Kunyonyesha mtoto

Kunyonyesha mtoto

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,010
Reaction score
60,472
Nimeona niandike hii makala baada ya kushuhudia watoto kadha wa kadha wakidhoofika kwa kulazimishwa kula vitu ambavyo umri wao hauruhusu. Wako ambao miili yao inakuwa sawasawa au hata zaidi (overweight) ila bado hawaendelei vizuri kwenye mambo mengine mf. Kuwa wazito kutembea, kuongea, kufikiri n.k.

Kabla ya kwenda mbali, tukumbushane kwamba faida za kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita bila kumpa chochote na kuendelea kumyonyesha kidogo kidogo hata baada ya hapo ni nyingi na ni muhimu sana kwa afya ya mtoto. Baadhi ni....
1. Kumsaidia mtoto kuepuka magonjwa, mtoto haugui hovyo.
2. Inampa mtoto nafasi kubwa kuepuka kuwa na mizio (allergies) kuliko anaepewa maziwa.
3. Maziwa ya mama yanaongeza ufahamu wa mtoto.
4.Ukaribu kati ya mama na mtoto unaongezeka na hiyo 'bond' inamsaidia mtoto kukua vizuri kwa furaha.
5. Speed ya ukuaji wa mtoto kiakili, kimwili, kisaikolojia na kihisia inakuwa juu. N.k

PS.
KWA WAMAMA, KUNYONYESHA EXCLUSIVELY KWA MIEZI 6 NI NJIA NZURI SANA YA UZAZI WA MPANGO. Wengine hata period wanasahau kwa zaidi ya mwaka mmoja (hii nimeifaidi..lol)

Tukirudi kwenye mada, wadada/wamama wengine huwa wanawalazimisha watoto kunywa uji/mtori/mziwa ya ng'ombe kwa kutopenda kunyonyesha, kudai hawana maziwa ya kutosha na kuwa busy na kazi kwa wale walioajiriwa ama kujiajiri.
1. Wasiopenda kunyonyesha.
..Huo ni ubinafsi uliotukuka.
Ikiwa hauko tayari kumtimizia mtoto mahitaji yake ya msingi kwanini ubebe mimba?! Kula ujana ukimaliza ndio uzae. Kwanza unataka manyonyo yakae juu juu maisha yako yote yamekuwa mawingu?!-😉
2.Wanaoamini hawana maziwa ya kutosha/mepesi kwasababu mtoto ananyonya non-stop bila kuonyesha dalili ya kushiba Nakushauri KULA VIZURI.

Nna rafiki yangu ana mtoto wa miezi minne tu na ana kilo 5,kadogoooo lakini anakunywa uji na maziwa huku maziwa ya mama yakiwa kama nyongeza tu kwa kisingizio cha "hashibi". Ila kwa kushinda na rafiki yangu niligundua tatizo lake, anaweza kunywa chai asubuhi na asile tena mpaka saa tisa mchana. Kwa maana hiyo mtoto ananyonya breakfast (Kipande cha mkate labda na mayai mawili) kwa masaa zaidi ya sita. Baada ya hapo anaweza akakaa tena mpaka saa mbili/tatu ndo ale tena. Hapo kitatoka kitu cha maana kweli?! Obviously not. Na sio yeye tu, kuna binti jirani yetu mtoto wangu na wake walipishana wiki tu kuzaliwa lakini kwenye ukuaji wamepishana kama vile wamezidiana mwaka mzima.

Binafsi siamini kwenye kula sana na kula vyakula vyenye mafuta mengi wakati wa uzazi. Na ile imani ya kwamba ugali,wali,maharage,cabbage,dagaa na vyakula vingine kama hivyo sio chakula cha mzazi sio kweli. Kila kitu kinalika na kila kimoja kina faida yake.

Ujanja ni kula portion ndogo ndogo kila baada ya masaa machache. Mf. Saa 1 CHAI na mayai mawili au na vipande viwili vya mkate, saa 3-4 kabakuli kadogo ka uji, saa 6 supu kidogo, saa 8 lunch (wali, ugali,ndizi,viazi, spaghetti, chapati za maji n.k), saa 11 matunda yoyote yale yanayopatikana kwa kipindi hicho au salad, saa 2 chakula cha usiku alafu basi. Katikati ya usiku ukisikia njaa kunywa chai/kikombe cha maziwa au juice labda na kipande cha mkate. Hapo hata ukimaliza uzazi hutoki umenenepa kama tembo na mtoto atakuwa mwenye afya tele.
3. Waajiriwa/waliojiajiri.

Mkamulie mtoto maziwa yahifadhiwe ili apewe kwa muda ule ambao haupo. Maziwa ya mama yanaweza kuhifadhiwa kwenye friji na mtoto akapashiwa kidogo muda wake wa kula ukifika. Pia, panga ratiba zako vizuri, kama uwezekano wa kurudi nyumbani mchana upo basi rudi unyonyeshe pia kuhakikisha mtoto wako yuko salama.

Kwa kuongezea tu, Maziwa ya ng'ombe ni mazuri kwa afya lakini sio kwa mtoto chini ya mwaka mmoja. Na sababu ni kwamba yana protein na madini zaidi ya ambavyo mwili wa mtoto mchanga unavyoweza kusaga. Pia minerals na vitamin zilizopo kwenye maziwa ya ng'ombe sio kiasi kile ambacho mtoto anahitaji. Ndo unakuta mtoto anakuwa na upungufu wa madini ya chuma ambayo inaweza kupelekea mtoto kupata anemia which is serious.

So, kuweni wazazi wazuri, kuleni vizuri (vyakula, matunda na mboga za kila aina) mnyonyeshe. Wababa wasaidieni wake/wazazi wenzeni kutimiza wajibu huu kwa kuwajali muwafaidishe watoto wenu.
 
bora uwakumbushe maana siku hizi wanajifanya usasa umewatawala,hawanyonyeshi tena,wanaogopa ziwa kulala wakati liliwekwa kwa matumizi ya mtoto na sio baba(baba wanadandia tu chakula cha watoto)
 
Kama kawaida yangu naangalia kitu kwa jicho la tatu...
Muwe mnapima afya zenu mara kwa mara...
Maana ung'ang'anie kunyonyesha huku mumeo mzinzi mtoto apate maambukizi toka kwa mama...

Na ukiona mtu hataki kunyonyesha mtoto wake mumuwache...
Wengine wameathirika...kuuliza uliza na kuwashangaa shangaa kunawafanya wajisikie vibaya...
Haya mambo ni very private...

Kuna rafiki yangu huko Mghana...alijifungua kipindi huko kwao kuna kampeni ya mama kunyonyesha mtoto...
Anasimulia ilikuwa worst experience kwake...
Alikuwa analetewa mtoto amnyonyeshe huku maziwa yana vidonda (alilazwa baada ya kujifungua)...sikilizia maumivu yake na usalama wa afya ya mtoto...

Mwili wangu...mtoto wangu...nani aniamulie...
 
WORD!, faida kubwa kwa Mtoto na mama, wamama keep in mind you loose baby weight like nobody's business!
 
Breastfeeding is special moment for mother and child to bond.

Nilienjoy sana ku breastfeed and I cannot wait to hold another little one in my arms and feed him for two years God willing.
 
Kama kawaida yangu naangalia kitu kwa jicho la tatu...
Muwe mnapima afya zenu mara kwa mara...
Maana ung'ang'anie kunyonyesha huku mumeo mzinzi mtoto apate maambukizi toka kwa mama...

Na ukiona mtu hataki kunyonyesha mtoto wake mumuwache...
Wengine wameathirika...kuuliza uliza na kuwashangaa shangaa kunawafanya wajisikie vibaya...
Haya mambo ni very private...

Kuna rafiki yangu huko Mghana...alijifungua kipindi huko kwao kuna kampeni ya mama kunyonyesha mtoto...
Anasimulia ilikuwa worst experience kwake...
Alikuwa analetewa mtoto amnyonyeshe huku maziwa yana vidonda (alilazwa baada ya kujifungua)...sikilizia maumivu yake na usalama wa afya ya mtoto...

Mwili wangu...mtoto wangu...nani aniamulie...

Umenichekeshaje Mkuu...
 
Kukosa maziwa ya kumnyonyesha mtoto au kuwa mepesi hiyo ipo. Ila isikufanye ukasema kuwa usinyonyeshe mtoto.
Changamoto iliyopo ni kwa waajiriwa imagine maziwa ya shida eti uyakamue utakamua nini.
La kufanya ni mungu tu atuwezeshe.
Nawaongelea wale wamama wa kweli
 
Mie kabla sijachukua mimba nilikua nawaza kwanza kuongezeka uzito stretch marks, kubwa maziwa yangu, lakini nilipokua na mimba tafran Za mimba nilipo Za twins Wangu Kwa ile furaha sikujali maziwa kuanguka wala nini na kama mnavyojua watoto wakiume wanavyo nyonyaa nilikua nakula ile mbaya nimenyonyesha Mpaka pale walipo anza vijino wakawa wananitafuna nikasema sasa wameshaa shiba, uzito nimejihidi kupunguzaa ila nido ilikataaa kabisa Kurudi Saa 6 kamili kama mwanzo, lakini am so proud to be a Mother, mwenyezi mungu anikuzie, na Alikua Hana mungu ampe inshallah...
 
nyumba kubwa hao ni exceptional na nnafahamu sana uwepo wao. Mimi nimezungumzia wale wasio na sababu za msingi zinazopelekea wao kukwepa ama kushindwa kunyonyesha inavyotakiwa.
 
Last edited by a moderator:
Kama kuna mtu hajaelewa hapa atakuwa na matatizo, tatzo la wadada wa siku hizi kunyonyesha hawatak et wataaribu kifua au matiti yatashindwa kubustika
 
nyumba kubwa hao ni exceptional na nnafahamu sana uwepo wao. Mimi nimezungumzia wale wasio na sababu za msingi zinazopelekea wao kukwepa ama kushindwa kunyonyesha inavyotakiwa.

nimekuelewa...hao watakuwa wale wa mimba za ujanani...anataka kuzaa lakini bado iatwe binti...(maziwa yasilale)
Lakini kama ulipanga kabisa kuwa na mtoto, afu usiwe proud kumnyonyesha utakuwa na matatizo....
 
miezi 6 maziwa ya mama tu...hayatoshi!!!
...
Hilo la miezi sita...ya mama tu ...kwa wengi ni ndoto hasa wafanya kazi...
Kukamua maziwa si shuguli ndogo...ni ya kusikia tu kwa wengine...
Mimi nilinunua mashine...nikajaribu nikashindwa...
Nikasema liwalo na liwe...nanyonyesha nikiwa around...
Afu mimi nina kinyaa...the fact kwamba hayo ni majimaji toka mwilini...eti nikamue afu niweke chupani...no....
 
Kukosa maziwa ya kumnyonyesha mtoto au kuwa mepesi hiyo ipo. Ila isikufanye ukasema kuwa usinyonyeshe mtoto.
Changamoto iliyopo ni kwa waajiriwa imagine maziwa ya shida eti uyakamue utakamua nini.
La kufanya ni mungu tu atuwezeshe.
Nawaongelea wale wamama wa kweli
Hahahaa eti utakamua nini.
Maziwa yapo bana, ni kiasi cha kula na kunywa vizuri. Alafu huonagi wengine wanaenda kazini blouse zinalowa maziwa wakati mtoto hapati, siyakamuliwe hayo ili hata mama nae awe confortable?!

Mtama kwa watoto hongera mwaya. Watoto wa kiume wanakamua haswa, wangu kafikisha miaka miwili ila ndo kwanza utamu wa nyonyo umekolea vizuri. Siwezi ku-imagine wangekuwa wawiwili.

Anyway, uzito gani umekataa kuondoka?! Wa mwili?! Kama ndo huo na umeshaacha kunyonyesha anza kupunguza chakula unachokula taratibu na mazoezi kidogo hata ya kutembea tu utapungua.

Mie kabla sijachukua mimba nilikua nawaza kwanza kuongezeka uzito stretch marks, kubwa maziwa yangu, lakini nilipokua na mimba tafran Za mimba nilipo Za twins Wangu Kwa ile furaha sikujali maziwa kuanguka wala nini na kama mnavyojua watoto wakiume wanavyo nyonyaa nilikua nakula ile mbaya nimenyonyesha Mpaka pale walipo anza vijino wakawa wananitafuna nikasema sasa wameshaa shiba, uzito nimejihidi kupunguzaa ila nido ilikataaa kabisa Kurudi Saa 6 kamili kama mwanzo, lakini am so proud to be a Mother, mwenyezi mungu anikuzie, na Alikua Hana mungu ampe inshallah...
 
Last edited by a moderator:
...
Hilo la miezi sita...ya mama tu ...kwa wengi ni ndoto hasa wafanya kazi...
Kukamua maziwa si shuguli ndogo...ni ya kusikia tu kwa wengine...
Mimi nilinunua mashine...nikajaribu nikashindwa...
Nikasema liwalo na liwe...nanyonyesha nikiwa around...
Afu mimi nina kinyaa...the fact kwamba hayo ni majimaji toka mwilini...eti nikamue afu niweke chupani...no....
halafu yataka usafi wa hali ya juu kumkamlia mtoto maziwa...ukikosea kidogo tu umemlisha mtoto uchafu
 
miezi 6 maziwa ya mama tu...hayatoshi!!!

Kwanini yasitoshe?!

Mama akijitahidi kula vizuri anatengeneza maziwa ya kumtosha mtoto mpaka anashiba kabisa kama we mtu mzima ulokula sahani ya ugali ukashushia na maji.
 
Mie kabla sijachukua mimba nilikua nawaza kwanza kuongezeka uzito stretch marks, kubwa maziwa yangu, lakini nilipokua na mimba tafran Za mimba nilipo Za twins Wangu Kwa ile furaha sikujali maziwa kuanguka wala nini na kama mnavyojua watoto wakiume wanavyo nyonyaa nilikua nakula ile mbaya nimenyonyesha Mpaka pale walipo anza vijino wakawa wananitafuna nikasema sasa wameshaa shiba, uzito nimejihidi kupunguzaa ila nido ilikataaa kabisa Kurudi Saa 6 kamili kama mwanzo, lakini am so proud to be a Mother, mwenyezi mungu anikuzie, na Alikua Hana mungu ampe inshallah...

....out of topic, hii avater yako inanichekesha nikajuaga wewe ni ME!
 
Back
Top Bottom