Kuondolewa Motor Vehicle Licence janga kwa wananchi wa kawaida

Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Hamnaga jema na hayajakukuta. Nikupe mfano mimi miaka iliyopita nilimpatia dereva wangu kigari ili aanzie maisha hasa kutokana na kufanya kazi vizuri ili naye abangaize. Naye akamuuzia jamaa ambaye aliuza kama screpa. Kumbe hawakubadili jina, juzi naenda kuangalia TIN nikakuta nadaiwa kama million tatu za MVL ya hilo gari. Nilipoandika barua ya kuomba iondolewe katika system wakasema nilipe nikali ila wakadai kabla ya kuiondoa lazima nilete Vehicle Inspection Report la sivyo itabaki katika system na niendelee kuilipia kila mwaka. Imagine!
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Hata wenye magari ni wananchi, kuna kodi nyingi sana wenye magari wanachangia kuanzia kuingiza gari, kununua mafuta, leseni ya barabarani, vipuli nk, hivyo ikiondolewa ni sawa kabisa au ipunguzwe
 
Wacha nikaweke oda ya gari yadi kabisa manake mateja watamiminika kwenye mayard ya magari, sasa tunarudi mtindo wa zamani mama ana gari yake mtoto ya kwake, nikivaa suti nyeusi natoka na benz nikivaa jeans natoka na hilux ya blue.
Sio kweli, hii inalipwa mara moja kwa mwaka na sio kikwazo cha watu kununua magari
 
Well,

Unadhani kati ya hiyo fee iliyoondolewa na gharama ya mafuta kuongezeka ipi inazidi ingine...??assume unamiliki gari na unatumia mafuta?? Baada ya hapo ndio unaweza ku draw concl..pia sasa ushuke chini wa wasio na magari ila consider kua nauli za mabasi au vyombo vya moto vina uhusiano na road licence fee..kisha relate na mwananchi wa kawaida kama ulivyotaka.....simply angalia multiplier effect ya mabadiliko ya vyote
Ndiyo hapo nasema, hii Road license ilikuwa na athali kwa kundi dogo, ila Mafuta yataleta mathara kwa kundi kubwa!
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.
Nilijibu kuwa ni wazo zuri huko nyuma, ila tuongezee vipengele vingine kama:-
  • Itakuwaje kuhusu yale magari ya thamani? Maana lazima yalipiwe licence..
  • Magari yanayotoa moshi sana kama malori na magari makubwa, hasa ya kizamani...
  • Magari mazito na yenye engine kubwa..
  • Magari fulani fulani hayatakiwi kukatwa kodi kama ambulances, mashine za hospitali na zingine zenye exemptions..
  • ...n.k.
Maana haiwezekani vyombo vyote vitumiavyo petroli na dizeli vikatwe kodi inayolingana, hili swala wameliharakisha, walitakiwa wasiwe na haraka nalo kabisa..
 
Acha iondolewe. Mfano umeenda nje ukakaa huko miaka miwili gari haiko barabarani. Ukirudi unalipia road licence au motor vehicle wakati hujaitumia na penalty juu. Huu ulikuwa ni wizi mkubwa. Hii ni nzuri. Sema kwa upande mmoja yule anaetumia mafuta ya taa au petrol kwa ajili ya generator itakuwa imekula kwake. Ila kwa wenye magari hii ni bombaaa
Ikiwa ulitakiwa kulipia June kuna haja ya kulipa?
 
Kumbuka hata nauli za mabasi zitapungua! Kuna malori kibao yamekatwa, kisa road license, sasa yatafanya kazi na mazao yatasafirishwa!
 
Waache washangilie bila kujua mashine za kusaga nafaka huko vijijini kwao zinatumia mafuta... hawajui gharama zitaongezeka kwa mitambo/mashine/majenereta zinazotumia mafuta japo haitumii barabara... Na hawajui kama gharama zitaongezeka, mzigo utahamishiwa kwa walaji wa mwisho ambao ni ndugu zao huko.

Labda kama kuna vituo maalum vya mafuta kwa ajili ya mashine/mitambo inayotumia mafuta.
teh teh, ongezeko la shiling hamsin kwa mia,... lita 100 shiling elfu 5,

watu wengine mlipaswa kua na vipara tu
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Ngoja gharama zipande na mimi naomba wapindishe kabisa ili sisi tunaojiita WANYONGE, tunyongwe kwa vitendo co maneno tu hata km nauli ya kutoka kituo kimoja had kingine iwe 1000, ama 1500 nitaunga mkono...sisi wa maisha ya chini ndo tulioiweka hiyo serikali eti hatuwezi kubadili (...CM) kwamba kilituletea uhuru!. Wakat tunasahau hata aliepigania huo uhuru ashatangulia mbele za haki!. So na cc tungepaswa na hiki (....) Tukitangulize nyuma ya demokrasia. WAPANDISHE TU mpaka ndamu itutoke labda tutajifunza cc tunaojiita wa maisha chini tupo zaidi ya 60% tunashindwa nn???.

Kisheria "the aim of punishment is to deter the offender from doing that wrongful act again"
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
Wengi watachukua muda sana kuelewa athari yake. Tutaumia sana kwenye mafuta na athari zake zitaenda kwenye maisha ya watu wa hali ya chini
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.

Tutaacha lini kulalamika kwa kila kitu? Road license kwa jinsi ilivyokuwa ikitozwa imelalamikiwa sana si hapa jamvini tu bali katika nyanja kibao. Katika nondo za haja zilizowahi kuwapo hapa ukumbini kuhusiana na hili ni pamoja na hii hapa chini:

MFANO HALISI: Road License inavyoikosesha serikali mapato

Hakika kama hata kwa hatua hii ya kufahamu Road License haipaswi kuwa kama ilivyokuwa au kutozwa hata kwa magari yaliyo mabovu na bado tunalalamika, basi wengi wetu tutakuwa na maradhi yasiyoweza kutibiwa - kwa maana tutakuwa hakika hatujui nini tunataka.
 
kuondoa hii kodi ni jambo jema mno mathalani kwa wale walio kuwa wana lipa sh 230,000 kwa ajili ya motor vehicle licence, atahitajika kununua lita takribani 479 kwa mwezi ili kuweza kucover hiyo pesa hasa kama ongezeko ni sh 40 kwa lita

hivyo serikali imepunguza hii kodi kwa kiwango kikubwa tu
 
Kuna mama mjane kadaiwa MVL kwa gari alilouza mumewe miaka kumi iliyopita na aliyeuza alilikata screpa yaani majanga,

jamaa yangu musukuma pale ofisini kwake anauza screpa za maroli na mabasi kote anakoyanunua yanadaiwa.
 
Moja ya Kitu Serikali ilichofanya cha ajabu ni Kuondoa Motor Vehicle Lisence kwa Magari na kuipeleka kwenye Mafuta.

Hili Jambo litaenda kuathiri Uchumi wa Mtanzania kuwa Mbaya zaidi. Kumbuka Nishati ya Mafuta ndiyo kila kitu. Hii itaenda kufanya bidhaa kupanda gharama ya kununua, nauli kupanda na mwishoe kuathiri maisha Mazima ya Mwananchi wa Kawaida.

Pia itaathiri mfumko wa bei na maisha yatazidi kuwa Magumu. Kipengele hiki Sikubaliani nacho kabisaa.

Ni maoni yangu tu haya.
inaonyesha.hujawahi miliki gari.hata thread nyingi tulizoweka humu kulalamikia hiyo kodi hukuwahi kuzisoma.unahabari kuwa tulikuwa tunatozwa hiyo kodi hata kwa magari yaliyojuu ya mawe/yaliyouzwa chuma chakavu/spea/yaliyoibiwa etc
wameelewa kilio hiki.wamiliki wa magari tumewaelewa.kodi hii haina impact kwa mkulima bado ipo kwa mmiliki mtumia/ barabara.
usipotoshe watu humu tafadhali
 
teh teh, ongezeko la shiling hamsin kwa mia,... lita 100 shiling elfu 5,

watu wengine mlipaswa kua na vipara tu
We mwenye kichwa chenye nywele nyingi unaona ni sawa kabisa kwa mtambo usiotumia barabara ulipe shs 5,000/= kama kodi ya barabara wakati mtambo huo hautumii barabara...

Hizi shule siku hizi mnaenda kusomea ujinga??
 
Sasa mbona ulichoelezea havina uhusiano, si ikiondolewa gharama za uendeshaji magari utapungua kwa kuondoa mlundikano wa kodi kandamizi, au?
Anachomaanisha ni kwamba kile kidogo au kwa wingi wake ambacho walikuwa wakikitoa wachache wenye magari baada ya ondoleo hilo itabidi kitafutwe kupitia waTanzania wote hata Bibi yako aliyeko kule Kibiti ambaye hajui hata gari ni kitu gani na kinafananaje!!!
 
Back
Top Bottom