Kuomba hela mwanaume/mpenzi

Aisee wewe ni wa kitofauti sana,wenzako wanaomba hadi hela ya kula kuonesha kwamba kwao ni dhiki kali
 
Nampenda binti anayekuwa muwazi kwangu kwa kunieleza changamoto zake zikiwemo za kiuchumi. Hii inanipa Imani & nafasi ya kuprovide, ndicho tulichoumbiwa wanaume na Mungu.

"Searching, getting, then provide ... It might be your family, parents, spouse etc...!"

Kwa sisi wenye salary kila mwezi tunajua kabisa kuna kipindi ACCOUNT haisomi mpaka unaamua kucheki na washkaji. Sasa, kwa binti hata naye akiwa na kazi kuna kipindi atayumba tu.

Swali: Kama hujawahi kuomba kwake, unaomba wapi?!!! Usiniambie kuwa hujawahi kuwa na changamoto za kiuchumi.

Anyways, tunatofautiana mtazamo.
 
Kuna kipindi nilikuwa field mahali na mdada mmoja wa ujeruman arusha. Siku moja akaniomba nimpeleke masai camp tukapanda kifodi/haice nauli njiani akalipa yake tu. Baadae hotelini mchana akalipa bill yake tu..nilimpenda saana huyo mdada
 
Wenzio hawaombi, wanadai kabisa. Utaona msg, 'baby sasa ile hela vipi nachelewa saluni mwenzio' kama vile aliiweka.
 
Inaelekea wote wamesomea chuo kimoja maana maneno hayatofautiani hata chembe. Hiyo stori ya mzigo kuna mmoja alishataka kunipata, nikamuuliza mzigo gani akadai vitenge vinakuja na bus toka congo. Nikamwambia isiwe shida twende tukachukue, tuliganda Ubungo masaa mawili hakuna cha mzigo wala basi la kutoka congo.
 

Wanaomba mpaka wanakera
 
Hongera naheshimu sana mwanamke/msichana wa hivi hiyo ni tabia nzuri usiichokonoe utapata matango pori,msichana wa hivi atakula hela yangu
 
Ni kweli kuna mtu ambae Hana changamoto.Lakini huwa ananipatia mwenyewe, Kama kweli anakupenda atajua wajibu wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…