Kununua/ ku Invest au kununua share Jamii Forums

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
wakuu
naona ni muda muafaka wa jamii forums kujitanua kibiashara zaidi baada ya kuwa na members zaidi ya 50,000
sasa nilikuwa nawaza kama wamiliki wakiamua kuuza share zao au kutafuta investors au kuiuza kwa makampuni makubwa kwa ajili ya kuboresha utendaji kama
makampuni mengine ya nje yalivyofanya hapa naongelea makampuni kama
youtube
skype
myspace

n.k
mimi najitolea kuwa mmoja kati ya watu ambao aidha watainunua, au wata invest kwa kiwango kikubwa au nitanunua shares kwa kiwang kikubwa na
nahshauri wanununuzi watoke humu humu ili tuwe na mtandao wetu wenyewe na hii itasaidia members wa jf kuwa wamiliki wa jf

nawasilisha
 
  • Thanks
Reactions: LAT
unataka kununua share nyingi ili uwe moderator .... ha haa haaa
 
hapana mkuu mimi ni mtu wa kuwaza profit mbele nitawaweka same moderator ila nitakuja na ideas ambazo zitafanya kampuni ku gain profit kwa kiwango kikubwa
 
WAZO ZURI SASAO WAKUU WA JF WAJE HAPA WATUPE MPANGO KAZI WAO LABDA WANA IDEA ZINGINE AU KAMA HIZI LETS WAIT

heshima mbele GT
 
Sahau hiyo kitu. Kwanza usidanganyike, JF members hawafiki hata elfu kumi. Kwa hesabu za haraka tu kila member ana ID zaidi ya tano na kuendelea. Tafakari fanya utafiti.
 
Mi nina ID moja tu, tano zote za nini ili ubishane mwenyewe au za nini hebu niambie mkuu ili na mimi niongeze tatu.
 
Sahau hiyo kitu. Kwanza usidanganyike, JF members hawafiki hata elfu kumi. Kwa hesabu za haraka tu kila member ana ID zaidi ya tano na kuendelea. Tafakari fanya utafiti.

Mkuu torabora wewe unazo id ngapi?
 
Nimeangalia profile yako wewe C.T.U unaonekana ni mnafiki,kwanza wewe hauna nia njema na JF kama ulivyoeleza hapa wewe hata sh 10 ujachangia JF ndio maana sio Premium member,pili hilo wazo lako unataka JF iingie mikononi mwa mafisadi hili ife,wazo lako ni mgando kama unataka kuipaisha JF changia bwana hatutaki porojo! HPP
 
Wazo lako lingeheshimika sana kama ungekuwa JF Premium Member, kama sasa huchangii hata kumi...nini kitakusukuma kununua hisa?
 
C.T.U,

JF inachangamoto ya kuweza kujibadili na kujiendesha kibiashara bila ku compromise thana nzima ya "Where we dare to talk openly". Sasa tukiingiza elemet ya biashara ya kuuza shares, watu watakimbia hapa.
 
Nimeangalia profile yako wewe C.T.U unaonekana ni mnafiki,kwanza wewe hauna nia njema na JF kama ulivyoeleza hapa wewe hata sh 10 ujachangia JF ndio maana sio Premium member,pili hilo wazo lako unataka JF iingie mikononi mwa mafisadi hili ife,wazo lako ni mgando kama unataka kuipaisha JF changia bwana hatutaki porojo! HPP
Kwani kutokuwa premium member ndio unafiki?
Kwani hao mafisaDi wakitaka kuinunua jf Ni lazima wapitie kwa kwangu
Mbona watanzania hatupendani kwa kila jambo ambalo linaonyesha mwenzako atafaidika haya basi wewe ndio utakuwa na hisa nyingi haya umefurahi??
 
C.T.U,

JF inachangamoto ya kuweza kujibadili na kujiendesha kibiashara bila ku compromise thana nzima ya "Where we dare to talk openly". Sasa tukiingiza elemet ya biashara ya kuuza shares, watu watakimbia hapa.
Hapana mkuu ni kuwa yale yale yaliyoanzishwa na moderators yataendelezwa ila kutakuwa na ideas tu ambazo zitalenga kwa ajili ya kuingiza profit zaidi
 
Ndio tuanze sasa kuongelea hizo ideas gani za kuingiza profit.

mkuu Mike tuliomba kuwa na subjukwaa la ujasiliamali siku nyingi sana pasipo na mafanikio baadhi ya madai tulijadili kwenye link hapo chini (naomba uyasome) naamini kwako hakuna linaloshindikana.

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/233530-zifanyeni-kuwa-sticky.html

https://www.jamiiforums.com/complai...ali-ndani-ya-business-and-economic-forum.html

Turudi kwenye mada jinsi ya kuingiza profit JF: Mkuu Mike JF itaingiza faida kubwa kwa kuongeza hadhi ya forum yenyewe i.e taarifa muhimu zitakazopatikana humu mfano taaarifa za jinsi ya kujiajiri, kilimo, mifugo, unanzashaji wa biashara etc taarifa za namna hii zitawavuta watu wengi na sponsors... ambao wengi wao huwa hawataki kujihusisha na mambo ya siasa.
Wale watakaotaka JF ifungwe kutokana na uchochezi, majukwaa haya yenye kuisaidia jamii yatatumika kuilinda JF.

Tafadhari pitia hizo links utusaidie kupata kajukwaa ka ujasiliamali maana kuna nondo zimewatajirisha watu kupitia JF business forum
 
mkuu Mike mimi natoa ahadi ya kuwa balozi wa JF, nitatumia uwezo wangu kuwashawishi sponsors waje hapa JF kutangaza biashara zao
 
Na haya ndio tunaotaka kutoka kwa great thinkers
Safi sana mkuu tuendelee na katika chakato huu kuliko sisi tuanzishe website nyingine badala ya jamii forums ni vyema tukawekeza humu humu
 
mkuu Mike tuliomba kuwa na subjukwaa la ujasiliamali siku nyingi sana pasipo na mafanikio baadhi ya madai tulijadili kwenye link hapo chini (naomba uyasome) naamini kwako hakuna linaloshindikana.

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/233530-zifanyeni-kuwa-sticky.html

https://www.jamiiforums.com/complai...ali-ndani-ya-business-and-economic-forum.html

Turudi kwenye mada jinsi ya kuingiza profit JF: Mkuu Mike JF itaingiza faida kubwa kwa kuongeza hadhi ya forum yenyewe i.e taarifa muhimu zitakazopatikana humu mfano taaarifa za jinsi ya kujiajiri, kilimo, mifugo, unanzashaji wa biashara etc taarifa za namna hii zitawavuta watu wengi na sponsors... ambao wengi wao huwa hawataki kujihusisha na mambo ya siasa.
Wale watakaotaka JF ifungwe kutokana na uchochezi, majukwaa haya yenye kuisaidia jamii yatatumika kuilinda JF.

Tafadhari pitia hizo links utusaidie kupata kajukwaa ka ujasiliamali maana kuna nondo zimewatajirisha watu kupitia JF business forum

Narubongo,

Hili tumelifanyia kazi.

mkuu Mike mimi natoa ahadi ya kuwa balozi wa JF, nitatumia uwezo wangu kuwashawishi sponsors waje hapa JF kutangaza biashara zao

Tunashukuru sana kusikia hivo. Na pia tuanze kujenga kwa pamoja jukwaa letu ya Ujasiriamali

Hapana mkuu ni kuwa yale yale yaliyoanzishwa na moderators yataendelezwa ila kutakuwa na ideas tu ambazo zitalenga kwa ajili ya kuingiza profit zaidi

C.T.U

Huu ndio wakati wa kuongelea hizo ideas mpya za kutuletea profit. Tuanze kuzijadili hapa alafu tunaangalia way forward.
 
Back
Top Bottom