Kunena kwa lugha kwa kuiga kulivyoshusha hadhi ya ulokole

Wakati Yesu anaondoka aliwaahidi wanafunzi wake kuwaletea msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu.

Na kama ilivyokuwa ahadi za Yesu ni kweli ilipofika siku ya Pentekoste akawashushia Roho Mtakatifu.

Na hapa ndipo kunena kwa lugha kulipoanzia.

Roho Mtakatifu ni nani, ni mwalimu na ni msaidizi wetu, ukiomba kwa kumshirikisha Roho yeye huugua na kutuonbea kwa baba kwa kuwa sisi hatujuib ukuonba ipasavyo.

Roho Mtakatifu anazo karama 9 na hizi ni baadhi ambazo Roho humjalia mtu nazo ni
Ni Unabii, Mwalimu, Unjilisti, Miujiza, Uponyaji , Imani nk 1Wakorintho 12:14.

Sasa wengi wao hawajui kwanza kazi za Roho Mtakatifu wao ukifika wakati wa kuomba huiga kuomba sawasawa na wengine wanakosea...

Sababu huwezi kuwa umeshukiwa sawasawa na mwenzio...

Nasio Kila mtu hishukiwa na Roho Mtakatifu ila yule aliyeokoka...

Hii imefanya watu kutowaelewa wanaomba Nini na kumfikia hatua watu kushindwa kuendeleza kusali katika makanisa.

Ikumbukwe kuwa mtu haneni lugha kama apendavyo yeye bali kama Roho Mtakatifu anavyopenda yeye Matendo 2:4..
Pia imefanya wakati mwingine Ulokole kuonekana ni kama Uchizi Fulani.

Na ambao wako huko hawajielewi kabisa, hii pia ni sababu ya watu wengi kuiga kuwa wameokoka lakini hawajaokoka.

Lakini wamevaa kivuli ambacho hujiita wao wameokoka lakini sio kweli.

Mungu atusaidie tumjue

Wengi hasa wanawake wanaojiita wameokoka hupigwa NDIZI sanaaa!
 
Back
Top Bottom