Ewe Mkristo, nani alikwambia kukusanyika kila Jumapili kwa ajili ya Ibada?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,626
Salam, Shalom!!

Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili kama siku kuu ya IBADA badala ya Jumamosi iliyovyokuwa awali?

Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,

Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli, hivyo muda wowote waweza kuwa Ibada.

Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI, hivyo kuabudu Siku Kwa kujiita wasabato Si sawa!!

Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili kama siku kuu ya ibada takatifu badala ya Jumamosi?

Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?

Ni nani aliyebadili siku kuu ya kukusanyika Kwa Ibada Kutoka Siku ya Saba ya juma, kwenda siku ya kwanza ya juma,jumapili?

Ni nani aliyekuagiza kusherehekea sikukuu ya Christmas tarehe 25 DECEMBER?
Unalo andiko?

Ni maagizo ya Roho mtakatifu kufanya mambo hayo?

NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.

ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.

Askofu Kilaini amebainisha wazi alipofanya mahojiano na DW kuhusu utata wa papa kubariki mashoga, ametanabaisha kuwa, Jumapili imeanzishwa mwaka wa 300 AD kuendelea sikukuu ya kumuabudu mungu jua.

SOURCE: OLE... MNAOTETEA JOKA KUABUDU JUMAPILI- UTUBE VIDEO, UNYAKUO TV.

Karibuni.🙏
 
Jumapili ni siku ambayo sio siku ya kazi. Ni nzuri kwa kukutana kutafakari maandiko na kutiana moyo sisi kwa sisi na kufanya ibada kwa pamoja.

Kusali ni muda wowote siku yoyote na mahali popote. Maana ni kuwasiliana na Muumba.
Umesoma andiko lipi likuelekezalo kuwa Jumapili Si siku ya KAZI?
 
Umesoma andiko lipi likuelekezalo kuwa Jumapili Si siku ya KAZI?
Hapa siongelei biblia naongelea uhalisia wa dunia ya sasa ulitaka tukutane pamoja kujifunza na kutafakari neno la Mungu jumatatu?

Paulo alilositiza tu tusiache kukutana pamoja. Haikutajwa siku. Ni nyie wenyewe kupanga ratiba.

Hata ww na wasabato wenzio mnaweza kuamua kukubaliana kukutana jumatatu.
 
Mimi ukiniuliza kwanini nafanya kusanyiko Jumapili nitakujibu kwasababu Jumapili ni siku ambayo serikali yetu imefanya siku ya mapumziko ya kazi hivyo tunapata muda kama kanisa (viungo) kukusanyika pamoja kwa utulivu.
That's my big reason.
Kuhusu ibada , ibada ni maisha ya mtu, so nakuwa na ibada rohoni niwapo kazini, kwenye mafunzo, nyumbani na barabarani.
Kwahiyo kama nchi yetu ingesema mapumziko ni Jumatatu I hope ibada za pamoja zingefanyika Jumatatu.
Any question?
Mkristo yeyote kama kuna siku ataitukuza kuliko siku nyingine huyo ni mchanga kiroho anastahili maziwa hata kama atapewa cheo kikubwa kiasi gani huko kanisani kwake
 
Unawauliza Wakristo tena.
Kwani Wasabato sio Wakristo?

Sisi huku Dubai tunakutana na kufanya ibada siku Ijumaa.

Kwakuwa ni siku ya mapumziko ya Serikali ya huku.

Ila ibada za kijumuiya na kifamilia zinafanyika siku yoyote Kanisani au Nyumbani kwa mwanajumuiya panapotokea nafasi ya muda,
Pamoja na Jumamosi.
 
Hapumziki?
20230930_013345.jpg
 
Wakristo hao uliowataja muda mwingi wako rohoni, si jumapili tu wanakutana hata siku nyingine kufanya ibada. Hii kukutana jumapili ni desturi tu, jumatano, ijumaa hukutana kwa ibada muda wa saa kumi jioni. Jumatatu, jumanne, alhamisi na jumamosi pia wapo kanisani muda wa jioni. Kumbuka pia kuna ibada za usiku pia, na huo usiku hutegemeana na wakeshe au waishie saa nne usiku jinsi watakavyoona ni vema. Siku hizi watu hawashindi sana muda mwingi kanisani kutokana na kuchalenjiwa huwa wanafanya kazi muda gani? Wapo wa jumapili tu katikati ya wiki huwaoni wako bize na kazi zao. Wale wa rohoni huendelea kufanya ibada hata huko walipo hawasubiri kukutana jumapili tu.
 
Nimeshiriki kwa kusoma maana katika ulowataja simo

NB:hii ya kusema leta maandika ili kudhibitisha jambo flani ina apply kwenye mambo yote?i mean u halali wa kusema leta maandiko unaletwa na nini au nkitaka kubishana tu naweza kutumia kama ndo uhalali wenyewe
 
Hapa siongelei biblia naongelea uhalisia wa dunia ya sasa ulitaka tukutane pamoja kujifunza na kutafakari neno la Mungu jumatatu?

Paulo alilositiza tu tusiache kukutana pamoja. Haikutajwa siku. Ni nyie wenyewe kupanga ratiba.

Hata ww na wasabato wenzio mnaweza kuamua kukubaliana kukutana jumatatu.
Mimi Si msabato,

Wasabato Si wakristo.
 
Salam, Shalom!!

Ni Kweli, Yesu alituagiza kuwa "Tusiache kukusanyika" wapi alisema tukusanyike Jumapili?

Ibada na kutafakari neno la Mungu ni muda wote, mchana na usiku,

Na Ibada Takatifu ni Ile ifanyikayo katika Roho na Kweli.

Na Mungu hufanya KAZI muda wote, hata sasa afanya KAZI.

Mungu anakuuliza Ewe Mkristo kupitia thread hii, ni nani aliyekwambia kukusanyika Jumapili Kwa ibada takatifu?

Ukiulizwa andiko utalitoa wapi?

NB: Mkristo aulizwaye swali hili ni yule aliyeokoka, aliyebatizwa Kwa maji mengi na Kwa Moto wa Roho Mtakatifu, yule aaminiye juu ya karama Tano, unabii ukiwemo, aaminiye juu ya kunena Kwa lugha, aliyefunguliwa macho ya Rohoni na kuisikia sauti ya Roho mtakatifu wazi WAZI.

ANGALIZO; Hii Si mada kuhusu Ukristo kama DINI, Bali Ukristo kama IMANI juu ya Yesu Kristo na maisha matakatifu.

Karibuni.🙏
Na tuliambiwa tusikusanyike Jumapili?
 
PAULO KATIKA MOJA YA NYARAKA ZAKE ALISISITIZA WATU KUKUSANYIKA SIKU YA KWANZA YA JUMA, KUFANYA MATOLEO.SIKU HIYO NI JUMAPILI.WASABATO KUKUSANYIKA SIKU YA SABA YA JUMA NI UTAPELI.
Lete andiko la Paulo katika nyaraka zake kuelekeza waamini kukusanyika siku ya kwanza ya juma!!
 
Back
Top Bottom