Habarini wa JF!
Kwa vijana wa zamani, nadhani mtakuwa mnakumbuka jinsi mila zetu za Kiafrika zilivyokuwa, kwa kijana hasa wakiume akitaka kuoa enzi hizo. Kwa ninavyokumbuka kwa makabila yaliyo mengi (Wajita, Wanyamwezi, Wasukuma) kuoa kwa kijana ilikuwa mpaka familia ya muoaji imejiridhisha vya kutosha juu ya mwenendo wa msichana na familia yake, tabia za ukoo ule ikiwemo na maradhi ya kuridhishana n.k. Hii ilikuwa na faida kubwa sana ktk ndoa hizo. Kiukweli ndoa za namna ile zilidumu sana.
Mara nyingi uchunguzi wa muoaji ulifanywa na ndugu/mtu wa karibu na kijana husika paspo familia/ukoo pamoja na msichana kujua kuwa anachunguzwa juu ya mienendo yake. Uoaji wa namna hii uoaji wa network (chunguza kwanza, jiridhishe na oa/olewa).
Kwa mkitadha huo, mimi napenda kufahamu kwa uzoefu
1. Je uoaji wa network bado unaendelea na kama ndiyo, ni wapi?
2. Je upi mtazamo wako juu ya uoaji / uolewaji wa namna hii?
3. Je ukitaka kuoa/kuolewa haraka lazima kijana wa kiume/kike awe na network?
4. Kwa mabadiko ya kijamii tuliyonayo leo, ndugu walio wengi hatujuani. Je kijana akitaka kuwa na network juu ya jambo hili, zipi ni network wanazoweza kuzitumia vijana kujipatia wenza wao?
Karibuni kwa michango yenu.