mkirua vunjo
Member
- Nov 11, 2011
- 25
- 5
Jamani naona kweli kwa upande wangu ni kichekesho kikubwa sana, inakuwaje mtu uombe upigiwe kura wakati wewe mwenyewe hujajiandikisha!
Naomba ma great thinkers mjaribu kuangalia hili.
Ni kwamba Mgombea wa CCM Arumeru Sioi Sumari hajajiandikisha kupiga kura popote Tanzania, sasa leo anakuja kuomba kura, hii inakuwajie
Jamani naona kweli kwa upande wangu ni kichekesho kikubwa sana, inakuwaje mtu uombe upigiwe kura wakati wewe mwenyewe hujajiandikisha!
Naomba ma great thinkers mjaribu kuangalia hili.
Ni kwamba Mgombea wa CCM Arumeru Sioi Sumari hajajiandikisha kupiga kura popote Tanzania, sasa leo anakuja kuomba kura, hii inakuwaje
Nadhani na hapo taratibu zitampinduliwa apige kura
Ili kugombea ubunge hakuna sifa ya kwamba lazima uwe umejiandikisha kama mpiga kura kwenye jimbo unalogombea au mahali pengine popote TZ.
Kama mnataka hiyo sheria itungwe basi pendekezeni kwenye katiba mpya na mtaona madhara yake. Itakapowakata mnaowataka msije mkalalamika.
Point hapa ni kwamba uandikishwaji wa wapiga kura kwa TZ haufanywi kila siku. Kuna vipindi maalum ambapo watu huandikishwa na mara nyingi wanaandikishwa kwenye sehemu wanazokaa.
kwa mfano Watanzania wote wanaokaa nje ya nchi hawatakuwa na nafasi ya kugombea uongozi wowote Tanzania. Hivyo hivyo watu wengi wanaofanya kazi mbali na kwenye wilaya zao za kuzaliwa hawataweza kugombea huko maana watakuwa hawajajiandikisha huko.
Tusianze kutaka sheria zetu zifuate matakwa yetu kisiasa, madhara yake huko mbele yatakuwa makubwa mno. Ila kama Watanzania tunalitaka hili basi tupendekeze kwenye katiba mpya.
Inasemekana alijiandikisha kupiga kura Kenya