Kununua GARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kununua GARI

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Soparino, May 9, 2012.

 1. S

  Soparino Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina best yangu ambaye alikuja kwangu kuniomba nimtafutie MTEJA wa GARI yake. Alikua na shida sana Kwani alikua anaumwa. Kwa Kua wateja ni shida nikaona njia raisi ya kumsaidia ni kuinunua Mimi mwenyewe. Tukaelewana nikampatia pesa akanipatia GARI na file yake, baada ya wiki moja akanijia anaomba mwisho wa mwezi huu anirudishie pesa yangu nimpe GARI yake.
  Wadau hebu shauri hili swala.
   
 2. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kama vp mrudishie halaf akupe cha juu.
   
 3. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,681
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Atalkuwa alibanwa tu, mwambie akupe interest ya lets say: 20% of the total value umpe, maana una haki ya kumwambia hapan, akikataa interest usimpe gari bwana. Kwani angeuza kwa mwingine lingerudi?
   
 4. Jephta2003

  Jephta2003 JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2008
  Messages: 3,586
  Likes Received: 1,888
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa umesema ni rafiki yako mrudishie gari lake akupe hela yako
   
 5. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lipeleke suala hili kwenye jukwaa la sheria kujua mambo ya mikataba ya kuuziana magari.
   
 6. T

  TUMY JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo nayo kali ila nionavyo mimi, kwanza naamini anakuomba na si kukulazimisha ama kukushurutisha kwamba upokee hela kwani katika hali ya kawaida hana haki ya kukulazimisha, sasa ni wewe utumie busara zako tu na kwa kuwa unasema ni mshkaji wako unaweza ukalitatua jambo hilo kishkaji pia.
  Hujatuambia umepita muda gani toka amekuuzia mpaka hapa anapokuja tena kukuomba umuuzie tena nasema hivyo kwani kama kuna muda umepita na kama gari bado liko katika hali nzuri basi bila shaka itambidi kukulipa na ka interest kidogo kwani inawezekana ulilikarabati kwa namna ya kuliboresha zaidi,huna haja sana ya kutaka kutengeneza faida kwani utu ni bora kuliko kitu alimradi amekuja kwa nidhamu na si ubabe na ukizingatia ni mshakaji na alikuwa na matatizo.

  Lakini upande wa pil iwa hilo suala inawezekana anaona kama ulimlalia sana unajua tena shida hazina adabu akajikuta amekuuzia kwa bei ya hasara sana sasa baada ya kupata nguvu ameona kukurudia tena na mara nyingi kama ana mawazo hayo mnaweza mkajikuta mnagombana kwani mara nyingi hapo suala la wivu linakuwa linamsukuma sasa kwa hiyo ni suala la pana kidogo ila mwisho wa siku tumia busara zako kwani details nyingi bado unazijua wewe.
   
 7. S

  Soparino Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikama wiki moja sasa, sijafanya ukrabati wowote, anaomba nimrudishie mwisho wa mwezi huu atakua amepata pesa. Kwa maana hiyo nitamsubiri kama wiki tatu hivi. GARI yenyewe ni Toyota corona siyo mzuri kiivyo na nimempa 3.5m
   
 8. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Rafiki wa kweli ni yule anayemjali rafikiye wakati wa shida na raha.Kama ulivyomjali awali ukampa fedha akakupa gari chukua tena chako na mpe gari bila ya longo longo lolote,Kwani ni Rafiki na amekuomba.Huu ni ushauri wangu uamuzi wa mwisho ni wako lkn ukifanya hili ninalokushauri urafiki hautaingia husda wala mikwaruzano utaimarika zaidi na huenda nawe iko siku shida ikakupata na akakumbuka hisani yako.
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kumbe hela za kununua gari mnazo ila za kusaidia ndo hamna Ok.
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Si ni rafiki yako? na aliuza kwa 7bu anashida? Hapo jaribu kumfikiria maana uhamuzi wowote utakaoamua utakuwa sahii
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama akiyajua ukweli ni huo huo kwamba haliwezi kurudi labda wafanye maamuzi tu ya kirafiki na siyo tofauti na hapo
   
 12. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Kwani wewe unataka kufanya nini? Ungetuambia unataka kurudisha au hutaki basi tukushauri.

  Je wewe unagari lako mwenyewe? Je rafiki yako hivyo sana hadi unakosa usingizi na kuuliza humu? Kama hamna urafiki ule wa sana unajua sana as naona ungemkopa kama mngekuwa karibu hivyo bila yeye kuuza gari.

  Jua huyo kashauriwa na mtu/watu aje aombe gari lake. Pia labda alijua atakufanyia hivi yaani mchezo huu usimwamini.

  Sasa pia unaweza test urafiki wenu mwambie nduguyo kalinunua toka kwako yupo mkoa mwingine, hapo utamsikia.

  Ila kuwa makini na watu wa namna hii, usi trust mtu sana katika urafiki. Kwa hiyo kuanzia sasa mwangalie. Usipompa anaweza kukuibia gari, au kuwapa tipu majambazi basi tu mkose wote.

  Pole nakuonea huruma as lazima ulishapangia kitu hilo gari, labda ndio lako moja kwa sasa. Mwingine ameshauri uende jukwaa la sheria ushauriwe.

  Tujibu tuzidi kukusaidia.
   
 13. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Nyie.c marafiki wa kweli! Km ungekuwa unampenda na kumjali rafiki yako ungemuazima pesa ya matibabu na c kununua gari yake!
   
 14. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Urafiki wa kweli ni kusaidiana kwenye mambo ya msingi chunguza kwanza kama hakwenda kuizalishia hela yako mrudishie gari lake akupe hela yako bila riba kwani ipo siku nawe utaitaji msaada toka kwake.
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa umesema ni rafiki yako, mrudishie gari akupe pesa yako. Ni vizuri kutengeneza SOCIAL CAPITAL kuliko FINANCIAL. Kumbuka leo ni yeye, kesho ni wewe. Chukulia kama hiyo gari aliiweka kama assurance ya kukurudishia pesa yako.
   
 16. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika hali ya kwawaida alingundua kabisa ngumu kumkopesha mil 3.5 bila yy kuweka dhamana yeyote, ndo maana alipata wazo la yy akuuzie gari.
  Mi naona mrudishie gari yako kwa kuzingatia:-
  1. kama hiyo 3.5 M ulikopa unatakiwa kuridisha riba mwambie ailipe.
  2. gharama zote ulizotumia wakati unalichukua kwake kama kuwalipa mashahidi nk anazilipa
  Ila yote hayo waweza kumsamehe kutokasna na ukaribu wenu
  NOTE leo kwake kesho kwako!" usinyee kambi"
   
 17. K

  Koola Member

  #17
  May 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa maelezo yako jamaa alitaka kuuza gari na wewe ukanunua.Sioni sababu za kurudisha kwani mtu yeyote angeweza kuinunua na isingewezekana kurudisha.Kwa sababu ya busara na urafiki unaweza kumpa gari yake na kuacha kununua gari za marafiki zako kwani huruma itakufanya ugombane nao.
   
 18. S

  Soparino Member

  #18
  May 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wakati Nanunua hii GARI , siyo Mimi pekee hata ndugu walishauri hivyo Kwani kimfaacho mtu ni Mali Yake na sio misaada pekee , huyu bwana siyo mchovu sana
  Kwani Ana GARI nyingine anayotumia sasa, ndo maana niliona Kama kuna katamaa ndani ya hilli swala. Kwa ubest na Mimi upo ila sio saana yaani katika Hali hii
  ngumu ya kiuchumi nimpatie m3 bila ya bondi. Ingekua ngumu
   
 19. S

  Soparino Member

  #19
  May 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo nilisaidia, yeye alileta issue hii kwa mabest baada ya kuona market ya GARI lake itachukua muda, akaomba nimtafutie Mteja nilivyona inakua ngumu kupata Mteja wa haraka Nae anashida nikaamua ninunue Mimi ingawa Sikua na mpango huo, baada ya wiki moja ndo akaibuka na swala hili. Hata hivyo Hana cash ni lazima nisuburi 3 weeks kuanzia sasa.
   
 20. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  nenda kwa Nduu zako wakushauri.
   
Loading...