Kuondoka kwa Harmonize WCB tutegemee Mwisho wa Ali Kiba?

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,317
Ni siku chache zijazo, tutaanza kuzisikiliza nyimbo za Harmonize bila kibwagizo cha ‘Wasafi Records’ na ‘Eyo Laiza’. Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake halisi ni Rajab Abdul Kahali ameandika barua ya kujitoa katika lebo ya Wasafi Records.
Msanii huyo ambaye nyimbo zake za ‘Kwangalu’ na ‘Show Me’ zimeleta gumzo nchini, bila shaka ataleta upinzani mkubwa kwa wasanii wa lebo hiyo akiwamo Diamond mwenyewe.
Kwa sababu Harmonize ameishi WCB, anajua nguvu yao, anajua udhaifu wao, anajua sehemu ya kupita na kufanya vitu vya tofauti.
Licha ya watu wengi kudhani kuwa WCB itatetereka, hali haiwezi kuwa hivyo kwa sababu Diamond na wenzake wataamka na kufanya vitu vya tofauti zaidi wakijua sasa wapo katika mapambano halisi.
Hilo haliwezi kukwepeka kwa sasa kwamba Diamond atajipanga zaidi kwa sababu katika akili yake anajua kuwa Harmonize anakwenda kuwa mpinzani wa kweli tofauti na Ali Kiba, ambaye upinzani wake umetengenezwa zaidi na mashabiki.
Ushindani huo unaweza ukampoteza kwa muda Ali Kiba, ambaye mashabiki wamekuwa wakilazimisha ili aonekane kuwa mpinzani wa Diamond.
Utajiuliza kwanini mashabiki wanalazimisha? Hoja hapa ni kuwa unamlinganishaje msanii ambaye kwa mwaka anatoa nyimbo zaidi ya 10 na mwingine ambaye anatoa wimbo mmoja.
Ni rahisi kutetea kuwa idadi haijalishi, lakini ni ukweli kuwa Diamond anafanya muziki kibiashara tofauti na Ali Kiba, ambaye kwa kiasi kikubwa anafanya kama ‘kujifurahisha zaidi’. Bila shaka mashabiki wa Ali Kiba na wale wanaomchukia Diamond, kwa muda fulani watashangilia chochote kinachofanywa na Harmonize na kila wimbo wa msanii huyo utapendwa na kundi hilo la mashabiki bila kujali kiwango chake.
Kwa namna fulani jambo hilo linaweza kufanya ushindani wa Diamond na Harmonize kuwa mkali kwa muda fulani na hasa itategemeana na jinsi Harmonize atakavyoondoka WCB kama ni kwa shari au kwa amani.
Kwa vyovyole vile, upinzani wa Diamond na Harmonize unaweza kufunika nyota ya Ali Kiba kama akishindwa kucheza karata zake vizuri.

Copy n Paste from
mwananchi Official IG
 
200% true.
Alikiba aliishi kwa hisani ya wasiopenda maendeleo ya Diamond, nao sasa watahamishia majeshi kwa Harmonize

Bora waeendlee kumshangilia Alikiba...Mana Konde boy kila kitu anachokifanya anahakisi kutoka kwa Domo hadi ile ya kuvimbisha na kutanua mdomo.....Kivuli cha Diamond hiko.
 
Ni siku chache zijazo, tutaanza kuzisikiliza nyimbo za Harmonize bila kibwagizo cha ‘Wasafi Records’ na ‘Eyo Laiza’. Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake halisi ni Rajab Abdul Kahali ameandika barua ya kujitoa katika lebo ya Wasafi Records.
Msanii huyo ambaye nyimbo zake za ‘Kwangalu’ na ‘Show Me’ zimeleta gumzo nchini, bila shaka ataleta upinzani mkubwa kwa wasanii wa lebo hiyo akiwamo Diamond mwenyewe.
Kwa sababu Harmonize ameishi WCB, anajua nguvu yao, anajua udhaifu wao, anajua sehemu ya kupita na kufanya vitu vya tofauti.
Licha ya watu wengi kudhani kuwa WCB itatetereka, hali haiwezi kuwa hivyo kwa sababu Diamond na wenzake wataamka na kufanya vitu vya tofauti zaidi wakijua sasa wapo katika mapambano halisi.
Hilo haliwezi kukwepeka kwa sasa kwamba Diamond atajipanga zaidi kwa sababu katika akili yake anajua kuwa Harmonize anakwenda kuwa mpinzani wa kweli tofauti na Ali Kiba, ambaye upinzani wake umetengenezwa zaidi na mashabiki.
Ushindani huo unaweza ukampoteza kwa muda Ali Kiba, ambaye mashabiki wamekuwa wakilazimisha ili aonekane kuwa mpinzani wa Diamond.
Utajiuliza kwanini mashabiki wanalazimisha? Hoja hapa ni kuwa unamlinganishaje msanii ambaye kwa mwaka anatoa nyimbo zaidi ya 10 na mwingine ambaye anatoa wimbo mmoja.
Ni rahisi kutetea kuwa idadi haijalishi, lakini ni ukweli kuwa Diamond anafanya muziki kibiashara tofauti na Ali Kiba, ambaye kwa kiasi kikubwa anafanya kama ‘kujifurahisha zaidi’. Bila shaka mashabiki wa Ali Kiba na wale wanaomchukia Diamond, kwa muda fulani watashangilia chochote kinachofanywa na Harmonize na kila wimbo wa msanii huyo utapendwa na kundi hilo la mashabiki bila kujali kiwango chake.
Kwa namna fulani jambo hilo linaweza kufanya ushindani wa Diamond na Harmonize kuwa mkali kwa muda fulani na hasa itategemeana na jinsi Harmonize atakavyoondoka WCB kama ni kwa shari au kwa amani.
Kwa vyovyole vile, upinzani wa Diamond na Harmonize unaweza kufunika nyota ya Ali Kiba kama akishindwa kucheza karata zake vizuri.

Copy n Paste from
mwananchi Official IG
Sasa hapa Tanzania kuna msanii anayeitwa alikiba kweli au ajuza kiba?
 
Mkataba wake na WCB ulikuwa wa miaka 15 na masharti kibao. Tuombe Mungu avuke kizingiti hicho. Ndio maana mameneja wa WCB wanacheeeeeeeka
 
Huyo alieandika Hilo gazeti pamoja na mtoa mada mnawaza kwa kutumia makalio yaani harmo ashindane na baba wa mziki wake?role model wake?mtu ambaye media kubwa Kama clouds,east Africa tv zimeshindwa kumbambana nae? Et awe harmo?hiki ni kichekesho Cha Karne aisee ! Kwanza umeona alichokiandika Leo kwenye Instagram yake akimshukuru mkubwa wake diamond kwa kufanya ngoma yake aliyemshirikisha mondy mwenyewe iwe kubwa pia na kufikishwa viewers mil 50 wakati hakuna hata ngoma yake nyingine iliyofika viewers wengi km hiyo.Ebu mwacheni harmo awe free msimwingine ktk Mambo yataomfanya arudi nyuma kimziki diamond Hana mshindani na hakutatokea mshindani wake kwenye ardhi hii ya bongo.
 
Ali hawezi shindana na Mond, wala harmonize walioshindana nae wote hapo awali hawapo wamepotea

why?

Kiba hatoi back to back!..anaweza akakaa miaka miwili akatoa hit song kisha akapotea!!...kujua anafanya nini ana uwezo gani ni ngumu, huyu wataisha akina Mond na wote mnaowajua yeye atabaki!'

Kama mtaishi maisha marefu, Kiba atatoa nyimbo mpaka uzeeni..iko damuni, na hana mzuka wa kushindana na mtu

Kwa hiyo uko sahihi, Kiba yuko level zingine, miziki mingine, vision tofauti na hao

Hata miaka sita anaweza kukaa kimya, siku akitoa anafuta zingine kwa muda na anakuwa kama "yuko kila siku kwenye game"
 
Huyo alieandika Hilo gazeti pamoja na mtoa mada mnawaza kwa kutumia makalio yaani harmo ashindane na baba wa mziki wake?role model wake?mtu ambaye media kubwa Kama clouds,east Africa tv zimeshindwa kumbambana nae? Et awe harmo?hiki ni kichekesho Cha Karne aisee ! Kwanza umeona alichokiandika Leo kwenye Instagram yake akimshukuru mkubwa wake diamond kwa kufanya ngoma yake aliyemshirikisha mondy mwenyewe iwe kubwa pia na kufikishwa viewers mil 50 wakati hakuna hata ngoma yake nyingine iliyofika viewers wengi km hiyo.Ebu mwacheni harmo awe free msimwingine ktk Mambo yataomfanya arudi nyuma kimziki diamond Hana mshindani na hakutatokea mshindani wake kwenye ardhi hii ya bongo.

mkuu kwani diamond alitokea wapi? na kabla yake nani alikuwa juu kimuziki? na ikawaje akatoboa?

umeandika kwa mahaba

ila mziki hata wewe ukiimba leo utapata washabiki

Diamond bila drama zingine hana nguvu hiyo

wakiimba Live hapa akina aslay, marioo rayvanny wanamkalisha, ni promo

kikubwa usipate na mahaba mpaka kujiapiza
 
Back
Top Bottom