Kunyonyesha mtoto

ngoja niihifadhi, itanifaa nikianza kunyonyesha. senkyu lizzy.
 
miezi 6 maziwa ya mama tu...hayatoshi!!!

yanatosha sana, mie dadangu wanae wote wanne wamenyonya 6 months bila kulishwa chakula kingine na walikuwa na afya na uzito mzuri tu
 
Yanatosha kwa wanaokaa nyumbani..
Lakini kwa wafanyakazi wengi hiyo ni ngumu...
Maana production ya maziwa inategemea pia na frequency ya unyonyeshaji...

Labda ndio maana nchi nyingi za ulimwengu wa kwanza likizo ya uzazi ni miezi 6...
(japo wanawake huko hawapendi kunyonyesha muda mrefu; na si issue kwao maana maziwa ya kopo kwa ni safe as maji yao ni safe, na vyakula vinapimwa ubora...si huku mchina; issue ya maziwa ya kopo kuwa si mazuri inalennga nchi masikini sababu ya hygiene na umasikini)

yanatosha sana, mie dadangu wanae wote wanne wamenyonya 6 months bila kulishwa chakula kingine na walikuwa na afya na uzito mzuri tu
 
yanatosha sana, mie dadangu wanae wote wanne wamenyonya 6 months bila kulishwa chakula kingine na walikuwa na afya na uzito mzuri tu

kuna wengine wakifika miezi 3 au4 huwa wanalia sana kama anapewa maziwa pekeee ndo mana naonaga wengi wanaanzishiwa uji mwepesi uliochujwa
 
Mimi kwa kweli mke wangu nampa bonasi ya 30,000/= kila mwezi kwa kumngonyesha mwanangu. Pia kifurushi cha muda wa maongezi cha cha 2,000.00 tigo kila wiki kama motisha amnyonyeshe mwanangu. Na bahati nzuri mwanangu anafahamu kama anaponyonya kua motisha kwa hiyo ye ni kunyonya mwanzo mwisho. Mama yake naye kwa kutambua hilo anajitabidi kula vizuri kwa ajili yake na mwanetu.
 

Nimewachisha Miaka miwili lakini ilikua shida duh, wanavuta nyonyo Mpaka unasikia kama mtu anakomba sufuria, mie nilikua sikamui nikawachiaa wananyonya asubuhi na nivile wawili wana maliza Saa 6 wanaletwa kazini kunyonya Mimi Saa 9 nakua home....
 
Last edited by a moderator:

Kwa kuongezea tuu kunyonyesha kunasaidia pia kupunguza uzito kwa Mama, kupunguza risks za kupata Cancer na magonjwa ya Moyo . Thanks!
 
bora uwakumbushe maana siku hizi wanajifanya usasa umewatawala,hawanyonyeshi tena,wanaogopa ziwa kulala wakati liliwekwa kwa matumizi ya mtoto na sio baba(baba wanadandia tu chakula cha watoto)

Alafu wanakuaga wanaboa ukiwaambia wanajidai vichwa vigumu eti dokta kasema tuanze kumnywesha uji apate nguvu, uji mtoto wa miezi minne akili ya wapi hiyo 😬😐😐😐😡😡😡😡😡
 

sio mama wa nyumbani, ni mfanyakazi na alimanage
 
Honestly Mimi nilinyonyesha mpaka mwanangu aliacha mwenyewe. Na nilikuwa nafanya kazi na kwenda shule full time . Nikiwa kazini au shule , huwa napump usiku wake kabla sijalala na kuyaweka kwenye fridge. Asubuhi nikimdrop mwa mwanangu kwa sitter nadrop na maziwa yake niliyokaamua ,ilienda hivi kwa muda . My dear inahitaji moyo, willing na commitment kunyonyesha. Kazini tunawashauri sana sana breastfeeding kwa Mtoto angalau miezi sita ya mwanzo., ili Mtoto asipate na allergies, or maradhi mengineyo kwa kuwa immune system zao haziko strong ,so breastfeeding inawasaidia sana sana watoto wetu ,. Jamani tukishakuwa wamama inabidi tuu tujisahau kuhusu wenyewe na kuwaza benefits za watoto wetu. Sisemi usijutuze hapana , kwa wale mnaohofia miili yetu mbona breastfeeding inasaidia kupunguza ,na hata gym pia mbona ziko za kumwaga tuu ni kuweka muda Wa kwenda huko na kututumka. Inauma , kuna wazazi kibao wanaokuja kazini kwangu nikiwauliza unanyinyesha anasema hapana kisa hataki maziwa yake yaanguke sasa najiuliza walizalia nini kama Bado usichana haujaisha. Au analalamika eti maziwa hayatoshi ,na akipewa suggestion ya food nutrition za kutumia ili apate lishe ya mtoto anakuambia vitamfanya anenepe, kazi Kweli Kweli Mungu atusaidie tuu . Thanks.
 

Kwa ufahamu mdogo nilionao ni kwamba mama hata kama ameathirika ananyonyesha miezi sita ya kwanza ila kwake yeye agizo la kutompa kitu kingine chochote linatakiwa lizingatiwe sana.....mama akizingatia hili huku anaendelea na dawa mtoto anakuwa salama kabisa
 

Hii ni very rare kushauriwa kufanya hivi . kwa maana wengine wanaweza kujisahau kufuata masharti matokeo yake Mtoto ndio anakuwa victim . Kuna dawa/ kinga Yes wamama wanapata ili waweze kuwanyonyesha watoto kwa muda Fulani. Ila inategemea na muathirika yuko katika stage gani, mashambulizi yako too strong or. So kuna precautions za kuchukua pamoja na vipimo zaidi. Ila for sure doctors wengi wanajitahidi sana sana kusave maisha akiwa tumboni asipate maradhi kama Mama, kwa kutumia dawa na masharti ,wengi wao wana succeed hilo lengo kutimia . Thanks.
 

Mmmmh suala la kuvunja masharti ni uzembe wake yeye mama. Ila kama mama ana hali nzuri anashauriwa kunyonyesha. Nimekaa PMTCT kwa miezi miwili na nimeona kabisa wamama wanaonyonyesha na watoto wana afya nzuri kabisa
 
Nauliza tu koh koh koh mtoto anakaaje 6mnths bila kunywa maji? baby wangu nmekaa nae wiki 2 akaanza kutoka mate mazito afu mengi, anasweat sana na lips zake znakauka mi nkahisi ana kiu ikabidi nianze kumpa maji kijiko kidogo 1, mate yakaisha na lipsi hazijakauka tena!!!
 
Mmmmh suala la kuvunja masharti ni uzembe wake yeye mama. Ila kama mama ana hali nzuri anashauriwa kunyonyesha. Nimekaa PMTCT kwa miezi miwili na nimeona kabisa wamama wanaonyonyesha na watoto wana afya nzuri kabisa

Ni Kweli kwa masharti kuzingatiwa, my dear sio Wa Mama wote ni wazembe wengine hujisahau kwa schedules especially nnchi za nnje , na ndio wanaafya Wa hapa tunawaeleza kabisa benefits na risks kama wakifuata masharti na wasipofuata masharti, in that case wengi wao hawataki kuweka Mtoto kwenye risks na kuwa victim so wanaamua kutofanya hivyo . Nnchi nyingi za nnje mtoto huwa anawekwa wa kwanza na sio wa mama . Na ndio maana hata kwenye kujifungua tuko tayari kusave maisha ya mtoto kwanza ya mama ndio yanafuata .Thanks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…