Kuoa/kuolewa kunabadilisha uhusiano wako na wazazi wako

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Wasaalam ndugu zangu,

Hope its been a wonderful sunday to you.

I passed somewhere in the internet and found an impressive piece of work; which i think might be helpful to some of us. particularly those who are married and about to be married.

Point to remember: The article is purely religious (Christian to be precise) but it has some intrinsic values which are likely to shed light upon people of all religions.

Its an Episode from One of Mwalimu Mwakasege's Seminars Called MAMBO YA MSINGI KABLA YA NDOA.

JAMBO LA KWANZA

Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano wako na wazazi wako.
Mwanzo.2:24 anasema,? Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja?. Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema,? Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie?.

Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako.
Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako.

Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako. Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo? Ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako kama umeoa, na ni mume wako kama umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako. Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa.

Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema,?Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie?. Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia,? Your priorities must change? Lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao. Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu.

Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako. Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana. Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani.

Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata kama atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni,? Anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; Kwanini? Kwasababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake. Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi.

Unaweza sasa ukaelewa kwanini watu wengine ikifika siku ile ya ? Send off?, yaani ya kum? Send? Msichana ? off? Asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwasababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine. Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.

Thats its folks,
Have a wonderful and please lets avoid religious feuds; we are talking about marriage here.

CC:
, Kaboom PAUL sergio de souz BADILI TABIA MK254 The Boss King'asti

Hicho kipengele cha kutamani wengi kinawashinda..Nadhani mapenzi mengi yanaanza na kutamani...

Btw mi sipo vizuri sana kwenye Bible..Kwa mujibu wa Biblia,Uhusiano wa mtu na familia yake unatakiwa uwaje baada ya kuoa/kuolewa??
 
Jali wazazi, wapende na uwaheshimu.
Its one of God's commandment.

But ukishaoa/olewa the mke wako au mume inabidi aheshimiwe sana tu.
Tena wazazi, ndugu na marafiki ni lazima walijue hilo.
Thats why kuna sehemu inasema NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
 
Useful word.... Kulielewa na kulifuata lazma uwe na hofu ya Mungu ndani yako otherwise utaishia kusikia "nyoooo nani kama mama, mume hawezi kuwa first priority over my mom"
Hiyo ndo maana haswa ya kuachana na wazazi kuambanata na mme/mke kamata umeoa au kaolewa na bado unahisi unahitaji kuambanata na wazazi heri ukaishi nao tu nyumbani
 
Ok nimekusoma..Ila kikubwa ni kupata mke/mme mnayeelewana..Hivi vitu sidhani kama vina kanuni ya moja kwa moja,coz watu tunatofautiana

kwa mfano
Kuna watu wakiwa kwenye ndoa hata ikipita miaka kadhaa hawajaonana na ndugu zao kwao ni sawa tu,Ila wengine hawawezi kupitisha mwaka bila kuwaona wazazi wao..So mkikutana wote ambao mko kwenye kundi moja sio shida sana

Tabu inakuja kwa wanandoa ambao interest zao zinatofautiana na kila mmja kujiona yeye yuko sahihi zaidi..Huyu anapenda hiki yule hapendi na anaona si sahihi kufanya hivyo..Hapo migongano ya mara kwa mara lazima itokee
 
Useful word.... Kulielewa na kulifuata lazma uwe na hofu ya Mungu ndani yako otherwise utaishia kusikia "nyoooo nani kama mama, mume hawezi kuwa first priority over my mom"
Hiyo ndo maana haswa ya kuachana na wazazi kuambanata na mme/mke kamata umeoa au kaolewa na bado unahisi unahitaji kuambanata na wazazi heri ukaishi nao tu nyumbani

Wewe umeliewa neno vizuri,....
Hongera kwa hilo.
 
Sijui kama ndio kunabadilisha uhusiano na wazazi wako....... ila unapooa/olewa vipaumbele??? Hubadilika.

Jambo ulilokuwa ukijadiki na wazazi au.kujiamulia mwenyewe inabidi ushauriane na mwenzio.

Familia yako inakuwa ya kwanza.

Ngoja nitulie niusome tena huu uzi kwa makini.

Na huu uzi unawahusu wale walioko kwenye ndoa ila maamuzi yanafanywa na wazazi wao
 
Wise words. Ila uhusiano na wazazi sioni kama utabadilika nikioa. If I can click with her, they will click with her and vice versa as well. Vivyo hivyo kwa upande wa kwao na mimi. Itakuwa tu uhusiano wetu na wazazi, badala ya uhusiano wangu/wake na mzazi/wazazi.

Btw, jana nimeongea na Mama mkwe kwa kifupi tu, na tume-establish good friendship. So I have a clue of what I'm talking about.
 
MALCOM LUMUMBA this's a wonderful marriage lesson!

With my little bible knowledge, nilikuwa najua ile part ya mwanaume pekee kwamba ataacha wazazi na kuambatana na mkewe, sikujua mwanamke has her part as well.
Na kama alivosema Evelyn hapo juu, it has to be more spiritual au kuwa na hofu ya Mungu (and that's where the catch is) cos wengi tunashindwa na tukifanya vinginevyo ndio mwanzo wa matatizo yote.
 
Last edited by a moderator:
...Btw mi sipo vizuri sana kwenye Bible..Kwa mujibu wa Biblia,Uhusiano wa mtu na familia yake unatakiwa uwaje baada ya kuoa/kuolewa??

Jali wazazi, wapende na uwaheshimu.
Its one of God's commandment..
But ukishaoa/olewa the mke wako au mume inabidi aheshimiwe sana tu.
Tena wazazi, ndugu na marafiki ni lazima walijue hilo.
Thats why kuna sehemu inasema NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.

Kuongezea kwenye swali la Kaboom kuhusu mahusiano na familia baada ya ndoa
MALCOM allow me to get a little out of the bible...

Ki binadamu naona ni vyema familia kuwapa nafasi ya kutosha wana ndoa, mahusiano na familia yawepo lakini yasichukue nafasi kubwa sana na kusababisha matatizo kwa wenye ndoa.
 
Miss u doll. Exactly kuwepo na kadistace kidogo. Me tangu nimezaliwa hadi now nazeeka naona mambo mengi baba na mama wanashauriana wenyewe na kufanya maamuzi yao binafsi. Sio mbaya kuomba ushauri kwa wazee but Iwe pale necessary. Isiwe kila kakitokea kakitu kidogo mnakimbilia kwa wazee. Kuna watu wameoana lakini wazazi wao ndo wanaowafanyia maamuzi, lazima itakuja kuleta matatizo kwa mwanandoa mmoja na hao wazee wanaowafanyia maamuzi au kama sio kila mwanandoa atataka mfuate ushauri wa wazee wake. Mkiona hamjagrow up enough kufanya maamuzi ya familia yenu, basi msioane tu.
 
Missed you too!,.....you're right on point!
 
Kuongezea kwenye swali la Kaboom kuhusu mahusiano na familia baada ya ndoa
MALCOM allow me to get a little out of the bible...

Ki binadamu naona ni vyema familia kuwapa nafasi ya kutosha wana ndoa, mahusiano na familia yawepo lakini yasichukue nafasi kubwa sana na kusababisha matatizo kwa wenye ndoa.

Wazazi hawatakiwi waingilie maisha ya ndoa ya watoto wao.
Mapenzi ni ya watu wawili na Mungu. (FULL STOP).
Wabaki tu kuwa washauri, tena only in sensitive matters.

Sasa unakuta mtoto wa kiume anamwambia mama mambo yake yote ya mke wake,..
Au binti anamwaga mambo yake yote kwa mama yake yaani ni shida tupu.
 
Asante kwa kuniita huku bwana MALCOM LUMUMBA, inafaa ifahamike ni muhimu kwa mwanaume kumtafuta mke ambaye mnaendana naye kwa mambo mengi na sio mapenzi tu. Mke ambaye atakua rafiki wako na utapendezwa kukaa naye muda mwingi. Mke ambaye kila ukitoka kazini unataka uwahi ili umkute nyumbani maana unahisi raha kuwa naye, mnaweza ongea mambo ya kawaida na kwa furaha kama marafiki.

Ikifikia hapo, utakuta kujitenga na wazazi wako pamoja na hata wale marafiki wako wa bar itatendeka yenyewe tu (automatically). Maana hapa kuna rafiki wako mpya mnayeendana katika mambo mengi kama vile uraibu na zaidi unanufaika na mapenzi pia.
cc: kui
 
MK254 true, na pia kuendana mke na mume kunapunguza matatizo mengi ktk ndoa, it's easy ku solve issues na mtu mnayeendana vizuri
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom