Kuoa au kuolewa mapema kwa kijana

baba stive

Member
Mar 10, 2016
11
10
KUOA AU KUTOKUOA KWA KIJANA


Kumekuwa Na mvutano mkubwa wa kimawazo kuhusu suala zima la kuoa kwa vijana hasa vijana wasomi Na vijana wanaoishi mjini Na hii imepelekea vijana wengi waliooa Na miaka 20-30 kuonekana kama watu waliokosea Raman ya maisha. Lakini katika Tamaduni zetu za kiafrika kijana wa kiume alikua anaoa pale tu alipobalehe Na kumaliza JANDO kati ya miaka 15-20 huyo aliweza kupewa mke Na kuoa Na binti pia pale alipoota matiti tu Na kupata Elimu ya familia aliolewa Na wengi waliolewa wakiwa Na umri wa miaka 12-15 Na binti alikua Na uwezo wa kuishi Na kutunza familia kwa kiwango kikubwa sana Na suala la kuoa Na kuoana lilikua lina heshimika Na linamvuto mkubwa kwa jamii na lilipendwa sana tofauti na sada

KUOANA KWA SASA
Katika dunia yetu ya Leo ukimwambia kijana wa kiume au kike kuhusu kuolewa anaweza hata kukupiga vibao Ni vijana wachache sana ambao wapo tayari kuoa wakiwa Na umri mdogo Na wengi wamekua wakidai kuwa wanajipanga kwanza ndio waingie kwene ndoa hivi unaweza jiuliza kwanini kila mtu anasema anajipanga Na wengine wanaseme hawapo tayari kuingia kwene ndoa kwa sababu wanaume au wanawake hawaaminiki yawezekana wapo sahihi lakini tujiulize nikweli kwamba kuoa au kuolewa mapema ni kikwazo cha kuendelea kimaisha? Na kipi kinasababisha ndoa zipoteze ubora? na je nikweli kuogopa kuoa ndio suruhisho la tabu hizo?

Kuhusu kuoana kuwa ni kikwazo cha maendeleo suala hili linategemea aina ya mtu ulienae katika ndoa ukipata mtu ambae yupo tayari kutafuta Na wewe na kukuandaa kuelekea kwene mafanikio sio siri utamcheka ambae anatafuta peke yake Na kusema bado yupo yupo kwanza lakini ukimpata MTU anaekuja kula vyako lazima atakukimbia Na wanaokuzunguka hawataoa mapema tena kikubwa hapa upate mtu sahihi kwa sababu unaweza tafuta Na usipate hizo pesa.

Natambua pesa imekua mbele kwene mahusiano ya siku hizi kijana usipokua Na kitu utawaita mashemeji mabinti wote wazuri tatizo hapa tumegeuza ndoa Na miili yetu kama kitega uchumi (Wanajiuza) kwakua ni mzuri aolewe Na mme mwenepesa lakini hawa ndio wakwanza kukimbia ndoa kwa sababu wanaume wao wanathamini pesa kuliko uzuri wake Na anaamini atapata mwingine mzuri Na mbichi kigezo cha pesa kimewafanya vijana wengi kuogopa kuoa mapema Na hiki kimekua kikiwatishia amani vijana kwa kuogopa kuachwa au kuchukuliwa wake zao

Lakini pia mmomonyoko wa maadili unachangia watu kujiingiza kwa ndoa Leo hii kijana wa miaka 18 anawafahamu wanawake 20 Na binti anawafahamu wanaume 20 Na mapenzi yote hayo yamejikita kwene tendo la ndoa unafikili hadi hapo kuna uthamani wa ndoa wakati ukitaka unapata? Siwacheki wanaosema bado wanatafuta huku wakichovyachovya Na mabinti wanaosema wanachuna mabuzi huku wakitumiwa hawa kamwe hawawezi tamani kuoa wala kuolewa na hawajui kwene ndoa anatakiwa kufanya nini wao wanajua ni kulala tu kumbe hiyo ni asilimia 1 ya ndoa kuna zaid ya hiyo hvyo lazima ndoa zivunjike na wengine waogope kuingia kwa kuwaangalia walioharibikiwa hapo kujana haoi

Kikubwa tulejee maandiko ya vitabu Vya dini zetu tusome Na tutambue Kuwait ndoa inatola kwa mungu ukimwomba mungu Lazima utapata mtu sahihi Na usikurupuke kuingia kwa ndoa bila kumfahamu ulienae lakini ukipata mtu sahihi hakuna haja ya kujipanga mtashirikiana kuweka mambo sawa.

by
MELKIZEDECK BASHINGWA
MTANZANIA
18/03/2016
 
Kisingizio cha hadi maisha yawe mazuri ndiyo nioe ukichunguza kwa undani wake utagundua ni uwoga tu wa maisha kwani kuna Wazee wamekuja fanikiwa kwenye maisha wakiwa kwenye 50s na si kwamba walikuwa hawapambani, No! ila ndiyo wakati waliokuwa wamepangiwa huo...Sasa na yeye angesema sioi mpaka life linyooke ingekuwaje? Cha msingi ni kujua kuna vigezo pindi unapotafuta hawara na kuna vigezo pindi unapotafuta mke..
 
Pateni Mawaidha mujaarab
 

Attachments

  • Mawaidha... (1).mp4
    3.1 MB · Views: 69
  • Mawaidha... (1).mp4
    3.1 MB · Views: 46
Sielewiiiiiiii huu uzi.
Kama uki jitahidi kusoma vitabu vyamungu kuliko vya mzungu uta uelewa tuuu.
Kitu kinacho itwa uzinzi,uasherati,nk vime kemewa sana kwenye vitabu vya mungu.
Nuhuwezi kuniambia hutaowa &huta olewa halafu huta fanya sex.
Uta kuwa muongo.
 
Bahati mbaya siku hizi ndoa zinazoharibika ni za vijana kuanzia miaka 25 mpaka 35 sijui kwa nini.
 
Ningepewa nafasi ya kutoa ushauri, kwa karne hii kuoa ukiwa 20-28 ni mapema sana. Japo najua kuna sababu chanya zinafanya watu waoe katika umri huo, lakini bado kuna sababu ya kusubiri hadi 28-35, hasa kwa kizazi na karne hii
 
Ngoja niwashauri vijana . .

1. Usio kwa shinikizo la filia ,rafiki au Kanisa/Msikiti.
2.Usio mwanamke Mzuri umbo na sura angalia tabia .
3.Usio kwa kutegemea kuijenga Familia yako Financially ukisaidia na mwanamke ,ingiaa kwnye Ndoa ukiwa unajua ww ndio kichwa cha familia ,Ujinga wa kudanganyana Mtasukuma familia pamoja ,ww kama kijana Acha . Ikija kutikea mnashirikiana itokew tu lakini sio Rasmi.


Mambo machache matatu yazingatia .
 
Ningepewa nafasi ya kutoa ushauri, kwa karne hii kuoa ukiwa 20-28 ni mapema sana. Japo najua kuna sababu chanya zinafanya watu waoe katika umri huo, lakini bado kuna sababu ya kusubiri hadi 28-35, hasa kwa kizazi na karne hii

hebu twambie kuna faida gan kusubili 28-30s kwa life span ya mtanzania 45 huoni ni kuandaa mayatima bure kwa taifa letu
 
Kuoa kupo na hakuna reason ya kuharakisha bcs ukijihis kuingia utaingia tu ndoa hailazimishwi but ni basic need at the right time.
So make sure unaweka malengo yako ya maisha mbele then hayo ya kuoa tatafatia.kuna jamaa kaoa lakin anakuja juomba 5000.heshima ya mwanaume ni kuweza kumudu family bila kutegemea.
Unashaur wakaoe rafiki zang wote waliooa nawadai saiv.usivae viatu ambavyo havikutosh subir miguu ikue.
 
Natamani ningeoa na miaka 18...

Kuoa mapema kuna manufaa sana ukipata mtu ambaye sio pasua kichwa.
 
Kuoa kupo na hakuna reason ya kuharakisha bcs ukijihis kuingia utaingia tu ndoa hailazimishwi but ni basic need at the right time.
So make sure unaweka malengo yako ya maisha mbele then hayo ya kuoa tatafatia.kuna jamaa kaoa lakin anakuja juomba 5000.heshima ya mwanaume ni kuweza kumudu family bila kutegemea.
Unashaur wakaoe rafiki zang wote waliooa nawadai saiv.usivae viatu ambavyo havikutosh subir miguu ikue.
Kujipanga muhimu.
 
Ngoja niwashauri vijana . .

1. Usio kwa shinikizo la filia ,rafiki au Kanisa/Msikiti.
2.Usio mwanamke Mzuri umbo na sura angalia tabia .
3.Usio kwa kutegemea kuijenga Familia yako Financially ukisaidia na mwanamke ,ingiaa kwnye Ndoa ukiwa unajua ww ndio kichwa cha familia ,Ujinga wa kudanganyana Mtasukuma familia pamoja ,ww kama kijana Acha . Ikija kutikea mnashirikiana itokew tu lakini sio Rasmi.


Mambo machache matatu yazingatia .
Umenena,wapiii wapenda mteremko waje waone hapa
 
Back
Top Bottom