Vivuko vyote viwe na "life rings" za kutosha na maboya mengine ambayo bamna yake inalingana na namba ya abiria na wahudumu mpaka nahodha.
KIla sehemu yenye kivuko iwe na boti ndogo ambazo zina waokoaji wa dharura na wameajiriwa kwa kazi hiyo.
Pia kila boti iwe na vifaa vyote muhimu maboya, matairi, na kila aina ya kifaa cha uokoaji.
Vijana wa ukokoaji wawe wameingizwa kabisa kwenye payroll ya idara ya mafa kila sehemu yenye kivuko.
KIla sehemu ya ivuko pawe na utaratibu wa kuchuja abiria kwa kweka uzio maalum au "barriers" ambapo mkataji tiketi anaambiwa kwamba namba imetosha na sehemu ya kupita kwenda ndani ya kivuko inafungwa.
Kwa mfano kwenye MV Nyerer namba ya tiketi ikifiikia 101 ambayo ndo namba ya abiria wanaoruhusiwa kuingia kwenye ivuko basi inapigwa stop, na abiria wengine wanangoja kivuko kiende na kirudi.
Serikal iijaribu kuwekeza zaidi kwenye sekta hii ya vivuko kwani vikiwa zaidi ya kimoja, vitasaidia suala la usafiri na pia vivuko hivi vitaiingizia mapato serikali yenyewe.
Mwisho, serikali iruhusu watu binafsi waingize vuvuko vyao na wafanye biashara hii badala ya kutegemea vuvuko vyake ambayo inashindwa kuvisimamia kupitia wasimamizi wake.