Kuogelea kusingekuponya ajali ya MV Nyerere

nyabhera

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2011
Posts
670
Reaction score
740
Haki ya Mungu kunawatu mnahitaji toba. Watu mliowadhihaki waliokufa maji huko Ukara eti wameshindwaje kuogelea mita 50 tu. hamjui nini maana ya chombo cha majini kupinduka majini, hili ni tukio la dakika moja kila mtu yuko majini kila mtu anataka kupona kila mtu anamshikilia mwenzie kama ndiye boya lake bro usiombe. Hapo kupona ni bahati tu si suala la kujua kuogela ama lah. Watu wengi hufa kwa sababu ya kunganiwa na wengine walio katika hamaki.

Kwanza niweke wazi mimi si msomi wa uogeleaji/diving bali nimezaliwa na kukulia katika familia ya wavuvi kando ya ziwa Victoria. Hivyo ajari za majini I am used to it several time.

Kuna aina mbili ya ajari za vyombo vya usafiri majini. Aina ya kwanza ni kile tunachoita kuzama bila kupinduka na aina ya pili ni kupinduka na kuzama. Kuzama bila kupinduka mara nyingi inatokea itilafu ya ndani au nje inayosababisha chombo kizame pole pole inaweza kuchukua nusu saa au masaa chombo kikizama. Katika aina hii ya ajari mara nyingi maafa huwa madogo kwani ni rahisi abiria kuwa organized kugawana maboya na vifaa mbali mbali vya uokoaji kwa utaratibu bila paniki kubwa..

Aina ya pili hii ya ajari chombo hupata tatizo la ghafla mara nyngi huwa upepo/mawimbi au kugonga mwamba na chombo kupinduka ghafla aiana hii ni mbaya sana kwani abiria hawapati muda wa kuchukua maboya au kujioganaizi itifaki ya kujiokoa. Kwa aina hii kila mtu hujiokoa kwa hamaki na taharuki yake.

Mv Nyerere amepata ajari kwa aina hii ya pili, kwa maana kuwa ilipinduka na kuzama ghafla kwa sabababu amabayo haijathibitishwa kitaalamu.

NINI HUTOKEA MELI /BOAT/MTUMBWI UKIPINDUKA MAJINI.

Chombo kikipinduka majini watu hutaaharuki sana wote hijikuta majini dani ya dakika moja hapo hakuna tena habari ya kutafuta boya kinachotokea usiombe kabisa kwani huwa vulumai kubwa ni kila mtu humshikilia mwenzie asizame huu ni wakati ambapo adui wa maisha yako ni mwanadamu mwenzio ndo wakati mme humpiga mke teke asimshike mguu wasizame wote, pale mme anajua kuogelea na mke hajui..

Hapa mtu humuona kila aliyekaribu nae ndiye boya/nguzo yake anakukamata kwa nguvu ili asizame. Hata kama unajua kuogelea ukishikwa na watu wanne moja kashika mguu mwingine kashia shati mwingine kashika mkono ni lazima utakufa kwa maji. Mtu akikushika uamini kwamba wewe ndiye mwokozi wake akikuachia tu atakufa hata umpige vipi hakuachii lazima ufe nae.

Tuliokulia kando ya ziwa hasa kushiriki kazi za uvuvi tulifundishwa mtumbi ukizama rukia mbali na wenzako kwani wakichoka tu kuogelea lazima ukushikile mfe wote.
 
Issue siyo kuogelea ,kujua kupiga mbizi kujinasua kutoka kina cha maji baada meli kupinduka juu chini.
 
Huu ni ukweli mtupu , na bila kusahau kuwa kilikuwa na mizigo mizito ya vyakula na magari yaliyopakiwa humo. Na yote haya hugeuka kuwa silaha dhidi ya binaadamu, kwa kugongwa nazo , hapo lazima upoteze fahamu. Ukiongezea na rundo la watu ktk eneo dogo. Huku mmefunikwa na chombo chenyewe!! .

Laiti ingezama kwa kutoboka wengi wangelipona. Kwani wangelijiorganise
 
Vivuko vyote viwe na "life rings" za kutosha na maboya mengine ambayo namba yake inalingana na namba ya abiria na wahudumu mpaka nahodha.

KIla sehemu yenye kivuko iwe na boti ndogo ambazo zina waokoaji wa dharura na wameajiriwa kwa kazi hiyo.

Pia kila boti iwe na vifaa vyote muhimu maboya, matairi, na kila aina ya kifaa cha uokoaji.

Vijana wa ukokoaji wawe wameingizwa kabisa kwenye payroll ya idara ya maafa kila sehemu yenye kivuko.

KIla sehemu ya kivuko pawe na utaratibu wa kuchuja abiria kwa kuweka uzio maalum au "barriers" ambapo mkataji tiketi anaambiwa kwamba namba imetosha na sehemu ya kupita kwenda ndani ya kivuko inafungwa.

Kwa mfano kwenye MV Nyerere namba ya tiketi ikifiikia 101 ambayo ndo namba ya abiria wanaoruhusiwa kuingia kwenye ivuko basi inapigwa stop, na abiria wengine wanangoja kivuko kiende na kirudi.

Serikal iijaribu kuwekeza zaidi kwenye sekta hii ya vivuko kwani vikiwa zaidi ya kimoja, vitasaidia suala la usafiri na pia vivuko hivi vitaiingizia mapato serikali yenyewe.

Mwisho, serikali iruhusu watu binafsi waingize vivuko vyao na wafanye biashara hii badala ya kutegemea vuvuko vyake ambayo inashindwa kuvisimamia kupitia wasimamizi wake.
 
Mimi kinachonishangaza inakuwaje umbali wa mita zisizozidi mia wafe watu wengi kiasi hicho
 
Haki ya Mungu kunawatu mnahitaji toba. Watu mliowadhihaki waliokufa maji huko Ukara eti wameshindwaje kuogelea mita 50 tu. hamjui nini maana ya chombo cha majini kupinduka majini, hili ni tukio la dakika moja kila mtu yuko majini kila mtu anataka kupona kila mtu anamshikilia mwenzie kama ndiye boya lake bro usiombe. Hapo kupona ni bahati tu si suala la kujua kuogela ama lah. Watu wengi hufa kwa sababu ya kunganiwa na wengine walio katika hamaki.

Kwanza niweke wazi mimi si msomi wa uogeleaji/diving bali nimezaliwa na kukulia katika familia ya wavuvi kando ya ziwa Victoria. Hivyo ajari za majini I am used to it several time.

Kuna aina mbili ya ajari za vyombo vya usafiri majini. Aina ya kwanza ni kile tunachoita kuzama bila kupinduka na aina ya pili ni kupinduka na kuzama. Kuzama bila kupinduka mara nyingi inatokea itilafu ya ndani au nje inayosababisha chombo kizame pole pole inaweza kuchukua nusu saa au masaa chombo kikizama. Katika aina hii ya ajari mara nyingi maafa huwa madogo kwani ni rahisi abiria kuwa organized kugawana maboya na vifaa mbali mbali vya uokoaji kwa utaratibu bila paniki kubwa..

Aina ya pili hii ya ajari chombo hupata tatizo la ghafla mara nyngi huwa upepo/mawimbi au kugonga mwamba na chombo kupinduka ghafla aiana hii ni mbaya sana kwani abiria hawapati muda wa kuchukua maboya au kujioganaizi itifaki ya kujiokoa. Kwa aina hii kila mtu hujiokoa kwa hamaki na taharuki yake.

Mv Nyerere amepata ajari kwa aina hii ya pili, kwa maana kuwa ilipinduka na kuzama ghafla kwa sabababu amabayo haijathibitishwa kitaalamu.

NINI HUTOKEA MELI /BOAT/MTUMBWI UKIPINDUKA MAJINI.

Chombo kikipinduka majini watu hutaaharuki sana wote hijikuta majini dani ya dakika moja hapo hakuna tena habari ya kutafuta boya kinachotokea usiombe kabisa kwani huwa vulumai kubwa ni kila mtu humshikilia mwenzie asizame huu ni wakati ambapo adui wa maisha yako ni mwanadamu mwenzio ndo wakati mme humpiga mke teke asimshike mguu wasizame wote, pale mme anajua kuogelea na mke hajui..

Hapa mtu humuona kila aliyekaribu nae ndiye boya/nguzo yake anakukamata kwa nguvu ili asizame. Hata kama unajua kuogelea ukishikwa na watu wanne moja kashika mguu mwingine kashia shati mwingine kashika mkono ni lazima utakufa kwa maji. Mtu akikushika uamini kwamba wewe ndiye mwokozi wake akikuachia tu atakufa hata umpige vipi hakuachii lazima ufe nae.

Tuliokulia kando ya ziwa hasa kushiriki kazi za uvuvi tulifundishwa mtumbi ukizama rukia mbali na wenzako kwani wakichoka tu kuogelea lazima ukushikile mfe wote.
Ulishatumbukiaga na chombo ukapata experience yake.
 
Ni kweli mkuu aisee yaani unajiona unakufa hivihivi, mi naona abiria wapewe life jackets,maboya pale tu wanapoingia kivukoni na wakishavuka wayarudishe kwa wasimamizi watakaokuwepo, siyo maboya yanafungiwa hata dharula ikitokea mpk hiyo store ifunguliwe dah. Rest Easy ndugu zetu
 
Back
Top Bottom