kununua gari kutoka Zanzibar

don-mike

Member
Apr 3, 2011
50
0
Mwenye uzoefu na hili wandugu.

Nahitaji kununua gari ya kubeba mizigo (i.e canter). Nikinunua gari kutoka Zanzibar na kuja kulitumia hapa bara ntatakiwa kulilipia ushuru gani?
Je kuna chochote ntatakiwa lipia endapo ntataka kulitumia bila ya kubadilisha jina na kulisajiri bara?

Asante.
 

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,401
2,000
Kuna uzi ulielezea hili vizuri sana.
Zanzibar ni nchi inayojitegemea,sasa ushuru wake upo chini,hapa hata milioni tano tu unapata Suzuki Carry safi kwenye Yard na unakula raha duniani,ila ukiipeleka Dar basi lazima ulipie Difference ya kodi,yaani kodi ya hapa Zanzibar unatoa kodi halisi ya bara ambayo ipo juu.Au kwa Tafsiri nyingine unajazia tofauti ya Kodi kwa Bara.
Halafu ni muhim sana kubadilisha Jina,kwanini unakuwa mvivu kwa haki yako,sasa mwenye gari akisema umemuibia?
Kubadilisha Jina kwa Zanzibar ni rahisi sana,kama sikosei kipindi cha nyuma ilikuwa Shilingi elfu hamsini,sijui sasa.Na hii wakala wako ndio anaifanya,na wakala mjanja ni siku moja kazi inaisha.Na gari linakuwa na jina lako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom