Mr. Bigman
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 2,560
- 1,299
Katika vyote madhara makubwa waliyoleta hawa kunguru weusi ni lile la kutikomeza ndege wa asili ya pwani. Karibu dsm yote kwa sasa haina tena ndege wa asili baada ya hawa kunguru kuletwa. Serikali inabidi ifanye juhudi za makusudi kuwatokomeza hawa kunguru weusi.
Hawajaletwa, wakuja hao.
Wakuu, nimekuwa nawaza mara kwa mara kuhusu jamii hii ya Kunguru ambao wamezagaa sasa karibu eneo lote la Pwani ya Tanzania,kuanzia Tanga hadi Mtwara. Jambo moja ninalolijua ni kwamba hawana asili ya Afrika. Wametokea India. One theory inasema walitua pwani ya Tz baada ya ku stow away ktk meli kubwa za kibiashara zilizofika Tz kutoka bara Hindi. Nyingine inasema waliletwa Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Sheikh Amani Abeid Karume alipofanya Ziara ya India in the late 60's. Alipewa zawadi ya kunguru kadhaa ili waje wazaliane as a control measure ktk mashamba ya karafuu kwani ndege hawa hula viwavi wanaoharibu zao la karafuu. Wakuu, maicologist na wanamazingira mliopo humu,hebu tujadili kama kuna faida na hasara za uwepo wa ndege hawa katika pwani ya Tz. Inasemekana wamewatimua aina ya ndege wengine wa asili katika miji yetu ya pwani,kwa ama kuwala wao wenyewe,makinda/vifaranga au mayai yao. Lakini pia ni maarufu kwa kukwapua sidiria , chupi, nepi na leso zinapokuwa zimeanikwa uani baada ya kufuliwa. Pia inasemekana wanakula uchafu jalalani hivyo wanaweza kutumika katika kazi za kusafisha mazingira ya miji. Lakini pia kwa nini wanaishi miji ya pwani tu? Je Dodoma, Arusha na Mwanza wanaonekana? Nawasilisha
Hao kunguru waliletwa. Kuna kipindi kilirushwa na itv kuelezea uwepo wao, ni muda umepita sasa lakini nakumbuka walisema hao kunguru waliletwa Zanzibar ili waje wale uchafu, huko walikotolewa kati ya India au Uarabuni walikuwa wanakula taka, walivyofika zenji wakaanza kula misosi badala ya taka, wakaasi na kuangua na kuongezeka wakasambaa ukanda wa pwani, ukaja mpango wa kuwaua na kila kunguru mmoja atakayeuliwa ni Tshs 50/- sijui kama bado hii kazi inaendelea
Mkiacha kuwa wachafu Kunguru watatoweka.
Mkiacha kuwa wachafu Kunguru watatoweka.
dawa ni kuwala , tufanye utafiti wanaliwaje ili wawe kitoweo maana nyama ya kuku ng'ombe haikamatiki, hata hivyo waziri Kamara aliulizwa jinsi ya kuwatomeza ngedele yeye akajibu dawa ni kuwafanya kitoweo ndio watakwisha.
dawa nyingine ni kwamba kwa kuwa kunguru hawa ni waoga sana mbinu mbadala ni kila mti walalapo unafunga puto wakae wanaelea pale hawawezi kukaa wala kuzaliana wanakaa na wasiwasi hivyo watakimbia wote huku tukiendelea na utafiti wa kuwa!!