Kunywa maji baada ya kusikia kiu ni kujiandalia kifo cha mapema na chenye maumivu sana: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunywa maji baada ya kusikia kiu ni kujiandalia kifo cha mapema na chenye maumivu sana:

Discussion in 'JF Doctor' started by Fadhili Paulo, Jan 13, 2012.

 1. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135


  KUNYWA MAJI BAADA YA KUSIKIA KIU NI KUJIANDALIA KIFO CHA MAPEMA NA CHENYE MAUMIVU SANA:


  Muda gani unamwagilia maji bustani yako? Kwa hakika ni asubuhi au jioni na si saa nane mchana wakati jua tayari likisha kuwa kali – la sivyo mimea itakufa. Pia ukitembea umbali mrefu na gari na ghafla maji yakaisha katika injini haushuki tu na kuongeza mengine papo kwa papo, utasubiri injini ipowe ndipo uongeze mengine – la sivyo injini ya gari (ambayo ni chuma) itakufa.

  Hivyo binadamu kuendelea kusubiri kiu au mdomo ukauke ndipo anywe maji, huwa anajiandalia kifo mwenyewe cha mapema na chenye maumivu sana. '‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. fereydoon Batmanghelidj''.

  Hivyo magonjwa kama maumivu, pumu, aleji/mzio, shinikizo la damu, kisukari, utipwatipwa, kansa, kuzeeka mapema na mengine mengi; yote haya ni ishara tu za mwili kutuambia kuwa tunapungukiwa maji, yaani tunaumwa kiu!!.

  Kiu hutibika kwa maji tena bila gharama yeyote!.

  Magonjwa ni moja ya maadui wetu watatu tuliotangaza kuendelea kupigana naye mpaka tumshinde mara baada ya kupata uhuru kutoka kwa wakoloni mwaka 1961. Ni zaidi ya nusu karne sasa bado tungali na adui huyu anayezidi kutia hofu mamilioni ya watu.

  Maajabuyamaji.com inaitaja sababu ya maradhi kuendelea kututesa kuwa ni mazoea yetu kusubiri kiu ndipo tunywe maji. Inajulikana wazi kuwa maji ni uhai. maajabuyamaji.com inafafanua sababu za maji kuitwa ni uhai, inaeleza madhara yatokeayo mwilini inapotokea tunaipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).


  Kumbe kwa kutumia maji tu yale tunayoyanywa kila siku tunaweza kujikinga na kujitibu magonjwa mengi bila idadi na hatimaye kumshinda adui maradhi na hivyo kujipunguzia gharama sisi wenyewe na serikali kwa ujumla.


  maajabuyamaji.com inafundisha pamoja na mambo mengine: kazi za maji mwilini mpaka kuitwa ni uhai, namna mpya ya kuitambua kiu, na namna ya kunywa maji ili kujikinga na kujitibu na maradhi mbalimbali.


  Hakuna anayependa kuugua, awe daktari, askari, kiongozi wa serikali au wa dini, mwandishi au mtangazaji, mfanyakazi au mkulima. Tovuti yako ya maajabuyamaji.com inapenda kushirikisha vyombo vya habari na wadau wengine katika kuelimisha hili, moja ya kazi mhimu za chombo cha habari ni kuelimisha jamii kwa manufaa ya jumla ya jamii nzima, kwa sababu hii tunakitoa bure kitabu cha kieletroniki (e-book) kinachoeleza kwanini kusubiri kiu ndipo tunywe maji ni kujiandalia kifo mapema na chenye maumivu sana. Kitumieni hicho kama mwongozo (user manual) wenu.


  Tuendelee kusherehekea miaka 50 ya uhuru tukiwa tayari na silaha ya kumshinda adui maradhi kwa kutumia maji tu.

  attached: maajabu ya maji e-book, download it for free
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Na ni nini/yapi ni madhara ya kunywa au kuwa na maji mengi mwilini? Maana kuna msemo kuwa 'too much of everything is harmful'.
   
 3. T

  TUMY JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani kwa ujumbe mwanana na maridhawa.:poa
   
 4. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  tafiti nyingine zinatia mashaka sana! unataka kusema kuwa wanamichezo wote maisha yao yanakuwa mafupi maana ndo wanaongoza kwa kunywa maji wanaposhikwa na kiu.Kwa mfano pembeni kuzunguka viwanja vya football utakuta maji kuna chupa za maji zimejaa au wale wanaokimbia mbio ndefu nao huwa wanakunywa sana maji huku wakiendelea kukimbia.Mi nadhani hii isue uliyozungumzia iko too theoritical.Hata wanyama pia hunywa maji pale tu wanaposhikwa na kiu sembuse binadamu!

  Mi nawashauri watu wasi-complicate maisha wakati sio magumu kihivyo.Ni muhimu sana kunywa maji pale unaposikia kiu.PLEASE OBEY YOUR THIRSTY!
   
 5. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,799
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nafuu Mkuu na wewe umeliona hilo. Ni kweli tunafaham maji ni muhimu lakini huyu mwenzetu amepitiliza kuyasifia. Hivi utakula chakula wakati hauhitaji kwa muda huo? Mwili una sencor zake kama alivyosema, unapohitaji kitu flan unapata signs then unatekeleza. Hivi ni sawa kuvaa koti wakati hausikii baridi na kuna joto? Na je utatembea kifua wazi wakati wa baridi kali? Hizi tafiti zisizo rasmi zitatupeleka kubaya.
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tafiti zingine Mungu anajua
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  eti enheee na hizi NGOs zimezidi kila mtu mtaalam wa afya...
   
 8. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Mkuu, swali nzuri, nimeattach kitabu bure chenye kurasa 100, kidownload bure na ukisome taratibu kurasa moja mpaka nyingine utakutana na jibu la swali lako, la sivyo utanijulisha tena.
   
 9. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Mtu akiwa na M.D kwa hakika ni mtaalamu wa afya au siyo mkuu?: WaterCure | About Dr. B
   
 10. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  aah! kazi iko hapo.
   
 11. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  SaidAlly, una mbwa au paka hapo kwako?, kama ndiyo fanya hivi; kila ikifika saa saba mchana mpatie chakula kila siku iwe ni saa saba tu bila kuchelewa na pembeni yake mwekee maji muda wote. fanya hivyo kama mwezi mmoja halafu mchunguze paka au mbwa huyo utaona ikifika saa sita na nusu anaenda kunywa maji yaliyo karibu kwa kuwa anajuwa saa saba utampatia chakula. Tofauti na hapo utabisha kwa kuwa inawezekana hakuna saa maalumu unawapatia chakula na pengine hata maji huwawekei karibu.
   
 12. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  myhem, hongera kwa picha yako, unaonekana kufanana na ferguson kocha wa man u. Madaktari wanashauri mtu akitoka kukimbia mwendo mrefu atakaposimama asipewe maji papo hata kama anasikia kiu kama unavyoona wanafanya wachezaji hao unaowasema, ni hatari kufanya jambo hilo. pia usiende kuogelea mara baada tu ya kutoka kula. vipi umepakuwa kitabu?
   
 13. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Hii ndo moja ya changamoto za watafiti. Kutumia species kama panya kutest hypothesis na kisha kugeneralise results hadi kwa wanadamu.

  Hii conventional scientific approach inapaswa ibadilike,la sivyo matokeo ya tafiti yatakua yanachukuliwa kama mzaha kwa binadamu.
   
 14. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #14
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Haya nakubaliana nawe.
   
 15. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #15
  Jan 14, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  wake up tiizii !!!!!!!!
   
 16. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  afadhali umeliona hilo mapema mkuu. wengine na sisi tumezoea kupokea maoni bila kuyachambua
   
 17. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tafiti zingine ndio hizi za kina Ndondi mtu hata lab wala magnifying lens hana anatisha watu utafikiri amefanya a tangible research! Tangu enzi za mbabu zetu watu mashambani kote huwa wanakunywa maji baada ya kushikwa na kiu miaka nenda rudi hao ndio wanaishi miaka hadi 100. Please usilinganishe wanyama na mimea! Ni vitu 2 tofauti
   
 18. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #18
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Unajuwa kuwa bila maji hauwezi kuishi? Unajuwa kuwa kila baada ya masaa 24 unapoteza glasi 4 za maji kwa kupumua tu? Unajuwa kuwa asilimia 94 za damu yako, asilimia 85 za ubongo wako ni maji na asilimia 90 za mtoto anayezaliwa ni maji?. Basi ili uelewe ni kuwa zaidi ya nchi nzima ipo katika mgawo wa umeme kwa zaidi ya mwaka sasa sababu kina cha maji huko katika mabwawa ya kuzarishia umeme kimepunguwa.
  • Bila maji hakuna kinachoishi. Wakati wowote unapopungukiwa maji, seli zako hufa.
  • Panapotokea upungufu wa maji, kitu kimoja lazima kipotee, baadhi ya kazi za seli hufa.
  • Maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu, maji ndiyo hela ya mwili, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

  jisomee kazi zingine 41 za maji mwilini: baadhi ya sababu kwanini unahitaji maji kila siku | maajabu ya maji
   
 19. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  lab na magnifying lens ndiyo vitu gani hivyo mkuu?, tatizo lako unajuwa unabishana na fadhili paulo. mkuu hii ni elimu tu, siyo kazi yangu kukuaminisha kuwa maji ni jibu kwa kila ugonjwa kwa binadamu, kunywa kwanza kama nilivyoshauri mimi kuwa usisubiri kiu ukiona ni kweli urudi kutoa ushuhuda hapa, bali usitegemee mimi naweza kuamini tofauti na hivi. http://maajabuyamaji.com/
   
 20. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  heeee!!!!
  Mambo mengine bana..
  Im outa of here.
   
Loading...