Kunguru katua juu ya kichwa changu, nashauriwa niende Bagamoyo, ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunguru katua juu ya kichwa changu, nashauriwa niende Bagamoyo, ni sahihi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzizi wa Mbuyu, Mar 23, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Leo asubuhi nikiwa nasalimiana na mtu nje ya ofisi yangu, akaja kunguru na kutua juu ya kichwa changu.
  Kwa muda nikahisi ni mtu amenishika kichwani kwa mkono lakini ilinishtua kidogo maana yule mtu niliekuwa namsalimia alifunua mdomo wake kwa mshangao, nilipoweka mkono wangu kwa nia ya kumgusa Kunguru yule akaruka.
  Tukio hilo limeonwa na watu kadhaa waliokuwa jirani...
  Sasa kimbembe, mie nililipuuza jambo lile na kuona labda yule kunguru kachanganyikiwa kwa kula sumu mbalimbali majalalani hivyo akapata ujasiri wa kutua kichwani. Lakini watu walioona au kusikia jambo hilo wananijia na ushauri wa kwamba eti siyo bure, lazima lile ni jini/uchawi natakiwa kwenda haraka kwa Waganga wa kienyeji ili waniokoe......... wamekomalia na kutoa mifano lukuki hadi nimeanza kuogopa tofauti na mwanzo....
  Jamani nifanyeje?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  ni bora ukakimbilia kwa Mungu wako (kwa imani yako) kuliko kuenda huko kwingine kama hilo jambo linakusumbua, ni kweli si kawaida kwa huyo ndege kutua juu ya kichwa cha binadamu maana hana ujasiri huo, ila ni bora umuulize Mungu badala ya mganga
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Njoo Kwa YESU, kila jambo linawezekana!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mimi imewahi kunitokea..
  kulikuwa na kunguru ananifuata asubuhi kila nikitoka nyumbani..
  ni kweli inahusiana na ushirikina labda,kwani on my case
  nilikuwa na jirani washirikina na nilihisi labda wanahusika.
  huyo kunguru alikuwa ananifuata na nikuzubaa anakuja kunidonyoa kichwani...

  sasa ushauri wangu usiende bagamoyo wala kwa mganga.
  fanya sala sana,
  kama ni mkristu nenda kanisani kila asubuhi...
  kama ni muislamu usali asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako...
  ukifanya hivyo hakuna lolote baya litakalokukuta......
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ukienda kwa mganga wa kienyeji, atakusaidia kuweka majini mengine makubwa kuliko hilo lililotua juu yako, na si muda mrefu atakuvuta akutafune kabisa. kwa kifupi kwenu ninyi ambao si wazoefu wa mambo haya, (kwasababu sisi wengine mambo hayo tumeacha na kuokoka), ukienda kwa mganga wa kienyeji, lazima utoke na pepo walau mmoja, anakuvaa na wewe hautajijua. another thing which mganga anakufanya, akikutazama kwenye kamera yake akaona una nyota nzuri, anaiiba, atakuja kumwuzia mtu mwingine akija, tena kwa mkataba ambao yeye atakuwa anavuna fungu lake la kumi karibia kila baada ya muda flani, yaani pale utakapokuwa unatakiwa kwenda kurenew (kuweka mafuta gari), si mnajua! nafahamu wengi maofisini lazima wanakuwa na mganga wao ambaye anawatumikisha, wanapeleka pesa kila watakapoishiwa nguvu, siku ukija kuwa immune, nakuambia dawa zote zitagoma, majini yatakayokuwa mwilini mwako yatakuwa mengi kupindukia, na yatakutafuna.

  so, what you are going to do kwa mganga wa kienyeji, ni kwamba, ataenda kukuwekea jini kubwa kuliko hilo lililokuja kutua juu yako. hilo jini likichoka lazima litaanza kukusumbua either kwa magonjwa, kutafuna watoto wako etc hadi uende kwa mganga akalitulize na damu za watu au wanyama etc, au ataliondoa na kuweka kubwa kuliko hilo ambalo litampiga aliyeko ndani na kuwa mfalme juu ya mwili wako. utakuja kujua kuwa una MIFUGO mwilini mwako kama milioni hivi na inahitaji chakula. shetani atakutumikisha apendevyo kwasababu uko chini ya himaya yake.

  hatari zaidi, Mungu anakataza uchawi, Mungu amekuumba na anakupenda, ana wivu sana Mungu, huwa anapenda yeye tu aabudiwe, hivyo unapoenda kwa mganga wa kienyeji badala ya kwenda kwake, anasema atakulaani hadi kizazi cha nne, yaani, utalaaniwa wewe, watoto wako, watoto wa watoto wako, na watoto wa watoto wa watoto wako. just think about this!

  nakushauri, NENDA PALE UBUNGO, KUNA KANISA MOJA LINAITWA GLORY OF CHRIST, au nenda KULE MWENGE KWA EFATHA, au kule mbezi beach, au agape tv au kanisa lolote la kilokole wakakuombee BUREEE, haulipi chochote na dhambi utaepuka. kama utaamua kwenda kwa mganga badala ya kwenda kwa Mungu aliyekuumba na aliyeahidi kukulinda bure, hakika mabaya yatakupata mengi sana baadaye, kwasababu shetani haji ila kuua, kuchinja na kuharibu, pamoja na kwamba utaona kama shetani kupitia maajenti wake waganga wa kienyeji, anaweza kuwa anaonekana kwako kama anataka kukusaidia, kuokoa maisha yako, kwa kifupi anakunenepesha tu akisubiri siku ifike akuangamize kabla haujatubu dhambi uende motoni moja kwa moja. Mungu na akusaidie.
   
 6. father-xmas

  father-xmas JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 530
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mkuu usiende huko nguvu za giza!jikabidhi kwa mungu tu!
   
 7. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ila kwa kifupi, hicho kilichotua juu ya kichwa chako, mzee ni kitu ambacho si cha kuchukulia juu juu, kama kweli unachosema kimekutokea ni kweli. chukua step kabla mambo hayajaharibika, pengine wameshakuwekea tarehe kabisa, kimbilia kwa mungu.
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Nshukuru mkuu, lakini nikikaa mwenyewe tu nikaomba kwa imani Bwana wa Majeshi si atanisikia?
  Kweli jambo hili limeni shake kiaina.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  nenda church au msikitini...
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Ni tukio la kweli kwa 100%, ah, maisha haya nimekosa nini kustahili matakataka haya?
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  atakusikia sawa lakini hiyo ni vita....hakuna vita anayoenda mwanajeshi mmoja...hutashinda ukiwa peke yako, hata vitani kuna mtaalamu wa vifaru, mashinegun,mabomu etc.....hata ulimwengu wa roho upo hivyo hivyo
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  what doesnt kill u.makes u stronger.......
   
 13. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Umenipa elimu mpya, ubarikiwe.
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  duniani kuna vingi vya kustaajabisha!mtegemee mungu hakuna kilicho zaidi yake!
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  imekutokea mara ngapi? ulimuua kunguru? kama imetokea mara moja inaweza kuwa bahati mbaya tu na endelea kuomba dua zako za kila siku kwa Mungu akuepusha na mabalaa yoyote.
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sikutanii, sisi sote tulikuwepo huko misri miaka ya nyuma, nakwambia hicho kitu si cha kawaida. hauwezi kukaa home na kupiga maombi tu, usichezee shilingi ******, huo ni uhai wako, nikiamua kukupa semina hapa, haitaisha leo juu ya mambo hayo yanavyofanyika. si ajabu kama kweli unachosema ni sahihi, wameshachukua nyota yako kichwani na mambo yako yakianza kuharibika utavaa kandambili na kutembelea daladala, unaweza kukosa hata nauli ya daladala. SI KILA MTU ANAWEZA KUTOA PEPO. na huyo anayekwambia nenda msikitini, huko ndo wanaenda kujaza kabisa. NENDA PALE UBUNGO, mdogo wangu alikuwa na tatizo kubwa la ajabu, ameenda pale, wale waliokuwa wanamloga wamepigwa na Mungu hadi wameamua kuokoka kabisa. kwenye uhai usichague kanisa, najua inaweza kuwa pengine hautaki kubadili dini, just try only for this, halatu utakuja kuniambia. kama utasubiri uombe mwenyewe hapo, hakuna daktari anaweza kujitibu. KAMA SHETANI ALIVYO NA MAAJENTI WAKE, HIVYO NA MUNGU ANAO WAFUASI WAKE SPECIAL, HAO NDO KAMA YULE JAMAA PALE UBUNGO, EFATHA, FENANDIS, MUNUO NA WENGINE WENGI. pale wanapiga maombi na hata nyota iliyoibiwa inarudi laivu, pale wanaharibu kalenda, vitabu vya kichawi ambavyo maadui zako wanaweza kuwa wameshakuandikia kukupangia tarehe, wanateketeza mitego, wanaharibu kabisa hata kama wameshakuzika wakati bado unatembea, kuna wachungaji kibao pale ukifika ukaeleza tatizo lako watakushambulia na nakwambia utakuja hapa kuniandikia msg. na mambo yako mengine ambayo hujaandika hapa yatanyoka. mimi nilienda pale baada ya kuona mdogo wangu yamemnyookea, nimesali pale na karibia nitakuwa mchungaji pia. si siri wakubwa, usichezee. na wengine wote wenye tatizo kama hili, njooni BUREEE.
   
 17. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Nimekusikia mkuu, ila hapo penye red pasije kubadili mjadala huu.
   
 18. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  unajua haya mambo yapo sana!
  mimi wakati nasoma,siku 1 wkt narudi shule kufika getini kwetu niliona kitu cha ajabu,nikaingia ndani nikamueleza mama yangu na ndugu,sasa kwa vile sisi ni familia yetu haiamini kabisa haya mambo wakanicheka na kudai eti nina njaa ndo maana naona mauzauza!nikajitahidi sana kuwashawishi lakini wapi,kila ninayemuelezea hadi leo haniamni.
  hata hivyo mi niliingia ndani nikasali sana kwa sbb niliingiwa na woga,hadi usiku nilikuwa naamka nasali, kilichotokea ni kwamba baada ya mimi kuona vile haukupita muda mrefu siku moja kukawa na kitoto kinachotambaa cha ndugu yangu kilikuwa kinacheza hapo getini kikaanza kuvutana na kamba nyekundu iliyokuwa imejitokeza,ndo mama yangu kuja akataka kuivuta kuitoa ili isije kuwaangusha watu wakipita ndo alipoivuta ikatoka na kichupa kina maandishi ya kiarabu,mahirizi na matakataka ya ajabu!
  watu wa kanisani wakaja tukafanya nao maombi,jamni alitokea mama mmoja wa jirani anawataka watu wa kanisani waondoke eti akadai wanapiga makelele akaanza kutukana ile mbaya na wala hatukuwahi kugombana naye wala nini tukabaki kumshangaa maana alikuwaga mstaarabu tu!
   
 19. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  you never know pengine huyo anayekwambia alikuwa huko na anafahamu anachoongea. kwenye mambo hayo ningekuwa profesa. lakini Bwana Yesu ameniokoa. asante Yesu wangu kuniondoa kwenye uchafu.
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  hivi we ni mgonjwa wa akili au vipi?
  nimenyamaza naona unazidi vipi unawashwa??????
  nimesema very clear aende msikitini kama yeye ni muislam
  na kama mkristo aende kanisani.
  kipi kilichokukera hapo?
  unajishaua kama mshiriki wa urembo,grow up stupid wewe...
   
Loading...