Katika jamii yeyote yapo makundi mbalimbali, kuna wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi na vijana wasio na ajira, wengi wakiwa ni wale wanasubiri kuajiriwa.
Katika utawala wa rais Magufuli makundi yote hayo ambayo ndio wapiga kura ameyaumiza kutokana na maamuzi yake ;
Wakulima, kundi hili limeumizwa sana kutokana na zuio la kuuza mazao nje, matokeo yake bei ya mazao yao ikashuka na wengi wakapata hasara, kundi hili halipati ruzuku ya pembejeo kama zamani, lakini kubwa ni jinsi kundi hili lilivyoumizwa kwenye suala la korosho, katika awamu hii kundi hili limebaki kuwa duni.
Kundi la pili ni hili la wafanyabiashara, katika awamu hii biashara imekuwa ngumu sana tofauti na awamu iliyopitia, wafanyabiashara wengi wanabambikiziwa kodi kubwa isiyoendana na mapato halisi ya mauzo, kiwango cha manunuzi kimeshuka sana, hali iliyowafanya watu wafunge biashara zao.
Kundi lingine ni wafanyakazi, kundi hili lina miaka minne bila nyongeza ya mishahara, mbaya zaidi wamezuiwa kuhama, ongezeko la makato toka bodi ya mikopo, wengi wana hali ngumu sana.
Kundi la mwisho ni vijana waliomaliza vyuo mbalimbali wakisubiri ajira, kundi hili wapo wengi sana lakini hawana matumaini, kutokana na ukweli kwamba serikali ya awamu hii imeshiindwa kuweka sera nzuri za kutengeneza ajira kwa vijana.
Tujiulize ni kundi gani sasa ambalo litamchagua rais huyu tena?