Kunguru hafugiki?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,959
Reaction score
828,684
Wahenga walishafanya mengi wakapitia mengi, wakajifunza mengi na hatimaye wakapata uzoefu mkubwa kwenye changamoto walizokutana nazo!
Mojawapo walilokutana nalo ni kwenye ufugaji wa wanyama mbalimbali
Imagine wanasema hata mnyama hayawahi kabisa kama fisi anafugika lakini si kunguru
Kunguru ni mbishi
Kunguru ana kiburi
Kunguru ni mjuaji
Kunguru Ana dharau pia
Ila hana maarifa pia japo anajiona ana akili sana.. Ni mwepesi kushawishika hata katika mambo ya kijinga kabisa..

Cha kuchekesha sasa pamoja na yote hayo lakini ni mwoga sana na anaweza kukimbia hata kivuli chake mwenyewe.. Na ndio maana kuna usemi unasema kunguru mwoga hukimbia/hukimbiza bawa lake mwenyewe

Mwingine ni kenge.. Kenge pia ana kiburi sana na si msikivu kabisa! Hapokei wala hakubali maonyo yoyote mpaka limkute jambo.. Kutokana na tabia zake hizo ndio wahenga wakaja na usemi usemao.. Kenge hasikii mpaka damu itoke masikioni.. Yaani apigwe apigike!

Maisha ni maonyo na tahadhari.. Wenye kuonya huwa na sababu kamili ya kufanya hivyo.. Waliopokea maonyo waliepuka madhila mengi, aibu nyingi na tabu nyingi
Kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio
Mafunuo ya hafrey hayakuzingatiwa...!
 
kunguru ndiyo moja kati ya ndege/wanyama intelligent klk wote duniani ukiondoa binadamu, sema tanzagiza hakuna meritocracy hivyo watu hawathamini intelligence na ndio maana intelligence ya kunguru inaonkekana kama ni kero badala ya kuwa jambo la kustaajabisha na kujifunzia, unaweza kufanya na kujifunza mengi sana kutoka kwa kunguru kama binadamu ...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…