Kuombwa hela, kutoa hela na kuhonga katika mapenzi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,139
33,201
Habari wadau.

Kitendo Cha kuhonga katika mapenzi Ni kitendo Cha asili.toka zama za mababu wanaume walikua wakiwahonga wapenzi wait vitu mbalimbali mfano khanga,vitenge,nguo,viatu,vipodozi,hell na Vito vya thamani. Mambo haya yalifanyika kabla ya kumpata mwanamke na baada ya kumpata mwanamke.

Wakati wa harakati za kumtongoza mwanamke,wanaume walikua wakipenyeza baadhi ya vitu tajwa happy juu ili kurahisisha tongozo.

Pia waliendelea kutoa vitu hivyo hata pale walipokua wamekubaliwa au kupata walichokitaka ili kudhibiti penzi( ku maintain).

Wanaume makini waliendelea kuhonga ama kutoa vitu nilivyovitaja hata kwa wake zao. Utakuta mwanaume akitoka Kazini anapita sehemu ananunua kitu anampelekea Mke wake,mfano anapita sehemu anapiga bia zake mbili anaoondoka anaweza kuchukua nyama choma au mishikaki na kumpelekea mke wake.

Kumnunulia nguo , viatu na vipodozi mke wake Wala sio swala la kuuliza.Wengi huwanunulia wake zao licha ya kuwapa hela ili wakajinunulie wenyewe.

Nia na madhumuni Ni ili mke afurahi ama apendeze. Wengine huwanunulia wake zao hata vitu vidogovidogo Kama zawadi,mfano pipi,biskuti,korosho,karanga,chokolate na vitu Kama hivyo Kama zawadi tu.

Zawadi au hongo zote hizo Ni mapenzi tu.

Hata hivyo ndani ya ndoa Mke pia pamoja na kupewa au kuletewa vitu vyote hivyo Kuna mda huweza kuomba anunuliwe kitu fulani ama huomba fedha taslimu kwa ajili ya shida yake.

Mambo yote hayo hayatofautiani saaan na mwanaume kumpa au kumfanyia Girlfriend wake,mchepuko wake,anaemtongoza au vinginevyo,Nia Ni hiyohiyo Kama ya mke ndani ya ndoa.

Shida iko hapa,
Umekutana na msichana au mwanamke,Ni wewe ndio umemwanza,hukua na mazoea nae,umemtongoza kwa Mara ya kwanza kabla ya kumuambia shida yako "anakupiga mzinga."

Kwa kawaida wanaume wengi kama Ana kakipato na ana mapenzi ya kweli Ni lazima ampe hela mpenzi wake,amtoe outing,ammpe zawadi hata bila kuombwa.

Hi ni Tabia ya asili kabisa haijalishi mwanamke Ana kipato kumshinda mwanaume au Hana kipato kumshinda mwanaume

Utashangaa na kujiuliza huyu msichana mbona hakuniomba hela kabla sijakutongoza ?

Ila mkae miijua kuwa kutongoza raha Sana,na kuhonga pia raha Sana.
 
^Taifa halitajengwa na watu wabovu kichwani, wabovu mwilini, wabovu moyoni, wabovu karibu katika kila nyanja ya maisha^ ~ JKN, Baba wa Taifa.
 
Back
Top Bottom