue.
Gharama imehamishiwa kwenye wese mkuu,unafuu upo tu kama gari halitumiki
 
Acha iondolewe. Mfano umeenda nje ukakaa huko miaka miwili gari haiko barabarani. Ukirudi unalipia road licence au motor vehicle wakati hujaitumia na penalty juu. Huu ulikuwa ni wizi mkubwa. Hii ni nzuri. Sema kwa upande mmoja yule anaetumia mafuta ya taa au petrol kwa ajili ya generator itakuwa imekula kwake. Ila kwa wenye magari hii ni bombaaa
Mimi nimefurahi kuwanyima ulaji trafic maana kila wakikusimamisha breki2ya kwanza ilikuwa kwenye ll
 
Kwa tusio na magari, hii ni ngumu kumesa. Kuna mtu enzi za TZ.. nulimuuzia mkoko wangu, zilipoanza namba mpya akabadili namba kwa kutumia
jina langu. Siku nilipocheck TRA, nikakuta nadaiwa limbikizo la miaka 10, zaidi ya 2.2m wakati gari yenyewe sijui iko wapi! Nashukuru serikali imetoa msamaha wa jumla.
 
Mafuta ukiyapandisha bei yanaathiri watu waote wenye magari na wasio na magari.
Wakati Road license ilikua inaathiri wenye magari tu.
Mafuta yakipanda watu wote tunaumia.
 
Pia usafiri ukiwepo wa daladala, USAFIRI WA VIJIJINI .A MIKOANI LAZIMA GHARAMA ZIPANDE KUFIDIA MAFUTA. TOFAUTI NA MWANZO KUWA KAMA UNA GARI UNA UWEZO WA KULIPIA KODI WEWE MWENYEWE HII INA MADHARA KWA MLAJI WA MWISHO
 
Back
Top Bottom