Kundi dogo linaiba na linaifilisi nchi na kuiacha utupu!!

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Wakuu wana jamvi bila shaka hamjambo!
Kama ilivyo ada hili ni jukwaa la great thinker sidhani kama ni other wise ! Kwa wakati huu ninapo andika haya kuna kundi dogo la watu wako kwenye mkakati wa kuiba na kudhulumu kwa nguvu saana wakikadiria muda uliobaki ikiwezekana wa wao kubaki kwenye madaraka!!!
Makusudi ya hili bandiko hapa ni kukufanya wewe Mtanzania mzalendo uweze kufikiri nje ya mzingo ( think beyond the perimeter), kundi hili linalojidai ni wana siasa wanadhibiti njia zoote za uchumi na utawala wa nchi hii!! Wameshikilia dora, kuanzia bunge, polisi, mahakama na vyombo vyote vya usalama!!
Nawaomba ndugu zangu hebu tufikiri nje ya ulingo tuliozungushiwa!! Tumewekwa kwenye kapu fulani eti ni siasa, eti dini, eti ni vyama vya siasa yoote hiyo ni kutufunga ili tupoteze malengo ya kujikwamua kwenye mikono yao ya ufisadi!!! Tumefungwa kwenye box, hawa watu wamepoka utawala wa nchi kupitia chama, wamekaa juu sasa wanatawala kila kitu, waniba bila kizuizi chochote, kuanzia kwenye serikali, migodi, gesi sasa, mikataba wanayoitaka wao, hadi kusafirisha wanyama hai!!!
Kwa hiyo inatubidi tusipumbazwe na hila zao, wanaleta sera za udini wana acha tugawanyike waendelee kufanya maovu yao, eti tugombanie kuchinja wao waendelee kufunga mikataba ya kuiba na kujinufaisha na mabillion ya dola!! Wanafanya watoto wetu mataahira ili wa kwao wasome kwenye shule za viwango, wakifeli shule eti wanalekebisha waendeleze ujinga kwa watoto, wanajenga himaya yao ili waendeleze utawala wa kifisadi!!
Kundi hili limepoka nchi kwa wizi kwenye kivuli cha siasa, fikiria ni serikali gani wezi wanasamehewa eti warudishe fedha walizo ibia taifa!!
Kumbe kuna tabaka la wezi wateule, na wezi uchwara!! Wezi wa EPA wanatamba mitaani, wezi wa RICHIMOND na DOWANS sasa wanataka kugombea Uraisi, BAADA YA MUDA WA MWENZAO KUISHA!!!
Waziri mkuu anasema eti tukiwakamata hao mafisadi nchi itayumba, kweli sisi bado tuna imani kuwa tunayo serikali makini???Hapo ndugu zangu sio dini wala siasa, wala kabila, maana wote sisi ni Watanzania, tunaelea kwenye nchi moja iliyopokwa na wezi wakitawala kwa mabavu kama tunavyoona kule Mtwara!!
Kwa nini mikataba ya GESI isiwekwe wazi kwenye bunge, magazeti, habari, ili tuone kama ina manufaa kwa nchi yetu???Hayo madeni wanayo ingia na kulimbikiza atayalipa nani???
Lazima tufikiri nje ya box, wanataka tufuate mkondo kama maji wanachimba mitaro ya udini, vyama, kabila ili tuelekee wanako taka tuende!! Tusikubali!!! Tanzania ni yetu bila kujali dini , kabila au chama cha siasa, woote tupigane kwa focus beyond the fence, out of the box, ili tuweze kujikomboa, tunaibiwa woote, tunadhurumiwa woote!!
Wenzetu wachache wanajilimbikizia mali, wanaficha fedha Uswiss, na sasa wamehamia uarabuni nadhani wamefungua ACCT zao huko!!!Ni lazima tupambane nao, wanajaribu kuzima mbinu zoote za kijikomboa, kama mnavyo ona, kila mahali, Media, kujieleza, kuandamana kudai haki!!
Ni lazima nchi yetu ikombolewe toka mikono ya mafisadi!!!
Tuepuke ushabiki kama wanavyotaka tufanye na kufuata!!
Nawasirisha!!
 
Kuna watu wanautaka sana urais wa nchii hii...lakini sioni kama wana kitu kipya cha kutoa...2015 tukilala tu..tumeliwa milele..
 
Hawa jamaa, tusipowatoa 2015, tumekwisha.
Hawa jamaa Mkuu wamekamata kila kona, yaani ni system, halafu wamewekana kila mahali, Waziri wa elimu anaboronga anaambiwa ajiudhuru anakataa mpaka aliye muweka amtoe!!
Watu wanaiba na kuboronga wanahamishiwa kwenye vitengo nyeti, toka afya hadi TRA, kweli tutafika???


 
Mkuu Mtumishi wetu, Ki-ukweli post yako imenifanya nidondoshe machozi hasa ninapo tafakari juu ya mstakabali wa vizazi vijavyo.

Lakini kinacho tia matumaini ni hiki hapa " Haijawahi na haitatokea utawala dhalimu ukadumu milele "; Hivyo basi ni jukumu letu sote kusambaza elimu ya uraia kwa kasi ya ajabu ili kuwapatia watanzania ukombozi wa kifikra, na wakisha jitambua mabadiliko yatatokea automatically.
 
Na hao watu wachache wanaishi dar upande wa kulia mwa barabara ya ally hassan mwinyi,na new bagamoyo kuanzia bibi titi mpaka unafika bagamoyo, upande wa kulia haswa wilaya ya kinondoni
 
Na hao watu wachache wanaishi dar upande wa kulia mwa barabara ya ally hassan mwinyi,na new bagamoyo kuanzia bibi titi mpaka unafika bagamoyo, upande wa kulia haswa wilaya ya kinondoni
Sawa Mkuu umepatia wengine wametapakaa mikoani ni wakubwa kama miungu, wanauwa wanapiga mabomu wanakuweka ndani hata bila kosa!!
Watasingizia ni uchochezi, wapo wengi tuu wamewekwa na mkubwa!!!

 
Hawa jamaa Mkuu wamekamata kila kona, yaani ni system, halafu wamewekana kila mahali, Waziri wa elimu anaboronga anaambiwa ajiudhuru anakataa mpaka aliye muweka amtoe!!
Watu wanaiba na kuboronga wanahamishiwa kwenye vitengo nyeti, toka afya hadi TRA, kweli tutafika???



Mkuu, nikukumbushe kidogo, Kanali Gadafi, Shekhe Sadam Hussein, Ndg Adolf Hitla, Shekhe Idd Amin Dada, Bw. Mabutu Seseseko, na Shekhe Hosni Mubarak, walikuwa na mitandao hatari, lakini leo hii wako wapi?
Hii inatufundisha ya kwamba, hakuna awaye yeyote chini ya jua anayeweza kuyashinda mapambano dhidi ya nguvu ya umma.
 
Dawa ya hawa ni siku pale Watanzania watakapo acha ubinafsi na kuungana kwa pamoja kudai haki ndani ya nchi yetu kwani nani asiye uozo uliofanywa na unaoendelea kufanywa na viongozi wetu?
Tatizo tumegawanywa na ndiyo maana inakuwa rahisi kutawaliwa kwani jaribu kuangalia kwenye maandamano ya kudai jambo lolote hata mfano kule Mtwara wengi waliojitokeza ni wale wa hali ya chini lakini majority wenye kazi wao wapo maofisin na wakitoka jioni wanapiga simu kuuliza "eti nija gani haina vurugu hawa jamaa wasije pasua gari yangu vioo"
Hili ndilo tatizo hofu, woga na mashaka yatatukula mpaka tuishe.
 
[/FONT]

Mkuu, nikukumbushe kidogo, Kanali Gadafi, Shekhe Sadam Hussein, Ndg Adolf Hitla, Shekhe Idd Amin Dada, Bw. Mabutu Seseseko, na Shekhe Hosni Mubarak, walikuwa na mitandao hatari, lakini leo hii wako wapi?
Hii inatufundisha ya kwamba, hakuna awaye yeyote chini ya jua anayeweza kuyashinda mapambano dhidi ya nguvu ya umma.
Kweli kabisa Mkuu, hawa ni swala la kujipanga tuu, mwisho wao unakaribia, pamoja na kupanga safu mpya eti wachukue Uraisi!!
Lakini Watanzania tuko macho, ila tusikubali kutenganishwa kwa misingi ya dini, ukabila sijui ukanda, hata kisiasa wote tuwe wamoja kwa lengo moja la kuwaondoa wakoloni weusi na mafisadi!!!

 
Watakao ikomboa nchi hii toka mafisadi hawa ni vijana pekee. Kilicho mbele yetu hivi sasa ni kuwafunda vijana wetu watambue umuhimu wa kuing'oa serikali dhalimu madarakani kwa sanduku la kura.
 
Watakao ikomboa nchi hii toka mafisadi hawa ni vijana pekee. Kilicho mbele yetu hivi sasa ni kuwafunda vijana wetu watambue umuhimu wa kuing'oa serikali dhalimu madarakani kwa sanduku la kura.
kwa kura ngumu mkuu,teknolojia ya kuiba kwa wino wa mchina ni balaa.unajua mwaka 2010 NEC walitoa tenda ya wino,kisha wakaifuta gazetini.wakanunua wino wanapojua wao
 
kwa kura ngumu mkuu,teknolojia ya kuiba kwa wino wa mchina ni balaa.unajua mwaka 2010 NEC walitoa tenda ya wino,kisha wakaifuta gazetini.wakanunua wino wanapojua wao
Kwanza ni lini NEC watabolesha daftali la mpiga kura???
Vijana wengi tangu uchaguzi uliopita wameisha timiza miaka 18 na zaidi inatakiwa wajiandikishe kupiga kura!!
Mkuu kweli nguvu ya vijana ni muhimu matokeo ya Kenya umeyaona!!!
Hiyo ya wino tutapambana nao kulinda kura zetu, katikati yao kutakuwa na supporters!!!

 
Hawa jamaa ni hatari kwa Taifa. Watoto na wajukuu na vitukuu vitatulaani sana tusipowaondoa 2015.
Mkuu inatakiwa watu wajue wezi wetu ni kina nani??
Nchi kama China zimefanikiwa kuinua uchumi wao baada ya kupambana na kuwashinda mafisadi, ukikamatwa China ni kunyonga hakuna mjadala!!!
Marekani walijitahidi kuweka vitengo mbali mbali vya kupambana na ufisadi, finally wakaweka FBI, ndani yake kuna vitengo tofauti, fisadi au mkwepa kodi akikamatwa anaozea jela!!
Tanzania inahitaji wazalendo kujitoa kupambana kuondoa huu uozo, ili tuweze kujikwamua kiuchumi, haiwezekani taifa tajiri kwa kila kitu eti tena ni masikini!!!
 
Back
Top Bottom